Major General Mbuge Kuwa RC kutoka Mkuu wa JKT Kapanda Cheo au kashuka?

Major General Mbuge Kuwa RC kutoka Mkuu wa JKT Kapanda Cheo au kashuka?

Habari wanabodi? naomba kupata uelewa kidogo, kwa nafasi kama ya Major General Mbuge kutoka kuwa Mkuu wa JKT na kwenda kuwa RC je hapo kapanda cheo ama kashuka? naomba uelewa wa kina juu ya hili tafadhali.

Hongera kwake kwa uteuzi!!
Obviously Jenerali kapigwa parking.
Kateremka, hilo halina ubishi.
Tetesi ni kwamba utendaji wake una walakin.
Miradi mingi waliyosukumiziwa na JPM iko below standard.
 
Kazi kwelikweli inaonesha umezaliwa baada ya Vita vya Kagera
mambo ya kuomba hela hata awe Kambini ataomba mpaka na chakula
Hebu jiulize wakina Mayunga, Kimario, Marwa hawa walikuwa na vyeo vikubwa Jeshini lkn walipewa Mikoa
Hao uliowataja hawakuwa wakuu wa Jeshi.
Ma brigade commanders.
 
Duuh, yaani CDF ana salute kwa DC? nlkua sijui hii, kwahyo unataka kusema CDF General Mabeyo sasa ata-salute kwa RC Major General Mbuge? mmh
Mbona ni Jambo la kwaida mwanajeshi au askari wa cheo chchte anapokutana na mwanasiasa yyte ambae nafasi yake ni ya uteuzi wa raisi anamsalimia kijeshi Yani salute, hio haina maan yule ni mkubwa wake kiprotocal
 
Duuh, yaani CDF ana salute kwa DC? nlkua sijui hii, kwahyo unataka kusema CDF General Mabeyo sasa ata-salute kwa RC Major General Mbuge? mmh
Kimsingi ndio kabadilishiwa majuku na kupewa nafasi ya kisiasa lakini kuhalisia kiprotocal nafasi ya ukuu wa chombo cha usalama na u RC ni kubwa ile ya kuwa boss wa JKT.....ni sawa na kamishna andengenye yule mkuu wazimamoto alietolewa na magufuli kwene lile sakata na lugola,..alipotolewa pale juu akapewa mkoa(RC) Sasa how do u promote mtu alieshindwa kwene nafasi unachofanya unamtoa kwene ile ngazi kubwa unampeleka ngazi ya uongozi ya kawaida kwa heshima kubwa aliyonayo kufwatana na cheo chake cha kijeshi
 
Kazi kwelikweli inaonesha umezaliwa baada ya Vita vya Kagera
mambo ya kuomba hela hata awe Kambini ataomba mpaka na chakula
Hebu jiulize wakina Mayunga, Kimario, Marwa hawa walikuwa na vyeo vikubwa Jeshini lkn walipewa Mikoa
Kupewa mkoa ni njia nzuri ya kufungwa break. JKT jamaa enzi ya JPM akipata masifa ya miererani mara Ikulu na alivyokuwa anajua kujikunja na salute yake ya kikorea.

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu wa JKT huwasiliana na Rais kupitia kwa CDF, wakati mkuu wa mkoa huwasiliana na rais moja kwa moja! Tofauti kubwa kabisa, labda tusema anapunguzuiwa influence jeshini.
Kuwasiliana na raisi moja kwa moja sio ukubwa....Yani uanze kufananisha mkuu wa jeshi la JKT nchi nzima na RC wa mkoa ur joking
 
Inasemakana aliwatumikisha vijana wa JKT kupitiliza utu, wapo walioondoka kwa madhara ya cement Mererani na miradi mingine. Alipaswa kuwapa vifaa vya kujikinga. Ni kweli Jeshi hufanya kazi usiku na mchana , tuliyaona tukiwa JKT kwa mujibu wa sheria lkn angalau kutakuwa na shift ili vijana wapate muda wa kupumzika.
 
Nani anakumbuka upandaji wa vyeo kwa huyu Major General Charles Mbuge!!....Paul Makonda analijua sana hili jambo

Huyu jamaa alizingua sana akiwa Mkuu wa JKT alikuwa anawachukia sana Makamanda waliokwenda shule na alipenda sana kuwaweka vibaraka wake kwenye nafasi mbalimbali JKT, professionalism kwa huyu Kamanda ilikuwa zeero kabisa!!

Kuna jamaa alimchukia sana kisa hakuenda kumpongeza alivyopandishwa cheo na mwendazake. Akaamua kumtupa Kigoma and then wakati wenzake wanapandishwa vyeo mwezi wa 2 kuwa Ma-Major jjna la huyo jamaa akalinyofoa makusudi tu kwa sababu ya chuki zake binafsi . Kwahiyo wenzake wamekuwa Ma-Major yeye bado ni Captain. Huyu jamaa yuko kambi ya Mtabila Kigoma na ni Msomi mzuri tu.

Acha karma imle!!!
Bila shaka huyo jamaa ni wewe!
 
Mkuu wa mkoa ni political figure tu ila inapokuja swala la bajeti na utendaji kila kitu kinaishia kwa RAS- Katibu Tawala Mkoa ndio kila kitu.
Kuwasiliana na raisi moja kwa moja sio ukubwa....Yani uanze kufananisha mkuu wa jeshi la JKT nchi nzima na RC wa mkoa ur joking
 
Issue ya vurugu ya wale watoto wa JKT wa Mkataba imemgharimu,

pia alipandishwa kwa kasi sana kutokea pale ruvu akiwa Kanali 2016
 
Hajapanda cheo wala hajashuka cheo ni mabadiliko ya kimajukumu tuu angekuwa amekuwa Brigedier ningesema ameshuka

Kivipi hapo, hebu fafanua kidogo! Kwani kati ya Meja Generali na Brigedia ni nani yupo juu ya mwingine?
 
Nani anakumbuka upandaji wa vyeo kwa huyu Major General Charles Mbuge!!....Paul Makonda analijua sana hili jambo
Ni baada ya kumwambia Magufuli kwa ukakamavu JESHI HALISHINDWI!

Magu akampenda sana akaanza kumpaisha.

Baadae akamtumbua jeshini huko, sijui alim dissapoint kitu gani masikini ya Mungu kwenye miradi ya JKT.
 
R C ni cheo cha heshima na majukumu mengi zaidi ya mkuu wab jkt pia RC alipo anamwakilusha Rais direct
Faraja kazini.
Yaani toka cheo cha hadhi ya Kitaifa kuwa ngazi ya kimkoa amepanda cheo?
RC Kigoma alivyotoka DG Zimamoto naye alipanda cheo?
 
Back
Top Bottom