Majira yamebadilika sana, badala ya kusubiri watalii waje, tubebe wanyama wetu tukawatembeze hukohuko na pengine kuwauzia kabisa

TANAPA wafunge kamera nyingi kwenye mbuga watu wawe wana Subscribe wanaingia online wanapata picha live za vijinyama vya pori usiku na mchana na wakati huohuo kipato kinaingia
Haya mawazo serikali iyabebe na kuyafanyia kazi haraka Sana!!

Mkuu, Safi sana
 
Mkuu, tunapoambiwa ni tajiri, utajiri wake unajumlisha na hifadhi zetu kaka
 
Propaganda nyingine hata ni aibu kuongea mbele ya watu waelewa. Kwa mujibu wa wanyamapori, tembo hubeba mimba miaka miwili, sasa piga mahesabu tembo wako 10,000, inawezekana vipi ndani ya miaka mitano wafikie 60,000? Hata kama walikuwa 10,000 huko nyuma huenda wote walikuwa majike, na walikuwa na mimba wote, je walipataje mimba bila madume? Kama hata hilo la wazi wanapika data, je una uhakika gani kuwa kuna hilo ongezeko kubwa?

Hilo la mabucha ya nyama pori, liko kinadharia zaidi kuliko uhalisia, ila ulivyolileta ni kama kweli kuna huo uchaguzi wa aidha nyama pori, au ya kufungwa. Propaganda zimepora ufahamu wako.
 
Hivi mkuu, siasa ni jitu gani hili, mbona ni kama likorofi kiasi hiki??

Kuna wakati mtu anajikuta mkali tu, wakati mwingine mtu anakuwa mropokaji tu, wakati mwingine mtu anaamua kufokea tu wengine na mitusi juu,

Hili li siasa ni li nini??
 
Nadhani kweli kunahitajika ubunifu yakinifu katika uwekezaji huu, la sivyo kuna hatari huko tuendako kukakosekana Maana ya kuwa na wanyama weeengi wasiokuwa na faida

Tatizo hakuna wa kujituma na kufanya vitu tofauti
Watu wameganda palepale tangu enzi za Mwalimu na hawataki kubuni chochote
Angalia Kruger National park mpaka kuna baiskeli na farasi ukipita katikati ya wanyama wakubwa
Pesa zipo ila hata wenye dhamana wanashindwa kujifunza kwa wengine
Bila kutembea na kuona mengi tutakuwa tumejifungia kwenye bubble tu

 
Hivi mkuu, siasa ni jitu gani hili, mbona ni kama likorofi kiasi hiki??

Kuna wakati mtu anajikuta mkali tu, wakati mwingine mtu anakuwa mropokaji tu, wakati mwingine mtu anaamua kufokea tu wengine na mitusi juu,

Hili li siasa ni li nini??

Umeshiba propaganda naona unacheua tu data za kupika. Kwa taarifa yako hili ni jukwaa la siasa, na mijadala humu ni ya kisiasa, sijui ulitakaje?
 
Mi sielewi bhana. Tembo anabeba mimba kwa muda gani? Ndani ya miaka 5 tembo 10K wamezaliana mpaka 60K, au nimeelewa vibaya.

AU ndani ya miaka 5 tembo wamepungua toka 60K mpaka 10K?

AU pengine wanazungumziwa sungura pori, au mbwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…