Makabila haya mtu ukifanikiwa jiandae kujaza ndugu tegemezi kwako ama kukuomba misaada kila mara, ukikataa unaonekana huna undugu

Makabila haya mtu ukifanikiwa jiandae kujaza ndugu tegemezi kwako ama kukuomba misaada kila mara, ukikataa unaonekana huna undugu

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
kuna hii tabia inakera sana kuna baadhi ya watu katika makabila flani wakishaona ndugu / kaka / dada yao katoboa ama ndugu yao wa kike / dada yao kaolewa na mtu mwenye maendeleo si haba basi huenda kujazana huko. Wanakula na kulala hapo bila kazi maalum.

Nyuma ya hii tabia hakukosekani visingizio vya oh tuna umoja, oh tunajaliana, oh sisi wakarimu, n.k lakini haibadilishi uhalisia wa hii tabia ya utegemezi. Hapa hatuzungumzii upendo au kujaliana, NO! Tunazungumzia ile tabia ya watu kujazana kwa ndugu, kaka, dada zao bila shughuli rasmi za kimaendeleo za kuwafanya nao wawe na maendeleo.

Kuna makabila kama wachaga, wakinga na wakurya hawa hawawezagi kuvumilia mtu kuja kukaa kwao awe tegemezi na wala si mgonjwa ama mzee. yaani unavyotoka huko kwenu uwe umeshatoa taarifa juu ya ujio wako, shughuli iliyokuleta, ratiba yako ikoje, upo mpaka lini, mipango yako n.k. Kama ni kusalimiana wala hakuna shida lakini sio kuzidi mwezi.

Hali hii ya makabila yanayolimbikiza utegemezi imewafanya hata ndugu zao wanaowalea wamejikuta wanashindwa kupanga maisha yao kwa kuelemewa na gharama za ulezi wa ndugu wasiopenda kujishug. unakuta mtu kakaa hata miaka miwili kwa ndugu na ni kijana mwenye nguvu ila bado hajahama kujitaftia pake na wala hana shughuli za kimaendeleo.
Makabila haya yaayojazana kwa ndugu ni kama

. Watu wa pwani - wazaramo, wasambaa, wadigo

. Wanyakyusa - hawa huwa wanaendeleza undugu hata ule wa mbali. Yaani hata mke wa mjukuu wa baba mdogo wa babu bado anahesabiwa kama ndugu, kawaida sana kukuta mnyakyusa ana ndugu 100

Waha na Wamanyema kutoka Kigoma

. , warangi

(Niliwaweka wabena kimakosa, hawa hawamo )
 
Kama unakwazika na ndugu kujaa kwako bila shughuli maalumu waambie live kuwa maisha ni magumu waende kwao wakajitegemee au waende Mombasa kuna vitu vya bure wapendavyo.
Kwanini upate shida na upo home kwako.
Speak out!!
Kuna makabila ukifanya hivi wanakutenga, hiki ndicho kinachoogopwa kwamba watakususia misiba, watakususia sherehe, ukienda kijinini kwenu wanakutenga, n.k.
 
Kuna makabila wana umoja lakini sio umoja wa kuwa tegemezi kama wachaga, wakinga, wakuria, n.k yaani kama wewe ni mgeni ukienda kwa ndugu utapokelewa vizuri tu lakini itabidi uwe umeshaweka ujio wako, ratiba yako ikoje, upo mpaka lini, mipango yako, n.k. kama ni kusalimiana ni sawa kukaa hata wiki 2 ila baada ya hapo unarudi kwenye shughuli zako, sahau kuweka kambi hapo ya kudumu. kama huna shughuli na umefika hapo labda muwe mshaelewana mwenyeji wako atakusaidia mtaji na kukuzoesha mazingira ya hapo ili nawe uanze kujitegemea uwe na pako.

zimeridhika na maisha mi naona hivo.

Sasa kuna makabila mengine mmoja akipata utasikia kaja baba, mama, shangazi, mjomba, mtoto wa baba mkubwa, mawifi, mashemeji, n.k yaani wote wanaenda kwa mji mmoja wa mtu mwenye familia moja wanakula na kulala hapo kisa eti wamesikia anafanya benki.😅😅 hii kitu inafanya mtu ashindwe kujikwamua kiuchumi yaani mtu mshahara laki7 au laki 5 mnamgandaa hivyo hawezi tobo.
kwa wachagga wengi huu utaratibu amna.

Makabila haya kwangu niliyoyaona ni kama.

-Wanyakyusa
-Wazaramo
-Wabena

Kuna ile kujifich nyuma ya kivuli cha undugu lakini inakuwa inazidi sasa, mtu hata maendeleo yanashuka
Wasambaa
Wapemba
Wagogo
Wazaramo
Wakurya
 
Kuna aina ya kwanza ya makabila wana umoja lakini sio umoja wa kuwa tegemezi kama wachaga, wakinga, wakuria, n.k yaani kama wewe ni mgeni ukienda kwa ndugu utapokelewa vizuri tu lakini itabidi uwe umeshaweka ujio wako, ratiba yako ikoje, upo mpaka lini, mipango yako, n.k. kama ni kusalimiana ni sawa kukaa hata wiki 2 ila baada ya hapo unarudi kwenye shughuli zako, sahau kuweka kambi hapo ya kudumu. kama huna shughuli na umefika hapo labda muwe mshaelewana mwenyeji wako atakusaidia mtaji na kukuzoesha mazingira ya hapo ili nawe uanze kujitegemea uwe na pako.

Kuna aina ya pili ya makabila Ukiachana na yale makabila ambayo ni mengi ambayo hayataki kabisa ndugu kqenda kuwasalimia haga tutayazungumzia siku nyingine na haya na

Ila kuna hii aina ya tatu ya makabila mengine, yaani mmoja akipata utasikia kaja baba, mama, shangazi, mjomba, mtoto wa baba mkubwa, mawifi, mashemeji, n.k yaani wote wanaenda kwa mji mmoja wa mtu mwenye familia moja wanakula na kulala hapo kisa eti wamesikia anafanya benki.😅😅 hii kitu inafanya mtu ashindwe kujikwamua kiuchumi yaani mtu mshahara laki7 au laki 5 mnamgandaa hivyo hawezi tobo.
kwa wachagga wengi huu utaratibu amna.

Makabila haya kwangu niliyoyaona ni kama.

-Wanyakyusa
-Wazaramo
-wasambaa
-Wabena

Kuna ile kujifich nyuma ya kivuli cha undugu lakini inakuwa inazidi sasa, mtu hata maendeleo yanashuka
How did you do this research?
 
Hapo kwa wanyakyusa ni uongo. Wanyakyusa wazazi kwenda kukaa kwa mtoto wao bila sababu yoyote ni mwiko
 
Back
Top Bottom