Majirani wamemripoti jamaa kituo cha polisi kisa kazi yake haijulikani! Sasa anadai Milioni 500 kwa kuletewa usumbufu

Wewe ni mmoja kati ya hao majirani wawili?
 
Tatizo sio majiran kuripoti polisi. Tatizo ni intelijensia ya jeshi letu la polisi namna inavyofanya kazi. Walipaswa kufanya uchunguzi kabla ya kumkamata na hata hivyo angehojiwa tu na kuachiwa sio kushikiliwa bila vidhibiti
 
Uongo, polisi huwa hawatoi utambulisho wa mtoa taarifa
 
ndo ivo best!! tatizo elimu
 
Uzi wa hivi hivi niliusoma kuwa kuna mtu yuko vizuri ila hamjui anafanya kazi gani
 
Kwamba huo mtaa hauna mjumbe wala mwenyekiti...atahivyo ni sawa kama mnamashaka nà mtu ni vyema kuwashirikisha polisi
 
Katika wale maadui 3 wa Taifa, kuna hili kubwa lao tulisahau na linatutesa sana, UCHAWI.
 
kwa hiyo jirani kutoa ripoti polisi ni vibaya?haya incase ikiwa jamaa alikuwa drugs dealer?

mahakama haitatenda haki,kwani hiyo ni kawaida kuhisi.
Huwezi ukamripoti mtu kwa kitu usichokuwa na uhakika nacho.
Kumripoti mtu kwa tukio baya ni jambo jema kiusalama ila unatakiwa uwe na vielelezo kwa mfano umemuona anatembea na silaha hicho ni kielelezo au anatembea na watu ambao unawajua kuwa wana matukio ya uhalifu hiyo inaweza kuwa kielelezo japo ni dhaifu,kutokujua kazi yake hicho sio kielelezo kwa sababu kazi yake wewe haikuhusu na hakuna sheria inayosema kila mtu awe anatangaza kazi yake kwa majirani hiyo moja kwa moja ni chuki za kijinga na ukosefu wa shughuli za kufanya sasa ngoja wapelekwe mahakamani ndio watajifunza siku nyingine ili waache kufuatilia maisha ya watu.
 
Sheria ya Whistle blowing inawalinda hao majirani wala wasibabaike wao walitoa taarifa Polisi kwa nia njema kutokana na wasiwasi waliokuwa nao. Hivyo wasishituke, Polisi watakuwa mashahidi wao wazuri tu.
taarifa vs shitaka , vitu viwili mbali mbali
 
labda polisi wa huko kwenu
Hata wakitoa kimakosa, bado haitakubalika kama ushadi mahakamani, inaotwa ‘Ill gotten information’ , hata kama ni kweli.

Mfano, mtu akampa siri mkewe, halafu huyo mke akaenda kuitoa polisi, hiyo taarifa haiwezi kupokelewa na mahakama kama ushahidi, maana ni ‘Ill gotten information’

Hata ukafanya upekuzi kwenye nyumba au simu ya mtu hila ‘Search warrant’, ushahidi wowote utakaopatiksna, hautapokelewa na mahakama, sababu ni ‘ill gotten evidence’

Kuna baadhi ya majimbo huko marekani, hata ukamrekodi video mtu akikiri kufanya jambo flani, na ikiwa hukumpa taarifa kwamba unamrekodi, huo ushahidi hautapokelewa mahakamani, sababu ni ‘ill gotten evidence’
 
Amna kesi hapo ata angeenda na tundu lissu kwanza mnajua maana ya kuzalilisha? Na iyo fidia yeye ndo anajipangia?
 
Mimi nina mjomba wangu anakula za mtu kati kila wiki! kimya kimya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…