MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Rais Uhuru yuko Mombasa, Pwani kwenye gatuzi inayoshikiliwa na gavana wa mlengo wa upinzani, wamekwenda pamoja bega kwa bega wakizindua miradi ya nguvu yaani hadi raha. Rais Uhuru alikubali kuwapa mkono wa salamu viongozi wa upinzani wakiongozwa na Raila Odinga, tangu hapo wote wameshirikiana pakubwa na nchi inapaa kwa kasi isiyo ya kawaida.
Hii haimaanishi siasa hazipo, tena wanazipiga tu na kutupiana vijembe vya kawaida, ila likija kwenye suala la maendeleo wanaweka tofauti zao pembeni na kukumbatia uzalendo maana maendeleo hayana chama.
Pia tumeona rais Uhuru akitumia diplomasia kuwafikia mataifa majirani, pamoja na kuchokozwa kote kule, hakuruhusu kiburi, ila kawapa mkono wa ushirikiano.
Sasa kwa mataifa yaliyotuzunguka, upinzani huko wanawindwa utadhani sio raia wa huko, Uganda kuna jamaa anaitwa Boby Wine hapumui, kila uchao ni mikimbio na mapolisi, mwengine wa huko anayeitwa Besigye sijui naye kafia wapi simuskii, alikua anachezea kibano kila akiongea.
Tanzania huko ndio usipime, wanaye kiongozi wao anaitwa Tundu Lissu katolewa huko kwa marisasi, ameshindwa kurudi nyumbani nchi ya baba na mama yake, juzi aliongea na kusema kamwe hayupo tayari kurudi hadi ahakikishwe hatokumbana na hayo marisasi. Tz wanaelekea kwenye uchaguzi ila kwa sasa upande mmoja ndio upo kikampeni kabisa, lakini upande wa pili hawawezi kukusanyika hata watatu.
Rwanda na Burundi japo hatupo nao kwenye mpaka mmoja, ila huko ndio sijui hata kama wana neno 'upinzani' kwenye misamiati yao.
Sudan Kusini na Somalia wao ni mwendo wa kutunishiana, risasi na mabomu yamerindima hadi wamechokana kiasi cha kuruhusu amani, Mhabeshi wa Ethiopia sijawahi kumfuatilia, yeye yupo yupo tu.
Muhimu sana mataifa yote haya yakajifnza kitu kutoka kwa uongozi wa Kenya, weka kiburi na mikwara pembeni, kumbatia ushirikiano na utengamano.
Hatujafika bado, ila tunaenda vizuri....