Nimevutiwa na Sura ya majini.
Hii inayazungumziaje au lengo ni nini. Msaada
SURA AL JINN.
1. Kwa jina la Mwenyezi Mungu,
Mwingi wa rehema, Mwingi wa ukarimu.
2. Sema: Imefunuliwa kwangu ya
kuwa kundi la majinni walisikia wakasema: Hakika Tumesikia Qur'an ya ajabu,
3. Inaongoza kwenye uongofu, kwa
hiyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha
yeyote na Mola wetu:
4. Na kwa hakika utukufu wa Mola
wetu umeinuka, Hakuchukua mke wala
mwana:
5. Na kwa hakika mpumbavu miongoni mwetu alikuwa akisema maneno ya
upuuzi juu ya Mwenyezi Mungu;
6. Nasi tulikuwa tukidhani ya kuwa
watu na majinni hawatasema uwongo
juu ya Mwenyezi Mungu
7. Na hakika kulikuwa na watu
miongoni mwa wanadamu wakijikinga
kwa watu miongoni mwa majinni, hivyo wakawazidishia kiburi:
8. Na kwa hakika wao walidhani
kama mlivyodhani ninyi ya kuwa Mwenyezi Mungu Hatamtuma ye yote.
9. Nasi tuligusa mbingu tukaiona
imejaa walinzi wenye nguvu na nyota
zing'aazo.
10. Na hakika tulikuwa tukikaa
humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza; lakini atakayejitahidi kusikiliza sasa
atakuta kimondo kikimvizia.
11. Nasi hatujui kama shari inatakiwa kwa wale wanaokaa ardhini au
Mola wao Anawatakia mwongozo.
12. Na hakika katika sisi wamo
wema na wengine katika sisi ni kinyume
cha hayo: tulikuwa njia mbalimbali:
13. Nasi tulijua ya kuwa hatuwezi
kumdhoofisha Mwenyezi Mungu katika
nchi wala hatuwezi kumponyoka kwa kukimbia:
14. Nasi tulipousikia mwongozo,
tukauamini, basi anayemwamini Mola
wake hataogopa hasara wala ubaya:
15. Nasi wamo miongoni mwetu
waliosilimu na wamo miongoni mwetu
wanaokengeuka; lakini aliyesilimu basi hao ndio hutafuta wema:
16. Waama wanaokengeuka basi
wamekuwa kuni za Jahanamu.
17. Na kama wangalishika kwa imara njia (iliyonyoka) Tungaliwanywesha
maji kwa wingi,
18. Ili Tuwajaribu kwa hayo. Na
anayepuuza kumkumbuka Mola wake
Atamsukuma kwenye adhabu ngumu:
19. Na kwa hakika misikiti yote ni
ya Mwenyezi Mungu, basi msimwombe
mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu.
20. Na hakika Mtumishi wa Mwenyezi Mungu aliposimama kumwomba
walikuwa karibu kumwangukia (wamwangamize).
21. Sema: Ninamwomba Mola
wangu tu wala simshirikishi na ye yote.
22. Sema: Kwa hakika mimi similiki
kwa ajili yenu dhara wala heri.
23. Sema: Bila shaka hapana ye yote
awezaye kunilinda na Mwenyezi Mungu,
wala sitapata makao ya salama ila Kwake Yeye tu:
24. Ila kwa kufikisha (ujumbe)
utokao kwa Mwenyezi Mungu na risala Zake; na atakayemwasi Mwenyezi
Mungu na Mtume Wake, basi bila shaka atapata moto wa Jahanamu, watakaa humo muda mrefu.
25. Hata watakapoyaona wanayoahidiwa, ndipo watajua ni nani msaidizi
dhaifu na mwenye idadi ndogo
26. Sema: Sijui kama yako karibu
mliyoahidiwa au Mola wangu Atayawekea muda mrefu:
27. Yu Mjuzi wa yasiyoonekana, na
Hampi ye yote uwezo wa kiutawala juu
ya milki Yake ya mambo yasiyoonekana.
28. Isipokuwa yule Anayemchagua
kuwa Mtume Wake. Na mbele yake na
nyuma yake hutembea malaika kama walinzi.
29. Ili Ajulishe ya kuwa wamekwisha fikisha risala za Mola wao; na
Ameyazunguka waliyo nayo na Amehesabu idadi ya kila kitu