Majina ya maeneo Zanzibar yanavyoacha watu midomo wazi

Mzee Rufiji

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2024
Posts
261
Reaction score
395
Wengi hawajui kama Zanzibara hasa Unguja iliwahi kuwa na usafiri wa reli iliyojengwa mwaka 1905. Sauti na mlio wa treni hiyo ilipokuwa ikipita ikazaa jina bububu.

b29cd2b8e5707bedb4f608d5f8548aac
Barabara katika eneo la Bububu.

Hivyo bububu ni tanakali sauti yaani jina linalotokana na sauti ya kitu. Kama ilivyo sauti nyau kupewa paka/ nyau, ndivyo sauti ile ya treni ikipita relini bu-bu-bu ilivyozaa jina la eneo Bububu.

Mangapwani
Ni jina linalomaanisha pwani/ ufukwe wa mmanga au mwarabu. Eneo hilo kwa kuwa ni la pwani na lilikuwa likikaliwa na Wamanga yaani Waarabu, wazazi wa Kiafrika walikuwa wakiwakataza watoto wao kwenda kucheza maeneo ya pwan, wakiwaambia kuna Wamanga pwani, hivyo neno Mangapwani likazaliwa kumaanisha pwani ya Wamanga/ Waarabu.

Uzini
Inasemekana kuwa huko zamani wakazi wa hapo walitaka kulinda eneo lao, wakachimba mtaro kuzunguka eneo zima na kuweka uzi ndani ya mtaro huo kama ishara ya dawa ya kutambika.

Ikawa watu wakitaka kwenda hapo wanasema wanakwenda Uzini, huo ukawa mwanzo wa jina Uzini.

Mwembemchomeke
Nilisema awali kuwa wakazi wa Zanzibar walitumia utundi na ustadi wa hali ya juu kuyapa majina maeneo hayo. Moja ya jina ni mwembemchomeke lililotumiwa kama tafsida ya kuficha hali matendo ya utusitusi yaliyokuwa yakifanyika eneo hilo.

71ff2835c37a08f5c5acf2a973ec6896
Mwonekano wa sasa wa eneo la Michenzani.
Simulizi zinaonyesha kuwa eneo hilo lilikuwa na matukio mengi ya ubakaji na kwa kupunguza ukali wa lugha, wenyeji wakapaita hapo Mwembe mchomeke.

Kibanda maiti
Ni eneo lililopo Unguja shehia ya Nyerere. Jina hilo limetokana na awali eneo hilo kuwa na kibanda kilichokuwa kikitumika kuoshea maiti.

Kisiwa Ndui
Ni mahala ambapo simulizi zinaeleza kuwa watu waliokuwa na ugonjwa wa ndui walihifadhiwa.

Mchambawima
Ustadi mwingine wa lugha kwa Wazanzibari unajionyesha katika jina la Mchamba wima. Kilugha kuchamba ni kujisafisha hasa kwa kutumia maji, pindi mtu anapotoka kujisaidia tena akiwa amechuchumaa.

Sasa simulizi zinaonyesha kuwa eneo hili lilikuwa na maji mengi hivyo kuwalazimu wapita njia kukunja nguo zao wanapopita

Kitendo cha kukunja nguo hali ya kuwa wamesimama kikafananishwa na mtu aliyevua nguo na kuchamba akiwa amesimama.

Chuini
Inaelezwa kuwa eneo hilo zamani kulikuwa na bustani na jengo lililokuwa likifuga wanyama wakiwamo chui.

Unadhani ni majina haya tu yanayowacha watu midomo wazi? La hasha! Yako mengi sana. Mwananchi tumeanza, wengine wanaweza kuchimba zaidi kuhusu utamaduni huu wa utoaji majina katika visiwa hivi vya karafuu.

©Mwananchi
 
Vipi chura kiziwi? Hapo kale vyura walifanya nini mpaka wakawa hawasikii?
 
Vipi na kidoti,kikombe tele,kitope na mwanakwerekwe..??
 
-Mfereji maringo
-Makunduchi
-chokocho
-chamba wima
-kiembe samaki
-kiembe ladu
😁😁😁
 
[emoji2398]Mwananchi
Kuna kituo Cha daladala kinaitwa tobo la kati [emoji23][emoji23]
 
Hayo maeneo kabla ya hayo majina yalikuwa yanaitwaje?
 
Tuletee na chukwaani
 
Back
Top Bottom