Major General Mbuge Kuwa RC kutoka Mkuu wa JKT Kapanda Cheo au kashuka?

Major General Mbuge Kuwa RC kutoka Mkuu wa JKT Kapanda Cheo au kashuka?

Habari wanabodi? naomba kupata uelewa kidogo, kwa nafasi kama ya Major General Mbuge kutoka kuwa Mkuu wa JKT na kwenda kuwa RC je hapo kapanda cheo ama kashuka? naomba uelewa wa kina juu ya hili tafadhali.
na, hongera kwake kwa uteuzi!!
Nyota mbili zinabakia palepale sema siyo tena mkuu wa JKT. Either itamlazimu Rais kumpandisha cheo brigedia general ili ashike nafasi hiyo ama atalazimika kumhamisha meja jenero mwingine ili awe mkuu wa JKT. Kwanza wamelundikwa huko hovyo hovyo tuu na hakuna wanalofanya. Madam chomoa kimeja kimoja kikave pengo!
 
Kimajukumu kijeshi kashushwa. Huyu alikuwa ni mkuu wa JKT nchi nzima na sasa hivi anaenda kuwa Mkuu wa Mkoa tuu.

Portfolio aliyokuwa nayo akiwa Mkuu wa JKT Tanzania ilikuwa ni kubwa sana kuliko sasa anavyokwenda kuwa Mkuu wa Mkoa.

Kwa kawaida wakiona umezingua jeshini they get rid of you kwa njia kama hii. Kumbuka wakati wa akina General Mirisho Sarakikya, T. Kiwelu n.k

Kwahiyo, Major General Charles Mbuge sasa hivi ameshika tama anasikitika.

Asantea!
Kulikoni? Nasikia alichukia sana waliosoma maana yeye ni msomi wa mechanical
 
Cheo bado anacho.... ila majukumu ni kama yamepungua. Unatoka ku-control mambo ya nchi nzima kwenda kwenye mkoa!!
 
R C ni cheo cha heshima na majukumu mengi zaidi ya mkuu wab jkt pia RC alipo anamwakilusha Rais direct
Mkuu wa JKT huwasiliana na Rais kupitia kwa CDF, wakati mkuu wa mkoa huwasiliana na rais moja kwa moja! Tofauti kubwa kabisa, labda tusema anapunguzuiwa influence jeshini.
 
What happened? Was he delivering? Was he trying to impress just his former boss?
Hayo ndio maswali ya kujiuliza.
Kama ni issue ya kutenguliwa, kuchunguzwa au kutumbuliwa iko palepale
Walitumbuliwa kina Lowasa, Kitwanga, Lugola sembuse hawa?
 
Duuh, yaani CDF ana salute kwa DC? nlkua sijui hii, kwahyo unataka kusema CDF General Mabeyo sasa ata-salute kwa RC Major General Mbuge? mmh
Salit ni salam ya kijeshi. Askari kama kavaa uniform Salut ndiyo salam yake na kama kavaa nguo za kawaida basi unanyooka vizuri unanyanyua visigino ukiwa umekakamaa. Ukiona mtu kapiga salut wala siyo ndiyo kawa mdogo hapana

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Duuh, yaani CDF ana salute kwa DC? nlkua sijui hii, kwahyo unataka kusema CDF General Mabeyo sasa ata-salute kwa RC Major General Mbuge? mmh
Kijeshi ni kuwa wewe mdogo unaanza kumsalimu kwa kupiga salute na yeye mkubwa analazimika kupokea salamu yako kwa kupiga salute.
Sasa inapokuja wewe raia unamsalimu mkuu wa jeshi ambaye amevalia kijeshi anajibu salamu yako kwa kupiga salute. Kwa hiyo ni kawaida kwa mwanajeshi kujibu salamu kwa kupiga salute na hasa katika mazingira rasmi.
 
Habari wanabodi? naomba kupata uelewa kidogo, kwa nafasi kama ya Major General Mbuge kutoka kuwa Mkuu wa JKT na kwenda kuwa RC je hapo kapanda cheo ama kashuka? naomba uelewa wa kina juu ya hili tafadhali.
na, hongera kwake kwa uteuzi!!
Watanzania bana
Ukiwa civil servant utapewa kaZi yoyote
 
Kanali kikwete alikua anapigiwa salute na CDF mwamnyange.
 
Daaa demotion kubwa umeonekana hufai kabisa heri anfempa ubalozi akakae mbali hapo akichemsha tena anarudi kikosini ila Maj Gen parefu atatoka vizuri hakuna njaa
 
Back
Top Bottom