Uchaguzi 2020 Majina 13,000 ya wagombea yamejadiliwaje kwa siku mbili?

Uchaguzi 2020 Majina 13,000 ya wagombea yamejadiliwaje kwa siku mbili?

Heater

Senior Member
Joined
May 28, 2019
Posts
168
Reaction score
350
Tufanye labda hawakulala wala kusinzia kwahiyo walitumia masaa 48.

Ukigawa kwa idadi ya wagombea, utapata majina 270 yalijadiliwa kila baada ya lisaa limoja.

Ukichukua majina 270 ukayagawa kwa dakika 60, utapata majina takriban 5 yalijadiliwa kila baada ya dakika 1.

Hii imenishangaza sana hasa baada ya kusikia Mwenyekiti wa CCM akikazia kwamba wamefanya tathmini ya jina kwa jina kwa muda wa siku mbili na Hivyo kuwa wamepitia majina yote 13000.

Naomba kuelimishwa iliwezekanaje, isije ikawa ni kudhulumu ushindi wa wale wasiowapenda
 
HAYO yalishachunguzwa/chujwa muda mrefu ndiyo maana kuna walioenguliwa kutokana na rushwa n.k hapo walikuwa wanathibitsha tu siyo ndiyo walikuwa wanaanza kujadiri huyu katoa rushwa huyu hajatoa huyu hafai
 
Tufanye labda hawakulala wala kusinzia kwahiyo walitumia masaa 48.

Ukigawa kwa idadi ya wagombea, utapata majina 270 yalijadiliwa kila baada ya lisaa limoja...
CCM wote walitoa Rushwa badala wafute huo mchakato warudie upya wameamua kuwachuja hao hao wanaccm waliotoa rushwa kwenye kura za maoni
 
Ya ccm tuachie ccm.. tunawaamini viongozi wetu..

Nyinyi endeleeni kujadiliana mwaka mzima

Mnatakiwa kutoa maelezo yanayoridhisha, Maana Ukisema tuwaachie wenyewe wkt mnahitaji kupewa ridhaa kuongoza nchi basi mm binafsi nitapigia mstari kwamba CHAMA kilichoshindwa kujiongoza hakifai kuniongoza,
 
Ya Ngoswe mwachie Ngoswe.

Tunaweza tukamuachia Ngoswe yaliyo yake...... lkn tukigundua kua yake yamemshinda basi hakutakuwa na shaka kwamba yataifa ataendelea kuvuruga tu , labda Ngoswe atueleze ata kwa ufupi alitumia formula gani?
 
Wametumia application ya upembuzi, mambo yamebadilika teknolojia inakua.
Kuna majimbo wamepita bila kujadili mfano ni jimbo la waziri wa fedha, waziri wa mambo ya nje waziri wa Sheria waziri wa uwekezaji waziri wa Nishati mkazi tokea chato na wengineo marafiki wa mtukufu, wamechambua majimbo machache ambayo mtukufu hana marafiki huko
 
ushaambiwa mwenyekiti anamajina yake mfukoni.
tufanye walijadili kwa majimbo 270
Kila jimbo dakika 10, then 270x 10 ni dakika 2,700 gawa kwa dakika 60 (1Hr) ni 45Hrs
45Hrs ni sawa na siku mbili bila kulala mfululizo.
wamewazaje?
kwa MACCM.
hakuna kinachoshindikana.
 
Haiwezi kusoma CV 5 kwa dakika moja?
na izo CV 5 kwa dakika tume assume hawajalala siku mbili kitu kisichowezekana Maana tukiweka ktk MASAA kumi na mbili kwa siku basi n CV 10 kwa dakika.
 
Kuna majimbo wamepita bila kujadili mfano ni jimbo la waziri wa fedha, waziri wa mambo ya nje waziri wa Sheria waziri wa uwekezaji waziri wa Nishati mkazi tokea chato na wengineo marafiki wa mtukufu, wamechambua majimbo machache ambayo mtukufu hana marafiki huko

MKuu usitete uongo, tumia akili ya kawaida tu ya kuombe MMAA!
 
Kama mtu ana uwezo kufanya kazi kwa weledi na ana uzoefu na kazi, hakuna haja ya kumuassess, Hata Kama ungekuwa wewe ni mtu maarufu kwa jambo fulani mtu akikuona unaenda kufanya jambo ambalo una uzoefu nalo hakuna mtu atakayedoubt, mfano ukimuona Lionel Messi kapewa nafasi ya kucheza kipindi Cha kwanza kwenye timu yake moja kwa moja unatambua aliyempa nafasi hiyo hajakosea.
 
Back
Top Bottom