Majira yamebadilika sana, badala ya kusubiri watalii waje, tubebe wanyama wetu tukawatembeze hukohuko na pengine kuwauzia kabisa

Majira yamebadilika sana, badala ya kusubiri watalii waje, tubebe wanyama wetu tukawatembeze hukohuko na pengine kuwauzia kabisa

TANAPA wafunge kamera nyingi kwenye mbuga watu wawe wana Subscribe wanaingia online wanapata picha live za vijinyama vya pori usiku na mchana na wakati huohuo kipato kinaingia
Haya mawazo serikali iyabebe na kuyafanyia kazi haraka Sana!!

Mkuu, Safi sana
 
Mkuu, tunapoambiwa ni tajiri, utajiri wake unajumlisha na hifadhi zetu kaka
 
Wanajamvi Amani kwenu

Hivi leo, Dunia imebadirika, majra nayo na nyakati zinazidi kubadirika

Huko tuendako, Kwa sababu ya milipuko ya magonjwa na masharti yanayotokana na milipuko hiyo ya magonjwa, inatufanya walimwengu tuishi kidizaini, kama tulikuwa na utalii, mtu kusafiri kwenda mahali, inamuwia ugumu Kwa sababu ya usalama wa maisha yake.

Nchi yetu Kwa takwimu za miaka mitano iliyopita, tunaambiwa kwamba, tembo wetu nchi nzima walikuwa ni 10k Tu, leo tunaambiwa tembo wamezaliana kama dagaa Hadi kufikia 60k+ Hongera Kwa saerkali kuwalinda hawa tembo na kuongezeka kwake ni matunda ya serikali iliyopo.

Bahati mbaya iliyopo leo, wanyama wetu wameongezeka Sana, na Hii inakuwa ni nzuri hasa Kwa watalii kuvutika kirahisi Kwa sababu ya ongezeko la wanyama hao, watalii kuwapa uharaka wa kuona wanyama wengi na Kwa muda mfupi pindi wanapotembelea mbuga zetu,lakini sasa kuna hili la Corona.

Je, tunaweza kuwabeba wanyama wetu kuwatembeza huko wanakotokea watalii Ili nchi ijipatie fedha kama kawaida?

Ukiondoa Hilo, Je sasa, Kwa kuwa wanyama hawa wameongezeka kiasi cha kuwa wanavamia tu Hadi makazi ya wananchi na kusababisha hasara kubwa Kwa wananchi hao, Serikali haioni sasa ni wakati wa kuwavuna hao wanyama pengine Kwa kuwauzia mabeberu ndovu Ili serikali ipate mapato ya kuendeleza Miradi yake ukiondoa swala la kuwabeba na kuwatembeza huko Ulaya wanyama wetu.

Nasema hivyo Kwa sababu, Serikali ndiyo mmiliki wa maliasili hizi, lakini cha ajabu imekuwa ikipata hasara kubwa kwenye swala la ujangili licha ya kutumia gharama kubwa Sana ya kuwalinda hawa wanyama,

Kipindi cha nyuma, karibu Kila siku tulikuwa tukisikia, majangili yakutwa na ndovu,majangili sijui yamepakia twiga kwenye ndege na kupeleka ulaya kuwauza, majangili yamekwiba hizi Mali na Serikali kuendelea kupata hasara,

Tunapozungumza leo, nguvu ya serikali na matunda ya uwekezaji Kwa ajili ya kuwalinda wanyama hawa, imeenda sambamba na ongezeko la wanyama hawa, Hongera Sana Kwa hili

Kwa sasa serikali yetu inaonyesha kuzidiwa kiasi cha wanyama hao kuwa kero tena Kwa jamii, Maana hawalindwi ipasavyo, wanavamia mashamba na kuleta maafa Kwa wananchi, umefika wakati sasa wa serikali kufaidi matunda ya uwekezaji wake, na Kwa kuwa majangili yamedhibitiwa, basi serikali ianze kuvuna hawa wanyama Ili nchi ianze kunufaika na uwekezaji huo

Tumeona baahi ya wanyama ambao hutumika kama kitoweo, kuna mabucha yamefunguliwa, wananchi tunajiamlia tu kwenye familia zetu, kwamba Leo ni Aina gani ya nyama tule, basi tunaingia tu Kwa mabucha na kuchagua nyama tutakayo

Swali linabakia Kwa hao Tembo, Kwanza sidhani kama wanaliwa, sasa ni zamu ya serikali tena iamue kuanza kuwapunguza Ili yenyewe ndio iwe muuzaji mkuu wa ndovu na nchi iendelee kujiletea maendeleo makubwa na Kwa Kasi


Wajivu wa mambo mnasemaje?
Propaganda nyingine hata ni aibu kuongea mbele ya watu waelewa. Kwa mujibu wa wanyamapori, tembo hubeba mimba miaka miwili, sasa piga mahesabu tembo wako 10,000, inawezekana vipi ndani ya miaka mitano wafikie 60,000? Hata kama walikuwa 10,000 huko nyuma huenda wote walikuwa majike, na walikuwa na mimba wote, je walipataje mimba bila madume? Kama hata hilo la wazi wanapika data, je una uhakika gani kuwa kuna hilo ongezeko kubwa?

Hilo la mabucha ya nyama pori, liko kinadharia zaidi kuliko uhalisia, ila ulivyolileta ni kama kweli kuna huo uchaguzi wa aidha nyama pori, au ya kufungwa. Propaganda zimepora ufahamu wako.
 
Hivi mkuu, siasa ni jitu gani hili, mbona ni kama likorofi kiasi hiki??

Kuna wakati mtu anajikuta mkali tu, wakati mwingine mtu anakuwa mropokaji tu, wakati mwingine mtu anaamua kufokea tu wengine na mitusi juu,

Hili li siasa ni li nini??
 
Nadhani kweli kunahitajika ubunifu yakinifu katika uwekezaji huu, la sivyo kuna hatari huko tuendako kukakosekana Maana ya kuwa na wanyama weeengi wasiokuwa na faida

Tatizo hakuna wa kujituma na kufanya vitu tofauti
Watu wameganda palepale tangu enzi za Mwalimu na hawataki kubuni chochote
Angalia Kruger National park mpaka kuna baiskeli na farasi ukipita katikati ya wanyama wakubwa
Pesa zipo ila hata wenye dhamana wanashindwa kujifunza kwa wengine
Bila kutembea na kuona mengi tutakuwa tumejifungia kwenye bubble tu

IMG_6068.jpg
 
Hivi mkuu, siasa ni jitu gani hili, mbona ni kama likorofi kiasi hiki??

Kuna wakati mtu anajikuta mkali tu, wakati mwingine mtu anakuwa mropokaji tu, wakati mwingine mtu anaamua kufokea tu wengine na mitusi juu,

Hili li siasa ni li nini??

Umeshiba propaganda naona unacheua tu data za kupika. Kwa taarifa yako hili ni jukwaa la siasa, na mijadala humu ni ya kisiasa, sijui ulitakaje?
 
Mi sielewi bhana. Tembo anabeba mimba kwa muda gani? Ndani ya miaka 5 tembo 10K wamezaliana mpaka 60K, au nimeelewa vibaya.

AU ndani ya miaka 5 tembo wamepungua toka 60K mpaka 10K?

AU pengine wanazungumziwa sungura pori, au mbwa?
 
Back
Top Bottom