Major Abdulrahman Shimbo: Kamanda wa Kikosi cha JWTZ kilichozima jaribio la mapinduzi Seychelles

Rene alimlaumu sana Nyerere kuingilia masuala ya Seychelles. Nimesahau hii historia kwa mapana. Ila all in all, sijui kwanini mambo mengi wanadanganya nchi hii. Hovyo sana!
 
Rene alimlaumu sana Nyerere kuingilia masuala ya Seychelles. Nimesahau hii historia kwa mapana. Ila all in all, sijui kwanini mambo mengi wanadanganya nchi hii. Hovyo sana!

..Rene anamlaumu vipi Nyerere wakati ndiye aliyemsaidia akadumu madarakani?

..Unless umemchanganya na mpinzani wake ambaye ilikodi hao mercenaries waliobambwa na Jwtz?
 

..hata mimi nadhani mtangazaji hakuitendea haki interview hii.

..naona kama ametunyima watazamaji nafasi ya kumsikia Abdulrahman Shimbo akifunguka kuhusu mission ya Jwtz nchini Seychelles.

..naweza kukubaliana na wewe kwamba mtangazaji hakuwa amejiandaa na hakujuwa anakwenda kumhoji mtu wa aina gani.

..tukirudi kwenye hiyo operation, kunapotokea crisis ktk uwanja wa ndege, na kukawa na raia ktk eneo hilo, ni lazima yafanyike mambo mawili.

1. Uwanja wa ndege lazima uwe sealed kwamba hakuna anayeingia na kutoka.

2. Ni lazima ndege zizuiwe kuruka na kutua. Haitakiwi kuwe na vyombo vinavyoruka karibu na eneo hilo.

..Sasa Shimbo wakati huo akiwa Major na incharge wa kikosi kilichokuwa Seychelles anaeleza kuwa aliwasiliana na ndege iliyokuwa inatarajia kutua Seychelles na kujaribu kuizuia.

..Ukisoma sources nyingine zinadai mercenaries waliteka control tower na kuanza kuzungumza na ndege na kuiruhusu itue.

..Kwa hiyo bila shaka rubani alitua kwa maelekezo ya mercenaries waliojaribu kupindua serikali.

..Na hao mercenaries walitoroka kwa kutumia ndege hiyo kwasababu ndege waliyotua nayo ilikuwa imeharibiwa.

..Jambo lingine la kulizingatia ni usalama wa RAIA waliokuwa ktk ndege iliyotekwa na kutorosha hao mercenaries toka Seychelles.

..Kuhusu umuhimu wa mission ya Jwtz Seychelles, kwa maoni yangu ni busara zaidi kupigana vita nchi ya mipaka yako, kuliko kuruhusu vita ije nchini kwako.
 
..Rene anamlaumu vipi Nyerere wakati ndiye aliyemsaidia akadumu madarakani?

..Unless umemchanganya na mpinzani wake ambaye ilikodi hao mercenaries waliobambwa na Jwtz?
Ok itakua nimechanganya jina.
Ni mambo niliyasoma kitambo sana siasa za visiwani huko
 
Ok itakua nimechanganya jina.
Ni mambo niliyasoma kitambo sana siasa za visiwani huko

..Tz ili-support upande mmoja dhidi mwingine huko Seychelles.

..kwa hiyo ni kweli kabisa kwamba tuliingilia mambo yao.

..na upande ambao tuliunyima support lazima utulaumu. Na ndio hao waliokwenda kutafuta msaada kwa makaburu wa Afrika Kusini na Walowezi wa Rhodesia.

..lakini uwepo wetu Seychelles naamini ulilenga ktk suala zima la USALAMA wa Tanzania.
 
Nguruvi3,

..katika mahojiano hayo Shimbo anadai alipoitwa makao makuu alidhani anapelekwa Msumbiji, au Zimbabwe.

..Watz wengi hawajui mchango wa Jwtz ktk vita vya ukombozi wa Zimbabwe, ni bahati mbaya kwamba muongoza kipindi aliacha hilo likapita.
 
Halaf kuna wajinga wanakuja hapa wanasema sijui Rwanda ni kiboko sijui nyenyenye ๐Ÿšฎ
 
Nguruvi3,

..katika mahojiano hayo Shimbo anadai alipoitwa makao makuu alidhani anapelekwa Msumbiji, au Zimbabwe.
CoS Shimbo alionekana kuwa tayari sana kueleza ''declassified' information kwa bahati mbaya muongozaji hakuwa na background ya mambo mengi. Kwa mfano aliposema Msumbuji hapo CoS T. Kiwelu angetajwa kwasababu alishiriki sana na Shimbo angeeleza.
..Watz wengi hawajui mchango wa Jwtz ktk vita vya ukombozi wa Zimbabwe, ni bahati mbaya kwamba muongoza kipindi aliacha hilo likapita.
Tatizo ni lile lile la muongozaji kutokuwa na ufahamu wa nyuma! huenda alikuwa amdogo lakini kazi yake inamruhusu kujifunza na ni muhimu kufanya homework kabla ya kukutana na watu kama Shimbo.

Ukitaja Zimbwabwe hapo Brigedia Hashim Mbita (RIP) angetajwa na Shimbo na kungekuwa na mengi ya kujifunza. Wazimbabwe wanajua hilo ndio maana Mugabe alipigania sana OAU wakati huo itoe jina la Nyerere , alisimama kidete na alieleza kwa uchungu sana mchango wa Mwalimu

Kuna siku mtangazaji Mwanamke alimhoji Gen. Zawadi Madawili aliyekuwa mwanamke wa kwanza jeshini mwaka 1973. Nilishangaa kipindi kiliisha bila kumuuliza ushiriki wake wa vita ya Kagera 1978. Huwezi kuongea na Afisa wa JWTZ wa miaka ya 70 bila kuongelea Kagera, missed opportunity

Lt. Gen Shimbo kaingia jeshini mwaka 1973 wakati CDF akiwa M.Sarakikya. Kwahiyo amefanya kazi na ma-CDF wote isipokuwa CDF Gen. Mabeyo, hivi kipindi kinakwisha bila kutaja hata mmoja!
 
baada ya kuwakamata wanajeshi wa kukodi wengi kutoka france na south Africa jw wakaweka silaha chini wakawaambia wapigane shimbo anakuja kufika alkuta wazungu wanamanundu ya kutosha ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

by the way shelisheli na tanzania tunategemeana kรฌusalama
 
wote tulkua wajamaa at by that time coldwar ilkua imetamalaki lkn pia south ilkua chini ya makaburu
nyerere alkua mbabe bingwa wa kuwadindia weupe
 

Tupo vizuri Seychelles, Comoro, Matatizo yote ya Uganda, Kenya, nchi zote za kusini, sisi ndio tunategemewa, tunaheshimiwa kutatua matatizo kidiplomia au kijeshi.

Tatizo tumepoteza kumbukumbu, kujitambua, kuchukua nafasi yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ