Majunio Wanazingua

Majunio Wanazingua

Mdigokhan

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2022
Posts
942
Reaction score
2,198
Wazazi naomba tuongee kwa dakika 5 tu…

Sisi Tumechoka sana Tukija kuwatembelea makwenu Iwe kipindi cha matatizo Au matembezi ya kawaida, ila Naomba Niongelee sisi ambao tunaofikia makwenu Kuja kutafuta maisha…

Kuna hawa watoto wenu hasa wenye majina ya JUNIO aisee wanatuboa sanaa sanaa Hawavumiliki Ni wasumbufu sana, Utakuta nimekuja labda kwa dada angu au kwa kaka au ndugu yoyote kwa mambo yangu Ya kutafuta kazi ila hawa watoto wenu wamekuwa kero…

Utakuta upo bizee na mawazo yako ila yeye kashakuja kukulukia na unajaribu kumkataza kisilent ocen Ili mama ake asisikie ila yeye Hataki Analiaa Unabaki Unambembelezaa… 😡

Wakati wachakula tunakula kwa woga ivo Tunapakua kidogo ili msijetusema tukiondoka ila ichoicho chakula kidogo Junio anataka na yeye ale Irihali mi mwenyewe sishibi Yani usumbufu tu na utakuta mama ake Anachekelea ujinga 😡

‘We junio muache anko’

Kudadeki inamaana huoni mwanao anavonigasi,Soda yenyewe moja ila hio hio anataka nimpe na yeye anywe Afu anataka tushee mdomo… 😡

Unaongea na simu anakuja na yeye anataka kuongea hajui naongea na nani ananipalamia Tu…TUMECHOKA TABIA ZA WENENU..😡

Saa 12 Alfajili kashakuja mlangoni kugonga mlango Kwa nguvu au Kashaingia mpk chumbani Kunisumbua kitandani Yani kero kero na mama ake anacheka tu ☹️

Unaangalia Tamthilia nzuri ila yeye anakuja anataka uweke ITV aangalie JIJI LETU 😡 How??? Afu mama ake anacheka tu

Ukitoka kutafuta job ushapigwa na jua Ushagombana na konda kwaajili nauli imefemea 100 Unarudi home anakudaka Anataka Zawadi huku analia Afu mama ake anacheka tu… 😡

Mmekaa Mnakula anaanza kukuliza ‘Anko unaondoka lini’ Unabaki unajichekesha afu mama ake nae anacheka tu 😡

Tumechoka Ivo wakatazeni wenenu Wafokeeni hao wakina junio Wanaboa sana, Kuja kwako Sijaja kujisikilizia mimba mimi ila nimekuja kujiweka ili nitafute kazi So wakati wowote naondoka zangu…

Kuna siku mtatufukuza mana atapigwa mtu kofi mpk aone wenge…
 
Wazazi naomba tuongee kwa dakika 5 tu…

Sisi Tumechoka sana Tukija kuwatembelea makwenu Iwe kipindi cha matatizo Au matembezi ya kawaida, ila Naomba Niongelee sisi ambao tunaofikia makwenu Kuja kutafuta maisha...
Nynyi si ndoo mnshadadia haki za mtoto hatakiwi kuguswa.
 
niliwahi kwenda kwa Mjomba wangu miaka ya nyuma, walikuwa wanajiweza sana kifedha.

Ile nafika navua viatu na soksi zangu zilizotoboka nkazificha ndani,nikakaa na kuanza soga na salamu na wenyeji wangu(Anko,mke wake, na mabinamu wa kike)

Mara ghafla junia wa Anko kashafichua soksi zangu kweny kiatu akaja sebuleni katikati ya watu na kusema” Mhhh mama ona soksi za anko zimetoboka halafu zinanuuuka”

Waliangua kicheko sebule nzima, na mimi nikabaki kujichekesha kinafiki ila niliuumia sana mana aliniuumbua kinoma.

SIKUPENDA NA NILIKAA SIKU 1 ILA YULE MTOTO ALIKUWA SHIDA SANA
 
Haya mambo ya kuwasema watoto kama wakubwa wenzenu ndio inapelekea matukio ya ubakaji na ulawiti kwa watoto uongezeke, mtu mzima kama wewe kuweka ligi na mtoto hadi kufungua uzi huoni aibu!?? Kwani ukituliza korodani zako kwako huyo Junia utamuonea wapi???
 
😂😂😂
 
Mlambe kibao kimoja wakati hamna anayekuona, yaani kile cha hakika kabisa. Baada ya hapo kausha tu kama kataendelea na mazoea tena. hata kakitumwa kakuulize swali la kichokozi na mamake (mwulize anko unaondoka lini) akikuangalia tu mkagonganisha macho anakimbilia ndani huko bila kusema kitu.

Ila pambana nawe uwe na kwako
 
Haya mambo ya kuwasema watoto kama wakubwa wenzenu ndio inapelekea matukio ya ubakaji na ulawiti kwa watoto uongezeke, mtu mzima kama wewe kuweka ligi na mtoto hadi kufungua uzi huoni aibu!?? Kwani ukituliza korodani zako kwako huyo Junia utamuonea wapi???
Tulia wewe, wafundisheni watoto adabu.
 
Namshangaa anavyolalamika,, hao ni watoto sipati picha wangekua watu wazima angeliaje🤣🤣
Leo ni ijumaa, Kuna wengine hawatoka out ku-enjoy weekend, hivyo huleta mada zisizo na masiko. Sio junior tu watoto wote huleta usumbufu na binadamu ameumbwa kufikiri kutumia ubongo hivyo suala la watoto halisumbui kichwa kihivyo hasa kwenye malezi. 😀😀😀😀
 
Yeah ni kweli...sema ndo vile watu wengine wameumbwa na makasiriko 🤣🤣🤣🙈
 
Back
Top Bottom