Mwakibinga,Mwakasege na Mwabulambo
Kiasili majina ya pili ya wanyakyusya ni tofauti sana na taratibu za kizungu.
Wanyakyusya hawarithi majina ya baba zao, wanaume wanarithi majina ya mashangazi, wana wanawake wanarithi majina wa mabibi zao upande wa baba. Tofauti tu ni kwamba wanaume wanawekewa "mwa" mbele ya hilo jina. Kwahiyo kama wewe ni mwanaume na dada yako anaitwa Ms Jane Kalinga, watoto zako wa kiume wataitwa Mr John Mwakalinga. Na kama mama yao alikuwa anaitwa Ms Anna Bulambo, basi watoto zako wa kike wataitwa Ms Amina Bulambo(bibi).
Na kwasababu wewe kama baba ulipata jina kwa shangazi yako sio ajabu kukuta baba surname anaitwa MwaAbc, mtoto wa kiume anaitwa surname MwaXyz na binti yako anaitwa surname anaitwa egh. Sema siku hizi watu hawafuati hizi taratibu, ndio unakuta Baba, Kijana wake wa kiume na wa kike wana surname zinafanana.
Kwanini waliweka utaratibu huo, nimewahi ambiwa kuwa hawakutaka majina ya watoto wao wa kike yapotee. Na ukiangalia, ni majina ya kiume ndio yanapotea, ya wa kike kwenye familia yanabebwa either ya watoto wa kiume(shangazi) au wa kike (bibi).