Major Abdulrahman Shimbo: Kamanda wa Kikosi cha JWTZ kilichozima jaribio la mapinduzi Seychelles

Askari wa jwtz akifanya kosa la jinai je, askari polisi hana mamlaka kisheria kumkamata? Naomba nipe maarifa mkuuu

Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app

..jeshi wana Polisi [ military police / MP ], pia wana mahakama za kijeshi.

..kwa hiyo, itategemea jinai unayoizungumzia imefanyika ndani ya jeshi, au uraiani.

..kumkamata Mnadhimu Mkuu wa jeshi sio jambo dogo.

..ukifuatilia hayo mahojiano, inaelezwa kwamba Mnadhimu anahusika na mambo mengi, na anajua mambo mengi sana kuhusu jeshi.

..nchi ikivamiwa, Mnadhimu mkuu ndiye anayepanga mipango ya vita, na kuiwasilisha kwa mkuu wa majeshi ambaye ataidhinisha mpango mmoja.

..sasa mimi nadhani mtu wenye dhamani kubwa kiasi hicho siyo rahisi akakamatwa na Polisi wa ndani, au nje ya nchi.
 

Yaani usalama wetu uko kwenye visiwa na si mipakani ??

Iddi Amin aliingiaje Kagera ?? tanzanite na madini nyengine zinakwendaje Kenya au ndio hofu yetu ni visiwani ??
 
Nemependa sana comments nyingi za wana JF kuhusu huyu kiongozi. Nyingi nahisi zina ukweli kumhusu huyu mzee wetu.
 
Yaani usalama wetu uko kwenye visiwa na si mipakani ??

Iddi Amin aliingiaje Kagera ?? tanzanite na madini nyengine zinakwendaje Kenya au ndio hofu yetu ni visiwani ??

..kuna mpaka wa nchi kavu.

..pia kuna mpaka ktk bahari ya hindi.

..Na mpaka wa majini ktk ziwa Victoria, Tanganyika, na Nyasa.

..vilevile kuna mpaka wa anga.

..rasilimali ziko nchi kavu, majini, na baharini.

NB:

..mpaka wetu wa bahari sio hapo ufukweni feri magogoni, coco beach, au kurasini. Kuna eneo kubwa zaidi la bahari ambalo ni miliki ya Tz.

..nakubaliana na wewe kulaani utoroshwaji wa rasilimali za nchi kavu kama tanzanite.
 
Wacha majungu wewe kama jeshi katika hali ya hatari linaweza ku-intervene air communication na kuamuru ndege ifanye diversion! Sasa kwa kesi ya Seyschelles at the time kulikuwa na pande mbili zinakinzana za Rais Albert René na aliyepinduliwa James Mancham na wote walikuwa na wafuasi ndani na nche ya serikali ikiwemo taasisi! Mpango kama huu lazma ulikuwa na insiders hata airport!

Ukisikiliza vizuri maelezo yake alijaribu kuielekeza ndege iende Nairobi kwa vile uwanja ulikuwa under control ya jeshi baada ya hali ya usalama kuwa tete hakujibiwa hii ina maana Nairobi walikuwa wanajua kuhusu uvamizi ule.

Pia ukiacha ukweli askari waliokuwa zamu at security check point waliruhusu abiria wapite bila ukaguzi . Mwisho air controller au yeyote mwenye kujua frequency ali-intervene na aliilazimisha itue kukiwa tayari kuna majeshi yanapigana!

Huihitaji rocket science kujua kulikuwa na askari wengine wa kukodi waliokuwa wanakuja na kama asingeharibu hizo ndege hali ingekuwa tete wangetoroka kwa kupaa! Unapaswa kujua ujasusi wa jeshi la makaburu kujua umafia uliokuwepo kipindi hicho plse wacha majungu ya vijiweni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…