Nachangia kama ifuatavyo:
1. Iringa. Asili: LIlinga (yaani ngome ndogo).
2. Ngara. Asili: Mti uloitwa MUNYINYA w'iNGARA,
3. Tabora: Asili; Ntoborwa (yaani chakula kitokanacho na viazi vilivyo katwa na kukaushwa.
4. Dodoma. Asili: IDODOMYA, (yaani Nchi yenye maji, inayodidimia).
5. Mwanza. Asili: mahali alipoishi Mzee (wa Kisukuma aitwaye Ngh'wanza). Kwa sasa ni eneo ilipo shule ya msingi Bugarika.
6. Songea; Jina la Chifu wa Kingoni aiywaye Songea.
7. Makambako: Asili; Neno la Kibena linalomaanisha MAFAHALi (Ng'ombe). Lilitokana na vita vilivyopinanwa kati ya Wasangu na Wabena. walizichapa kwa muda wa wiki moja hivi na hakuna aliyeshinda. walitoshana nguvu kama mafahali.
8. Changanyikeni. (Hii iko karibu na UDSM). Ni mahali palipokuwa PORI (enzi chuo kinaanzishwa). wakaanza kukaa "wasomi wa UD", wakaCHANGANYIKA na Raia.....
9. Dongobesh...Iko mkoani Manyara. Asili (Neno la Kibarabaig linalomaanisha Tembo Mweupe)...
10. Chato....Neno la asili ni UBWATO (Kikerewe/Kizinza) likimaanisha Mtumbwi. wazungu alishindwa litamka Vwema...