Majina, misemo na maneno kwenye khanga

Majina, misemo na maneno kwenye khanga

Ala! Kumbe!

Asante gari ya muhishimiwa

Asiyekujua hakuthamini

Atakae hachoki

Bahati ni upepo sasa upo kwangu

Chanda chema huvikwa pete

Chokochoko mchokoe pweza, binadamu hutamweza

Chokochoko si njema mchague la kusema

Dua la kuku halimpati mwewe

Dunia duara

Embe mbivu yaliwa kwa uvumilivu

Ewe Mola tuepushe na mahasidi

Fadhila za punda ni mateke

Fimbo la mnyonge halina nguvu

Fitina yako faida yangu

Haba na haba, hujaza kibaba

Halahala mti na macho

Halua ya lozi imemshinda mdokozi

Hasidi hana sababu

Hata tukibanana hapa atapata aliyejaliwa

Hata ukinichukia la kweli nitakwambia

Hata ukinuna buzi tumelichuna

Hodi hodi naikome mwaka ujao naolewa

Huyo kibuzi mwarika mtizame anavyojitingisha

Japo kidogo chatosha kwa wapendanao

Japo sipendezi kubembeleza siwezi

Je! iko namna?
 
Raha ya moyo wangu mimi kupendwa na wewe
Hakika nimesadiki paka hana urafiki
fadhila mfadhili mbuzi binadamu atakudhi
Panua paja mkwanja waja.
Nanai kama Mama.
Kheiri liwe roho zenu ziwatue.
Alie pewa kapewa.
 
-Umeshindwa kutakata mtono, utatakata bafuni??
-Unakwea mnazi na msuli babu??
 
800px-ASP-TANU_kanga.jpg
 
Back
Top Bottom