Majina ya Mikoa, Wilaya, sehemu ndani ya Tanzania pia na maana yake

Majina ya Mikoa, Wilaya, sehemu ndani ya Tanzania pia na maana yake

Na hii ilitokana na Mmishonari wa Kibenedikitini aliyeomba eneo la kuanzisha misheni. Alipoomba kwa Chifu akapewa eneo la Mbali. Msituni na pasipo na makazi ya watu. Alipopewa akauliza; Mpaka wa eneo ulilonipa ni upi? Akaambiwa: Pale macho yako yatakapoishia kuona...Kusema kweli: WALIJIMEGEA PA KUTOSHA!
Walijimegea pa kutosha
 
Meli= Mails ( barua)
Enzi ya mkoloni pale Posta ya Zamani yalikuwa makao ya jeshi kwa ajili ya askari kwenda Burma.
Wakoloni wakipokea barua (mails) toka ulaya.
Na zililetwa na "Meli". Walipokuwa wakiona meli inatia nanga walikuwa wakishout"mails,mails, mails".
Sasa wamatumbi wakajua vile vyombo vilivyokuwa vinaelea majini baharini ni MELI.
Ndio asili ya neno Meli.
 
Dodoma - Idodoma yaani tetemeko

Bariadi- Burying yard Hapo wakoloni walifukia Mali nyingi sana
Hapana bariadi imetokana na neno baryadi, maana yake wanaokula usiku watu Wa kale pale walikuwa wanakula usiku ndo wakaitwa baryadi na ikawa bariadi.
 
Tanzania ipo mikoa, wilaya na sehemu tofauti tofauti na majina yake. Lakini huwa najiuliza haya majina yametokana na nini au ni kwa sababu gani waliita hivyo?

Kwa mfano Msasani nasikia ilitokana na mmakonde flani kushindwa kutamka Musa Hassan na kwa sababu walikuwa wanakaa wamakonde wengi basi wakaamua kupaita Musa-sani ile ' Ha' walishindwa kutamka na huyu mtu alikuwa maarufu. Hapo ndo msasani ikaanza kutumika.

Kilimanjaro-hii ninkutokana na mlima ulipo. Nafahamu Kilima ni Mlima, Sasa Njaro sijui yatokea wapi...

Je wewe wajua jina gani na historia yake!!! Twende pamoja sasa tueleweshane tuwe na kumbukumbu sahihi...

kuna mtu aliwahi kuniambia chanzo cha neno KILIMANJARO kuwa wenyeji wa mahala pale hasa vunjo, waliita "kilema kyalo" wakiwa na maana ya "kilima cha Mungu" sasa wazungu walipokuja, wao wakapotosha matamshi ya neno wakanza kuita kilima nnjaroo...Sasa na sisi tukasawazisha tukaanza kusema KILIMANJARO. Niliamini kwa uwepo wa eneo liitwalo KILEMA huko moshi vijijini kilipo chuo cha ualimu MANDAKA
 
Dodoma-limetokana na neno idodomya, maana yake sehemu ambayo tembo alizama, asili ya neno sijapata

Tosamaganga-limetokana na neno la kihehe likiwa na maana ya tupa mawe.
 
Meli= Mails ( barua)
Enzi ya mkoloni pale Posta ya Zamani yalikuwa makao ya jeshi kwa ajili ya askari kwenda Burma.
Wakoloni wakipokea barua (mails) toka ulaya.
Na zililetwa na "Meli". Walipokuwa wakiona meli inatia nanga walikuwa wakishout"mails,mails, mails".
Sasa wamatumbi wakajua vile vyombo vilivyokuwa vinaelea majini baharini ni MELI.
Ndio asili ya neno Meli.
[emoji3] [emoji3] [emoji3] asante
 
Mabibo External. Mabibo ni matunda yatokanayo na mti wa mkorosho.
Hilo eneo lilikuwa linamikorosho inayotoa matunda(MABIBO).
Enzi hizo wakati wa vita vya ukombozi wa ( Msumbiji, Angola, Zimbabwe nk)kulikuwa na kituo cha radio hapo kwa ajili ya kuhabarisha mwenendo mzima wa mapambano na harakati zs ukombozi. Kituo hicho cha radio kilikuwa kinaitwa EXTERNAL SERVICE.
Kama tujuavyo, tukabatiza eneo na kupaita MABIBO EXTERNAL!
 
Hapana bariadi imetokana na neno baryadi, maana yake wanaokula usiku watu Wa kale pale walikuwa wanakula usiku ndo wakaitwa baryadi na ikawa bariadi.

hiyo baryadi kabila gani
 
Makalio. Kuna changu wa bongo muvi alikuwa anajitembeza mbele ya watalii akitikisa matako yake. Wale wazungu walivyomuona wakasema kwa sauti 'Carry on," yaani aongeze spidi ya kutikisa tako, ndipo neno la kalio likaanzishwa.
 
Back
Top Bottom