MAJUTO: Nimejenga kimya kimya Mume wangu kajua hanishirikishi tena mambo yake

Sayansi ya akili inasema kiwango cha raha unayotafuta kwa kigezo cha kutafuta furaha huwa ni kidogo tofauti na madhara yanayotokana na furaha uliyopata, sasa twende wakati unajenga kimya kimya ulikuwa na furaha sana ila unaona madhara yalivyokuwa makubwa kwako hata furaha ya nyumba uliyojenga imegeuka sumu, kwenye maisha kamwe usitafute furaha bali tafuta amani ya moyo na afya ya akili, furaha ni adui wa amani ya moyo na afya ya akili, watu wengi waliotafuta furaha wameishia kwenye matatizo makubwa kwakuwa furaha huwa haidumu.
 
Huko ndo ulichokuwa unakitaka furahia matunda yake.

Ulihisi ungemshirikisha angekukataza au!?
 
Wewe ni mwizi bila shaka
 
Wanawake ni viumbe wabinafsi sana wallah, tukiwa nao kwenye mahusiano tusijidanganye kama eti WANATUPENDA, hawana upendo hawa. Imagine mwamba aliokua akiyafanya, kasahau hadi ndugu zake kwa ajili ya mkewe! Inasikitisha sana.
Nimewahi kushuhudia jambo kama hili miaka ya 90 mkoa 1 wa kanda ya ziwa, Mr & Mrs wote ni wqtumishi wa umma, hivo hivo, mwanamke akaanza kujenga nyumba kwa siri, mumewe hajui; hawakuwahi kua na ugomvi, jamaa alivogundua hilo, vikao vilikaa, wazee wa kanisa, ndugu na marafiki; jamaa aligoma na baadae ni kama ndoa ilikufa, wana wajukuu but hawaishi pamoja tena. Wanaume tuna UPENDO sana
 
Ww umesema ulimuomba msamaha,lakin hujaona mabadiliko yyte kwake,Je Katika msamaha ulioomba,ulisema na sababu zako za msingi za kutokumshirikisha Katika manunuzi ya kiwanja pamoja na ujenzi?sababu zako za msingi ni zipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…