Uchaguzi 2020 Majimbo zaidi ya 11 ya mikoa ya Lindi na Mtwara hatarini kupotea

Kwi kwi kwiiiii. Huyu dikteta uchwara aliyenyang'anya korosho kwa kutumia jeshi akija ndo ataharibu kabisaa!!
Ukisema waling'ang'anywa unamaanisha nini?uhakika unao kuwa hawakulipwa?,kwa hiyo kangomba kununua korosho ikiwa shambani ni sawa ila Serikali kununua kwa bei ya 3000/= ni wizi kisa zilishukuliwa kwa jeshi.Na vipi mwaka huu hao wanunuzi wamefikia bei ya serikali ni nani mnyonyaji ,mnakurupuka sana bila kuchangamsha hata akili hilo swala lipo kisiasa mmezeshwa kombe na nyie ndio mnalipuka kama moto wa kifuu.
 
Ukisema waling'ang'anywa unamaanisha nini?uhakika unao kuwa hawakulipwa?,
Wengi Sana hawakulipwa. Walikuwa wakiporwa halafu wakienda kudai wanaambiwa kaoneshe shamba. Mtu akienda kuonesha shamba wanadai haliendani na kilo.

Ndiyo maana dikteta huyu ameogopa kwenda Kusini. Aende aone.
 
Atakwendaje wakati anadaiwa hela za korosho alizokwiba?
 
Mkuu aliahidi kuwapiga shangazi zao. Sidhani kabisa kama Mzee Baba anaweza kwenda kule kuipeperusha ilani ya chama chake, zaidi ya kumtumia VP ama PM wake. Spana zimekaza, na mtori unavyozidi kunyweka ktk sahani lkn ni bayana hakuna kipande cha nyama hata kimoja ndani yake.
 
Ahakikishe amekamata fedha zao za korosho mkononi ndipo atinge kule. Ahadi zimechokwa na Wanakusini. Pia asisahau wale Mashangazi wanamsubiri kwa hamu.
 
Ataenda kuwaambia nini kuhusu korosho? Usimponze mwenzako, we komaa tu mbunge mteule 😂
 
Kusini Kuna Moshi. JPM hawezi rudi huko
 
Kuhusu Mtwara Vijijini, Mama Ghasia ana hali mbaya sana yaan kama mwaka 2015 alipatia ushindi Mahakamani basi safari hii kura zake haziwezi kutosha kabisa.

Mama Ghasia amekataliwa mpaka kwao kijiji cha Naumbu, yaani ndani ya miaka mitano ametimiza ahadi ya kujengwa MADRASSA tu na haijaisha mpaka raia zimemkataa.

Kuna mdada mmoja hivi anaitwa Shamsia ndio ana asilimia kubwa ya kuchukua Jimbo. Ningekuwa mtu wa karibu wa Ghasia ningemshauri aende Nanyumbu tu akamsaidie kampeni mume wake.

Kuhusu Nachingwea, halina ubishi Dr. Mmoto wa CHADEMA anachukua jimbo mapema tu, pale angesimama Mwl. Masala angemsumbua Mmoto ila kwa yule wa CCM hatoboi.

Kuhusu Liwale, mama Mitambo na kundi lake wamechukia sana kubadilisha matokeo na kumoa yule wa CUF. CCM wana 9% ya kushinda lile Jimbo.

Lindi Mjini, Mchinjita ana uelekeo mzuri wa kuchukua jimbo. Kiowa kule BWEGE kama kawa anarudi mjengoni. Kwa Lindi labda Mchinga na kwa Nape na Majaliwa ambapo alifanya kila hila wapinzani wasifanikiwe kurudisha fomu.
 
Na bora tushinde
 
Mwenyekiti wenu alikwisha onja joto la jiwe alipofukizwa kule Ruangwa ikabidi akimbie bila kugeuka nyuma mwacheni akae mbali na wakulima wa Korosho alizopora mpaka walipwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…