Majina ya Mikoa, Wilaya, sehemu ndani ya Tanzania pia na maana yake

Majina ya Mikoa, Wilaya, sehemu ndani ya Tanzania pia na maana yake

Nachangia kama ifuatavyo:
1. Iringa. Asili: LIlinga (yaani ngome ndogo).
2. Ngara. Asili: Mti uloitwa MUNYINYA w'iNGARA,
3. Tabora: Asili; Ntoborwa (yaani chakula kitokanacho na viazi vilivyo katwa na kukaushwa.
4. Dodoma. Asili: IDODOMYA, (yaani Nchi yenye maji, inayodidimia).
5. Mwanza. Asili: mahali alipoishi Mzee (wa Kisukuma aitwaye Ngh'wanza). Kwa sasa ni eneo ilipo shule ya msingi Bugarika.
6. Songea; Jina la Chifu wa Kingoni aiywaye Songea.
7. Makambako: Asili; Neno la Kibena linalomaanisha MAFAHALi (Ng'ombe). Lilitokana na vita vilivyopinanwa kati ya Wasangu na Wabena. walizichapa kwa muda wa wiki moja hivi na hakuna aliyeshinda. walitoshana nguvu kama mafahali.
8. Changanyikeni. (Hii iko karibu na UDSM). Ni mahali palipokuwa PORI (enzi chuo kinaanzishwa). wakaanza kukaa "wasomi wa UD", wakaCHANGANYIKA na Raia.....
9. Dongobesh...Iko mkoani Manyara. Asili (Neno la Kibarabaig linalomaanisha Tembo Mweupe)...
10. Chato....Neno la asili ni UBWATO (Kikerewe/Kizinza) likimaanisha Mtumbwi. wazungu alishindwa litamka Vwema...
 
Peramiho ipo songea imetokana na neno la kingoni ambalo ni pegipelela mihu ambayo ina maana yanaporuhusu macho au mwisho wa macho kuona..
Na hii ilitokana na Mmishonari wa Kibenedikitini aliyeomba eneo la kuanzisha misheni. Alipoomba kwa Chifu akapewa eneo la Mbali. Msituni na pasipo na makazi ya watu. Alipopewa akauliza; Mpaka wa eneo ulilonipa ni upi? Akaambiwa: Pale macho yako yatakapoishia kuona...Kusema kweli: WALIJIMEGEA PA KUTOSHA!
 
1. Kibororoni nasikia ilitokana na wenyeji wa eneo hilo kushindwa kutamka kibao cha alama barabarani kilichoandikwa Kibo Road. Kwahiyo wao wakawa wanatamka Kibororoni!

2. Chekeleni huko Moshi. Hii ilitokana na wenyeji wa eneo hilo kushindwa kutamka vema kibao cha angalizo la njia ya Treini cha Check Train. Kwahiyo wao wakawa wanatamka Chekeleni!

Moshi hakuna sehemu inaitwa Kibororoni, wala Chekeleni. Pimbi!
 
Dodoma - Idodoma yaani tetemeko

Bariadi- Burying yard Hapo wakoloni walifukia Mali nyingi sana
 
Mbarali, linatokana na neno la kisangu barali lenye maana ya tambarale. Sasa kutokana na ukubwa wa tambarale yenyewe (barali) wakaita mbarali kwa maana ya tambarale kubwa.
 
1. Kibororoni nasikia ilitokana na wenyeji wa eneo hilo kushindwa kutamka kibao cha alama barabarani kilichoandikwa Kibo Road. Kwahiyo wao wakawa wanatamka Kibororoni!

2. Chekeleni huko Moshi. Hii ilitokana na wenyeji wa eneo hilo kushindwa kutamka vema kibao cha angalizo la njia ya Treini cha Check Train. Kwahiyo wao wakawa wanatamka Chekeleni!
Sio kibo road ni kibo alone
 
KILIMA (MLIMA)NJARO UNGU)yaani "mlima wa mungu"maana wachaga walioishi pembezoni mwa mlima huu,walikuwa wanauabudu wakiamini kuwa mungu yuko pale.
Hapana ilikuwa n kilima kyaro (kilima kirefu)
 
Mkoa wa kagera ulikua ukifahamika kama mkoa wa ziwa magharibi ulibadirisha baada ya vita ya kagera 1980
 
Back
Top Bottom