MAJUTO: Nimejenga kimya kimya Mume wangu kajua hanishirikishi tena mambo yake

Sayansi ya akili inasema kiwango cha raha unayotafuta kwa kigezo cha kutafuta furaha huwa ni kidogo tofauti na madhara yanayotokana na furaha uliyopata, sasa twende wakati unajenga kimya kimya ulikuwa na furaha sana ila unaona madhara yalivyokuwa makubwa kwako hata furaha ya nyumba uliyojenga imegeuka sumu, kwenye maisha kamwe usitafute furaha bali tafuta amani ya moyo na afya ya akili, furaha ni adui wa amani ya moyo na afya ya akili, watu wengi waliotafuta furaha wameishia kwenye matatizo makubwa kwakuwa furaha huwa haidumu.
 
Niko kwenye ndoa huu ni mwaka wa 7, katika kipindi chote hicho mambo yalikua mazuri, mume wangu alikuwa akinishirikisha kwa kila kitu na mara nyingi akinunua kitu chake ananunua na cha kwangu. Akinunua kiwanja kimoja, akaandika jina lake, kinachofuata kina majina yangu. Tuna nyumba mbili, ingawa sijachangia chochote, lakini moja akaandika majina yangu na nyingine yake, hata gari letu moja kaniiandika majina yangu. Huwa haniulizi kuhusu pesa yangu, ananiambia hata nisipochangia hajali.

Mwaka jana kuna kitu kilitokea, nilikuwa nanchat na Mama yangu, meseji ikajitokeza juu bila mimi kujua. Mama alikuwa ananiambia kuhusu wapangaji. Kwa maana nilikuwa nimenunua kiwanja kimya kimya bila kumwambia mume wangu na nilishamaliza kujenga na kuweka wapangaji bila kumwambia mume wangu kuwa najenga. Alipoiona aliniuliza, nikamwambia ni wapangaji wa Mama ambao anasimamia.

Hakuuliza tena, nikadhani yameisha kumbe alikuwa ananichunguza. Alifuatilia na kujua nimenunua kiwanja na nimejenga bila kumwambia. Aliponiuliza mwanzo niligoma, lakini alikuwa na ushahidi, kwani alishaongea mpaka na aliyeniuzia. Niliamua kukubali kumwambia ni kweli nina nyumba, nikamuomba msamaha kwa kutomwambia.

Aliniambia kuwa amenisamehe, lakini tangu hapo hanishirikishi tena kwenye kitu chochote. Amefungua biashara nyingine mbili bila kuniambia, kuna nyumba anajenga bila kuniambia, amekaa karibu na ndugu zake. Mwanzo alikuwa hataki kabisa ndugu zake kuwa kwenye biashara, lakini sasa hivi kamleta mdogo wake ndiyo anasimamia biashara zake. Anahudumia kila kitu ndani, lakini shida ni kwamba hanishirikishi tena.

Naumia sana kwani najua nimekosea, lakini inaonekana haniamini tena. Nimeweka nyumba yangu wazi na hata nikipokea kodi namwambia, lakini hataki kusikia, ila namuona kama mtu tofauti sana. Nisaidie nifanye nini nisamehewe na aanze kunishirikisha tena?
Huko ndo ulichokuwa unakitaka furahia matunda yake.

Ulihisi ungemshirikisha angekukataza au!?
 
Wewe ni mwizi bila shaka
 
Wanawake ni viumbe wabinafsi sana wallah, tukiwa nao kwenye mahusiano tusijidanganye kama eti WANATUPENDA, hawana upendo hawa. Imagine mwamba aliokua akiyafanya, kasahau hadi ndugu zake kwa ajili ya mkewe! Inasikitisha sana.
Nimewahi kushuhudia jambo kama hili miaka ya 90 mkoa 1 wa kanda ya ziwa, Mr & Mrs wote ni wqtumishi wa umma, hivo hivo, mwanamke akaanza kujenga nyumba kwa siri, mumewe hajui; hawakuwahi kua na ugomvi, jamaa alivogundua hilo, vikao vilikaa, wazee wa kanisa, ndugu na marafiki; jamaa aligoma na baadae ni kama ndoa ilikufa, wana wajukuu but hawaishi pamoja tena. Wanaume tuna UPENDO sana
 
Ww umesema ulimuomba msamaha,lakin hujaona mabadiliko yyte kwake,Je Katika msamaha ulioomba,ulisema na sababu zako za msingi za kutokumshirikisha Katika manunuzi ya kiwanja pamoja na ujenzi?sababu zako za msingi ni zipi?
 
Back
Top Bottom