Majina niliyoyaona ndani ya Lodge ya Alafaya iliyoko Vikindu yameniacha mdomo wazi

Majina niliyoyaona ndani ya Lodge ya Alafaya iliyoko Vikindu yameniacha mdomo wazi

Habari wakuu.

Kama mnakumbuka niliwahi kuandika uzi juu ya ndoto yangu ya kuanzisha Lodge na nikaumba ushauri juu ya biashara hiyo ambayo Kwa mapenzi ya Mungu mwakani nitakua tayari kuifanya InshaAllah🙏🏼.

Sasa ktk harakati zangu za kufanya research juu ya biashara hii kuna mtu akanishauri nipite pite ktk Lodge kadhaa nione wenzangu wanavyofanya na akanishauri ktk Lodge nitakazopitia nisiache kufika ktk Lodge inayoitwa ALAFAYA iliyoko VIKINDU.

Nikamwambia why niende mbali kote huko?Akasema wewe nenda amini utajifunza mengi.Siku ya siku nikaenda hapo ALAFAYA nikajifanya mteja.Nilipofika hapo nikaelewa kwanini jamaa yangu alisisitiza niende hapo.

Ni ka Lodge fulani hivi kadogo dogo kenye mazingira tulivu na yenye kuvutia sana ndani na nje.Naweza kusema kwa wilaya nzima ya mkuranga hakuna Lodge Classic kama ile.Vipo vingi nimeiga na kuvifanya vizuri zaidi yao😀😀

Tuachane na hayo.Kilichonishangaza hadi kuandika huu uzi ni majina ya vyumba vya ile Lodge.Nimezoea kuona watu wakiandika room numbers au majina ya mikoa au wanyama ila huyu mwenye hii Lodge sijui aliwaza nini hadi akaweka haya majina.

Hili la haya majina sina uhakika kama ni la kuiga bado linanifikirisha😀😀😀

Jioneeni wenyewe kwenye picha wakuu🙃⬇️⬇️View attachment 3153877View attachment 3153878View attachment 3153879View attachment 3153880View attachment 3153882View attachment 3153889View attachment 3153890
Nimekuja fasta nikajua unaongelea majina ya kwenye kitabu cha wageni!
 
baadhi ya majina kama ameyaandika kwa ufasaha wa wahusika hayawezi mletea shida kweli..?
wanasheria mnasemaje hapa..?
Hakuna MTU duniani mwenye Haki miliki ya jina.Mf Wema au Dianna wako kila Kona duniani.kama utaenda kusajiri jina binafsi basi watakushauri kuwe na jina lifuatalo la ziada lisilo na ukakasi...
 
Grahams nazani unaona jinsi gani vijana wanajaribu ku brand biashara yako mkuu
Nimeona Mkuu, Kwa kweli nimejifunza kitu.

Nafikiri Siku Moja nitamweka Mapokezi Wema Sepetu ama Hamisa kwaajili ya Kuwavutia wateja wangu.

Najua wateja wangu wakihudumiwa hata matauro tu na hao watu japo Kwa Siku moja, wataenda kuhadithiana hivyo kuzidi kuja wengi Kulala kwangu 🤗
 
Sorry nilikuwa na mgeni

Unamilik guest wapi?

Wateja utapata kwa sababu wanafata huduma, ila kiukweli huwa walinzi wanakaa na number za wanaojiuza ukitaka wanakupa. So sioni tofauti hapo, hata hizi guest za kawaida zina watu silent wanajiuza
Worry out mkuu

Guest yangu bado iko kwenye mchakato mkuu.Nataka by mwakani Feb. hivi ianze kazi,

Nafikiria kulenga kutoa huduma nzuri waje watu kwa lengo la kufuata huduma nzuri na sio machangudoa ila yakfanyika
nyuma ya pazia hiyo huwezi zui ila kujua kabisa kuwa nahusika kuuza ngono nitakosa amani
 
Sorry nilikuwa na mgeni

Unamilik guest wapi?

Wateja utapata kwa sababu wanafata huduma, ila kiukweli huwa walinzi wanakaa na number za wanaojiuza ukitaka wanakupa. So sioni tofauti hapo, hata hizi guest za kawaida zina watu silent wanajiuza
Mkuu Gily Gru naomba siri mbili tatu za kufanikiwa ktk hii biashara ili siku nikifungua nisiyumbe🙏🙏
 
Back
Top Bottom