Majirani wamemripoti jamaa kituo cha polisi kisa kazi yake haijulikani! Sasa anadai Milioni 500 kwa kuletewa usumbufu

Majirani wamemripoti jamaa kituo cha polisi kisa kazi yake haijulikani! Sasa anadai Milioni 500 kwa kuletewa usumbufu

Wakuu Kuna jamaa hapa mtaani alikua anahisiwa anafanya shuguli haramu sababu anamaisha mazuri ila kazi yake haijulikani anashindwa ndani akitoka jioni

Sasa Kuna majirani wawili wamemripoti polisi akaja kukamatwa. Sasa akiwa huko polisi akasema yeye kazi yake ni kubeti na analipa Kodi Kwa serikali kupitia mikeka yake anayoshinda na kweli kaonyesha mikeka anakula mamilioni ya pesa ni aina ya watu wanaoweka pesa nyingi sana kwenye mechi.

Sasa kingine kaenda mahakamani anawashitaki majirani zake hao wawili Kwa kosa la kumdhalilisha na kumpotezea mda wa kufanya mambo yake ya msingi na anadai fidia million 500 na ana mawakili wake kabisa wa 3

Hivi hii kesi anaweza kushinda huyu jamaa ishu ipo serious sana
Wewe ni mmoja kati ya hao majirani wawili?
 
Tatizo sio majiran kuripoti polisi. Tatizo ni intelijensia ya jeshi letu la polisi namna inavyofanya kazi. Walipaswa kufanya uchunguzi kabla ya kumkamata na hata hivyo angehojiwa tu na kuachiwa sio kushikiliwa bila vidhibiti
 
Wakuu Kuna jamaa hapa mtaani alikua anahisiwa anafanya shuguli haramu sababu anamaisha mazuri ila kazi yake haijulikani anashindwa ndani akitoka jioni

Sasa Kuna majirani wawili wamemripoti polisi akaja kukamatwa. Sasa akiwa huko polisi akasema yeye kazi yake ni kubeti na analipa Kodi Kwa serikali kupitia mikeka yake anayoshinda na kweli kaonyesha mikeka anakula mamilioni ya pesa ni aina ya watu wanaoweka pesa nyingi sana kwenye mechi.

Sasa kingine kaenda mahakamani anawashitaki majirani zake hao wawili Kwa kosa la kumdhalilisha na kumpotezea mda wa kufanya mambo yake ya msingi na anadai fidia million 500 na ana mawakili wake kabisa wa 3

Hivi hii kesi anaweza kushinda huyu jamaa ishu ipo serious sana
Uongo, polisi huwa hawatoi utambulisho wa mtoa taarifa
 
ndo ivo best!! tatizo elimu
Actually shughuli nyingine zina trade secrets na mtu kukutajia shughuli yake unaweza kumgeza na kumharibia nafasi yake ya kupata kipato.

Kwa msingi huo, habari nzima ya kumtaka mtu ajieleze shughuli yake ni uonevu.

Kama unamshuku mtu, mchunguze mpaka upate makosa, halafu mshitaki kwa makosa hayo.

Kuna watu wana uwezo wa kuishi kwa kuwekeza pesa kwenye masoko ya mitaji na hisa tu, pesa zinawafanyia kazi wao hawahitaji kufanya kazi.

Kuna watu wanafanya kazi kwenye mitandao, unaweza kuona mtu hatoki nje, kumbe anafanya kazi mitandaoni, analiowa nishahara ya kinataifa. Mimi kuna rafiki yangu anafabya kazi remotely online huju Marekani, kuna wakati anaona hana haja ya juwa Marekani anarudi Tanzania anafanya kazi mtandaoni mapaka miezi 6.

Sasa mtu kama huyo ukimshangaa jwamba hatoki nje kwenda kazini, utamshangaa kwa ushamba na ujima tu.
 
Uzi wa hivi hivi niliusoma kuwa kuna mtu yuko vizuri ila hamjui anafanya kazi gani
 
Kwamba huo mtaa hauna mjumbe wala mwenyekiti...atahivyo ni sawa kama mnamashaka nà mtu ni vyema kuwashirikisha polisi
 
Katika wale maadui 3 wa Taifa, kuna hili kubwa lao tulisahau na linatutesa sana, UCHAWI.
 
kwa hiyo jirani kutoa ripoti polisi ni vibaya?haya incase ikiwa jamaa alikuwa drugs dealer?

mahakama haitatenda haki,kwani hiyo ni kawaida kuhisi.
Huwezi ukamripoti mtu kwa kitu usichokuwa na uhakika nacho.
Kumripoti mtu kwa tukio baya ni jambo jema kiusalama ila unatakiwa uwe na vielelezo kwa mfano umemuona anatembea na silaha hicho ni kielelezo au anatembea na watu ambao unawajua kuwa wana matukio ya uhalifu hiyo inaweza kuwa kielelezo japo ni dhaifu,kutokujua kazi yake hicho sio kielelezo kwa sababu kazi yake wewe haikuhusu na hakuna sheria inayosema kila mtu awe anatangaza kazi yake kwa majirani hiyo moja kwa moja ni chuki za kijinga na ukosefu wa shughuli za kufanya sasa ngoja wapelekwe mahakamani ndio watajifunza siku nyingine ili waache kufuatilia maisha ya watu.
 
Sheria ya Whistle blowing inawalinda hao majirani wala wasibabaike wao walitoa taarifa Polisi kwa nia njema kutokana na wasiwasi waliokuwa nao. Hivyo wasishituke, Polisi watakuwa mashahidi wao wazuri tu.
taarifa vs shitaka , vitu viwili mbali mbali
 
labda polisi wa huko kwenu
Hata wakitoa kimakosa, bado haitakubalika kama ushadi mahakamani, inaotwa ‘Ill gotten information’ , hata kama ni kweli.

Mfano, mtu akampa siri mkewe, halafu huyo mke akaenda kuitoa polisi, hiyo taarifa haiwezi kupokelewa na mahakama kama ushahidi, maana ni ‘Ill gotten information’

Hata ukafanya upekuzi kwenye nyumba au simu ya mtu hila ‘Search warrant’, ushahidi wowote utakaopatiksna, hautapokelewa na mahakama, sababu ni ‘ill gotten evidence’

Kuna baadhi ya majimbo huko marekani, hata ukamrekodi video mtu akikiri kufanya jambo flani, na ikiwa hukumpa taarifa kwamba unamrekodi, huo ushahidi hautapokelewa mahakamani, sababu ni ‘ill gotten evidence’
 
Amna kesi hapo ata angeenda na tundu lissu kwanza mnajua maana ya kuzalilisha? Na iyo fidia yeye ndo anajipangia?
 
Actually shughuli nyingine zina trade secrets na mtu kukutajia shughuli yake unaweza kumgeza na kumharibia nafasi yake ya kupata kipato.

Kwa msingi huo, habari nzima ya kumtaka mtu ajieleze shughuli yake ni uonevu.

Kama unamshuku mtu, mchunguze mpaka upate makosa, halafu mshitaki kwa makosa hayo.

Kuna watu wana uwezo wa kuishi kwa kuwekeza pesa kwenye masoko ya mitaji na hisa tu, pesa zinawafanyia kazi wao hawahitaji kufanya kazi.

Kuna watu wanafanya kazi kwenye mitandao, unaweza kuona mtu hatoki nje, kumbe anafanya kazi mitandaoni, analiowa nishahara ya kinataifa. Mimi kuna rafiki yangu anafabya kazi remotely online huju Marekani, kuna wakati anaona hana haja ya juwa Marekani anarudi Tanzania anafanya kazi mtandaoni mapaka miezi 6.

Sasa mtu kama huyo ukimshangaa jwamba hatoki nje kwenda kazini, utamshangaa kwa ushamba na ujima tu.
Mimi nina mjomba wangu anakula za mtu kati kila wiki! kimya kimya!
 
Back
Top Bottom