Majina 19 yanayotajwa kuwarithi Halima Mdee na wenzake bungeni

Majina 19 yanayotajwa kuwarithi Halima Mdee na wenzake bungeni

Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake, kwangu ingependeza zaidi kumuona Hilda Newton bungeni.
Nami nikawa najiuliza someone Newton simwoni kwenye orodha...kumbe aitwa Hilda Newton.

Kila la heri kwake
 
Yule shujaa binti wa Muheza hayumo?

Yosepher Komba
A3D12176-9549-48A2-A007-EA28992D0A32.jpeg
 
Chadema wakikubali kupeleka wengine bungeni maana yake watakuwa wanahalalisha ule uharamia uliofanyika 2020, haya majina mnayookoteza huko kwangu naona ni usanii mtupu, sasa waamue wao.

Kama wapo tayari kudanganyika mwishowe waendelee kuchezewa akili na serikali ya CCM kwenye kila uchaguzi, au wabaki na msimamo wao wa kutoutambua ule uchaguzi hata kama itawagharimu kuikosa ruzuku.
Una hoja lakini inahitaji kujitoa mhanga sawa na kupanda juu ya ghorofa refu ukajiachi....
 
Sijaliona jina la Lucia M. Mlowe aliyekuwa mbunge wa viti maalum 2015-2020, na aligombea jimbo la Njombe 2020 kupitia CDME
 
Huyu Joyce Mukya sijawahi kumuona katika ujenzi wa Chama ila miaka yote anapeta tu, labda kwasababu anampa furaha mwenyekiti wetu basi acha tu aulambe
Acha umbeya wewe,huyu yupo nyuma ya keyboard' kwenye taasisi Kuna watu watu muhimu invisible"
 
Msihesabu vifaranga kabla kuku hajatotolewa
 
unamwacha Hilda aliye active kwenye Chama unampa Joyce,anafanyia siasa wapi huyu au uvunguni?
Active kwenye Chama wakati kichwani hakuna kitu.. Ataenda kuongea nini au kuchangia nini cha maana Bungeni??

Michango yake tu ya Twitter inajidhihirisha alivyo mtupu kichwani..
 
Sakata la kuvuliwa uanachama wabunge 19 wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) linaendelea kushika kasi baada ya tetesi zinazodai kuwa kuna uwezekano mkubwa wa chama hicho kupeleka majina mengine ya wabunge wa viti maalum ili kuchukua nafasi yao.

Majina yanayotarajia kuwarithi ni Catherine Ruge (Katibu Mkuu Bawacha), Sharifa Mohamed (Kaimu Mwenyekiti Bawacha), Suzan Kiwanga (Aliyekuwa mgombea jimbo la Mlimba, Morogoro) Grace Kiwelu, Joyce Mukya, Suzan Lyimo.

Wengine ni Devotha Minja (aliyekuwa mgombea jimbo la Morogoro Mjini) Upendo Peneza, Lucy Owenya, Rose Moshi, Rhoda Kunchela, Gimbi Masaba, Rose Mayemba, Aisha Luja, Husna Said, Nice Gisunte, Moza Ally, Dorcas Francis, Ruth Molle, Pamela Massay na Lucy Magereli.

Ungeweka heading ya tetesi. Kama ni kweli cdm watakuwa hawafanyi sawa kwa kuweka sura hizo hizo kila siku hata kwa viti vya dezo.
 
Una hoja lakini inahitaji kujitoa mhanga sawa na kupanda juu ya ghorofa refu ukajiachi....
Nitawashangaa Chadema kwa ukongwe wao na yote waliyopitia kama hawatafanya nilichoandika kisa ruzuku!
 
Back
Top Bottom