Majina ya Kiafrika mbioni kutoweka

Na kanisa lina operate kulingana na utamaduni wa sehemu husika
Kwa nchi ambayo wananchi wake wanajali tamaduni zao hawana hata haja ya kubadili majina ili kuwa wakristo
Hata msikiti haukulazimishi kubadili jina. Shida ni sisi wenyewe waumini mkuu
 
Majina ya kigeni ni utumwa, ushamba, ulimbukeni, ujinga na kudhani ndiyo ustaarabu. Hakuna kitu nakichukia kama majina ya nje. Mtu analazimisha kubana pua anapomwita jina la weupe, wakati wao wanatuona nyani, takataka tu. Ningekuwa na uwezo kuhusu majina, ningepiga marufuku mtu kuita jina la weupe, bila kujali dini. Dini mtu ajiamulie lakini sio jina. Mimi nina watoto 2 wana majina ya kibantu, langu, la kibantu na la babu yao pia.
 
Na yupo mmoja namfahamu ana watoto 6 wote amewapa majina ya kibantu. Na sio mzee ila bado ni wa makamo tu.
 
Yani hata hayo ya nje , ukimuita "Samsoni" hataki anataka "Samson" hali kadhalika "Saidi" hataki anataka "Said"

Hili jambo tumeshsfeli
 

Madhara makubwa yameonekana kwenye maeneo ambayo desturi za waarabu (wengine huita dini ya kiislamu) imeenea. Kwenye maeneo hayo siyo ajabu mtu akaitwa ally rajab Abdulaziz. Majina yote matatu ni ya kiarabu. Na hata kusalimiana kwao wanasalimiana kwa lugha ya waarabu.
 
Hata Lugha zetu hawazijui

Siku wakianza kutumia Lugha itakuwa rahisi kutumia majina.

Unawezaje kumrithisha mtoto wako kipenzi zawqdi yake ya kwanza kwa kitu usichojua maana yake?
Emu niambie nini maana ya majina,Trump,Frank,Fredy,William,Paul,Pascal,Charles,Charlie,Zephania,Gerlad,James,Steven,Robert?????
 
Swali zuri, embu tupe solutions?
Solution ni simple ni kama ambavyo serikali hufungia mambo ya hovyo katika Jamii.unapiga marufuku watu kutumia majina ya wazungu na waarabu.
Mtoto akizaliwa tu aandikishwe kwa majina ya kiafrika, na ndio yatumike ka.a Officials names.
 
Solution ni simple ni kama ambavyo serikali hufungia mambo ya hovyo katika Jamii.unapiga marufuku watu kutumia majina ya wazungu na waarabu.
Mtoto akizaliwa tu aandikishwe kwa majina ya kiafrika, na ndio yatumike ka.a Officials names.
Ni ngumu , nyaraka nyingi za serikali zipo kwa kizungu, ndo waje walazimishe watu watumie majina ya kiswahili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…