Majina haya yanatoweka kwa kasi katika Jamii

Majina haya yanatoweka kwa kasi katika Jamii

1. Sikudhani
2. Mwamvita
3. Chiku
4. Mwadhani
5. Sipati
6. Jualako
7. Ubaya
8. Havijawa
9. Havintishi
10. Hakai
11. Hazimala
12. Msichoke
13. Ongeza yako
Siku hizi mitaani kuna majina ya kisasa tu kama Janet, Happy, Ilham,Snura, Barkis, Barke, nk nk. Je ndiyo kuelimika au kuwa wa kisasa zaidi.
Siku hizi kuna "Kadinda".
 
Majina ya kiswahili mazuri bwana,
Nimemkumbuka sikudhani,mwamvita, havijawa, kuna kidawa, kashinde, mwamboni, mwanahamisi, mwanaidi,tatu pili.
Yeah. Ni kama ya kichaga nayo nayakubali sana. Upendo, Pendo, Eliapenda, Ngurelo, Mushi,
 
Mimi watoto wangu wote wanaitwa majina ya Kisambaa tu. Na idadi yao ndiyo hii hapa; wa kiume kuna Makange, Mweta, Kiango, Hiza, Hoza, Kihiyo, Mdoe, na Mtoi. Wa kike yupo Mboni, Nemghwa, Kidangu, na Matabu. Jumla wapo 12! 😇

Na mimi baba yao mzazi naitwa Tate Mkuu Shebughe!
kubabake...
Tafuta wa 13 uje umuite utopolo bila kujali jinsia☺️☺️☺️
 
1. Sikudhani
2. Mwamvita
3. Chiku
4. Mwadhani
5. Sipati
6. Jualako
7. Ubaya
8. Havijawa
9. Havintishi
10. Hakai
11. Hazimala
12. Msichoke
13. Ongeza yako
Siku hizi mitaani kuna majina ya kisasa tu kama Janet, Happy, Ilham,Snura, Barkis, Barke, nk nk. Je ndiyo kuelimika au kuwa wa kisasa zaidi.
Nitakupa jibu la kisomi.

Haya majina yalikuwa common sana katika maigizo ya TV, nyimbo na hadithi za vitabuni, na mara nyingi yaliendana na sifa mbaya. Kwenye hadithi na nyimbo ni kina Mwajuma, Asha, Havijawa nk waliokuwa machangudoa, wenye kuvunja ndoa za watu nk, wakati kina Mudi, Masudi nk walikuwa majambazi, vibaka nk.

Sasa hili lililetelea jamii kuanza kuyasusa majina haya. Wewe ukisikia wimbo au ukisoma hadithi ambapo Roza ni changudoa, utampa mwanao jina la Roza? Sasa hilo ndilo lililotokea, na jamii kuanza kutafuta majina yasiyo na madoa. Kuna nyimbo kama hizi zilizotia doa kwenye majina

Asha (usifuate mambo ya dunia) - Tabora Jazz
Masudi (amekuwa jambazi)- Dar International
Farida (kaiba vyombo nikiwa safarini) - Tabora Jazz
Tatu Said (kutoroka nyumbani) - OSS
Rukia (wamkubali mchumba ukiwa shule) - Urafiki Jazz
 
Back
Top Bottom