Majina ya Mikoa, Wilaya, sehemu ndani ya Tanzania pia na maana yake

Majina ya Mikoa, Wilaya, sehemu ndani ya Tanzania pia na maana yake

kweli hapa nikisima cha maarifa , ningeomba anaefahamu maana ya majiya ya mikoa ifuatayo
1. singida
2.katavi
3.kigoma
4.tanga
7.mara
 
Makalio. Kuna changu wa bongo muvi alikuwa anajitembeza mbele ya watalii akitikisa matako yake. Wale wazungu walivyomuona wakasema kwa sauti 'Carry on," yaani aongeze spidi ya kutikisa tako, ndipo neno la kalio likaanzishwa.
Haujatulia 'Jamaa Mbishi' hahahaha
 
Vizuri sana ila naomba unielezee vizuri hapo kwenye neno nyika mana sijaelewa na pia uniambie nchi ya Tanganyika ilichukua jina kutoka mkoa wa Tanga au jina la Ziwa Tanganyika?
 
Mabibo External. Mabibo ni matunda yatokanayo na mti wa mkorosho.
Hilo eneo lilikuwa linamikorosho inayotoa matunda(MABIBO).
Enzi hizo wakati wa vita vya ukombozi wa ( Msumbiji, Angola, Zimbabwe nk)kulikuwa na kituo cha radio hapo kwa ajili ya kuhabarisha mwenendo mzima wa mapambano na harakati zs ukombozi. Kituo hicho cha radio kilikuwa kinaitwa EXTERNAL SERVICE.
Kama tujuavyo, tukabatiza eneo na kupaita MABIBO EXTERNAL!
Na kule Salasala karibu na Green Acres kilikuwa na nini?
 
Tanzania mpaka sahivi tunashindwa ku document,sababu za majina za sehemu kuitwa "kwa jina fulani"
Wasomi wetu mbona mnatufelisha

Mfano Victoria pale lazima kuna sababu yake kuitwa vile...

Ova
 
Nachangia kama ifuatavyo:
1. Iringa. Asili: LIlinga (yaani ngome ndogo).
2. Ngara. Asili: Mti uloitwa MUNYINYA w'iNGARA,
3. Tabora: Asili; Ntoborwa (yaani chakula kitokanacho na viazi vilivyo katwa na kukaushwa.
4. Dodoma. Asili: IDODOMYA, (yaani Nchi yenye maji, inayodidimia).
5. Mwanza. Asili: mahali alipoishi Mzee (wa Kisukuma aitwaye Ngh'wanza). Kwa sasa ni eneo ilipo shule ya msingi Bugarika.
6. Songea; Jina la Chifu wa Kingoni aiywaye Songea.
7. Makambako: Asili; Neno la Kibena linalomaanisha MAFAHALi (Ng'ombe). Lilitokana na vita vilivyopinanwa kati ya Wasangu na Wabena. walizichapa kwa muda wa wiki moja hivi na hakuna aliyeshinda. walitoshana nguvu kama mafahali.
8. Changanyikeni. (Hii iko karibu na UDSM). Ni mahali palipokuwa PORI (enzi chuo kinaanzishwa). wakaanza kukaa "wasomi wa UD", wakaCHANGANYIKA na Raia.....
9. Dongobesh...Iko mkoani Manyara. Asili (Neno la Kibarabaig linalomaanisha Tembo Mweupe)...
10. Chato....Neno la asili ni UBWATO (Kikerewe/Kizinza) likimaanisha Mtumbwi. wazungu alishindwa litamka Vwema...
DODOMA hapo mmmh hayo maji
 
Ilala wakati wanakuja waarabu kutangaza dili walikua wanasema lailaha Illa llah mzalamu akashindwa akawa nasema ilala
 
Back
Top Bottom