Majina ya Kiafrika mbioni kutoweka

Mnyakyusa unakataa kumuita mwanao Gwamaka au Lusajo. Unaona ni la mizimu ili tu umuite Sean Roberts?

Unakataa kumuita mtoto Mwamba ila unamuita Peter, ambayo kimsingi ina maana ileile.
 
Mfano Mimi Charles Joachim Elias manoni

Hapo ni kupambana surname origin isipotee
Mtoto wangu nimemwita Brian Charles manoni instead of Brian Charles Joachim Elias manoni.

Surname yetu ya manoni haito potea..

Majina ni ya kubuni 😅
 
Utumwa wa kifikra mbaya sana aseee.
 
Pale Makumbusho ya vita ya Majimaji Songea, mashujaa walionyongwa na wajerumani tarehe 27. 02. 1906 ni kama vile:

1. Mfuta Mkuzo Gama
2. Njoroza Mbamba Mbano
3. Mgendera Gama
4. Mahengo na wengine wengi sana.

Lakini leo hii, mjukuu wa Mbano au Gama anaona Mkuzo au Mbamba ni jina baya la mizimu.
Bora aitwe Peter au John, majina kama ya wale walionyonga babu zake kwa halaiki, ambao pia washakufa na ni mizimu vilevile.

Upumbavu ni kipaji.
 
Urithi wa kwanza uliobora kwa mtoto ni jina...

Wewe mwite Mashaka, Masumbuko, Gwandumi, Mayala au Anyosise, Kamala au Rugaba au Manka hakuna Shida.

Mwingine atamwita Happy au Joy,Marry, Joshua sawa tu...

Ila kumbuka Urithi ulio bora wa kwanza ni jina.
 
Mkuu, unadhani kwanini jamii zingine hazitumii majina yetu ya kiafrika, ila sisi tunatumia yao?
 
Mkuu, unadhani kwanini jamii zingine hazitumii majina yetu ya kiafrika, ila sisi tunatumia yao?
Hata Lugha zetu hawazijui

Siku wakianza kutumia Lugha itakuwa rahisi kutumia majina.

Unawezaje kumrithisha mtoto wako kipenzi zawqdi yake ya kwanza kwa kitu usichojua maana yake?
 
Hata Lugha zetu hawazijui

Siku wakianza kutumia Lugha itakuwa rahisi kutumia majina.

Unawezaje kumrithisha mtoto wako kipenzi zawqdi yake ya kwanza kwa kitu usichojua maana yake?
Sasa maana yake si unamuambia tu.

Hata ukimuita Mary, hawezi kujua maana ya Mary ni nini mpaka umueleze.
Kwanini usimpe jina la asili yake Kisha umwambie maana yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…