Majumuisho kesi Mbowe, Kinyang'anyiro ni katika DR

Majumuisho kesi Mbowe, Kinyang'anyiro ni katika DR

Nilisikia/kuona Video ktk bunge la umoja wa ulaya wakisema kuwa wawakilishi wao walio hudhuria mahakamani kufuatilia kesi ya Mbowe walitoa tathmini kwa kusema kuwa kesi haikuwa na msingi wa kisheria bali ni ya kisiasa.Kama video ile ni ya kweli,tutegemee DPP kuachana nayo maana hakuna namna.
 
hivi haki unayoitegemea ndugu hapani kama ipi maana naona kama una jibu tayari kuwa akiamua hivi tu hajatenda haki na akiamuahivi katenda haki?
Wewe uonavyo mpaka sasa katika hiyo kesi kuna shahidi kaelezea ugaidi ?
 
Kesho Inshallah, mawakili wasomi watawasilisha majumuisho yao mbele ya Jaji Tiganga.

Msingi wa kinyang'anyiro bila shaka utakuwa katika uhalali wa Detention Registers (DR). Moja kutokea Central Police Dar na nyingine kutokea kituo cha Polisi Tazara.

DR ya Central iliwasilishwa na D/C Msemwa aliyedai kuwa akilitumikia jeshi la polisi kutokea Central katika kipindi hicho. Ya Tazara, ikiwasilishwa na mkuu wa sasa kituoni hapo.

Hata hivyo shahidi wa utetezi Lembrus Mchome anadai D/C Msema hakuwahi kuwa central polisi kipindi hicho bali alikuwa Oysterbay polisi. Kwamba yeye akiwa mahabusu D/C Msemwa, askari H4323 alimhudumia mara kwa mara Oysterbay Polisi.

Ya Lembrus Mchome yanaweza kuwa na nafuu kwani ni madogo!

Funga kazi ni ya komando Mhina. Mhina anadai kuwa Tazara na baadaye kupelekwa mahakamani kutokea hapo.

Alikuwapo Tazara Polisi mahabusu 23/9/2020 - 25/9/2020 lakini hayumo popote kwenye DR ya Tazara:

View attachment 2035235

View attachment 2035236

Wasaa wa Jaji kuithibitishia dunia kuwa mahakama ni huru na yenye hukumu za haki kwa mara nyingine unajongea.
Unawajaza watu matumaini kwa habari za uongo- mda utasema natamani tu hutahamisha milingoti ya goli wala kusema uamuzi umetolewa na jaji wa michongo
 
Back
Top Bottom