Makabila ya Mara mnatia aibu: Wanaume kutahiriwa bila ganzi sio ushujaa, Heshima ya Mwanaume ipo kwenye Pesa na Power

Makabila ya Mara mnatia aibu: Wanaume kutahiriwa bila ganzi sio ushujaa, Heshima ya Mwanaume ipo kwenye Pesa na Power

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Dunia imepuga hatua kwenye nyenzo za utabibu kwenye kutahiri na hakuna mantiki ya kutumia mbinu za zamani zenye maumivu makali bila ganzi.

kuahiri kwa kisu kwa zama hizi ni kama kuhangaika kutafutana majumbani wakati yupo zama za simu za mikononi.

Hayo mambo ya kutahiriwa bila ganzi yaachwe na ikiwezekana serikali ipige marufuku maana ni unyama.

Yani kinachofanyikaga ni ushamba aisee, mvulana anatahiriwa na kisu kikali na kuna muda yule anaetahiri anafanya zoezi taratibu sana ili tu kijana apate maumivu makali, na hapo mvulana anaetahiriwa sharti inabidi asilie wala kuguna,

Hayo mambo ya kutahiriwa kuonesha ushujaa yalishapitwa na wakati, siku hizi mwanaume anapimwa heshima yake kwa pesa aliyonayo iwe anafanya biashara au kazi inayomlipa poa au vyote, mbali na pesa heshima ipo kwenye kushika power katika vyombo vya dola na humu kwa kiasi kikubwa tiketi ya kuingia ni elimu sio kutahiriwa.
 
Heshima ya mwanaume inajengwa na sifa za uanaume kwanza kabla ya kuwa na pesa. Hizo sifa Inatakiwa zimtofautishe na mwanamke.

Sifa zenyewe ni ujasiri, kujua kwamba anamajukumu kwenye jamii, kujijua kwamba Yuko tofauti na mwanamke. Sasa jamii ya hao watu imeona hicho kitendo kinawapa pride wanaume na kujihisi wako tofauti na wanawake.

Natamani kama jamii zote zingeendeleza Mira zinazotufanya tujione tufauti na wanawake na kubeba vizuri majukumu yetu ya kiuanaume.
 
Tunatahiriwa kwa kisu, na hela tunazo.

Uzi wako ungekua na mantiki kama ungeweza kuthibitisha kwamba kutahiriwa kwa kisu kunamzuia mtu kua na hela!

Sisi ni vidume kwelikweli, na wala hatuhitaji ushauri wako. Ukiona mila zetu zinakukera, rudi kwenu huko ukacheze rede na dada zako!

"SASA UNAINGIA MKOA WA MARA, GANGAMALA"
 
Hawa ndiyo unakuta kwenye familia yake anawalea watoto wakiume sawa na watoto wakike. Hajui kwamba anatakiwa awalee na mentality tofauti kwasababu ukubwani wanamajukumu tofauti kwenye jamii. Character ya ujasiri ni muhimu sana kwa mototo wakiume
Mafala wanaona ndio usasa na maendeleo wakati hata mtoto wa kike mwenyewe anaharibika akilelewa kima yai.....

kwanza kwa mtoto wa kiume kusema uaana ume ni pesa naona io kauli imekaa kidhaifu kwakua na mashaka na uana ume wake au teyari ana uchoko ndani yake
 
Kati ya vitu wazungu wamefanikiwa ni kutuaminisha wasomi kwamba njia zetu za kiafrica ni barabaric na njia zao ndiyo kwenda na wakati. Wasomi wamekuwa brainwashed mpaka unawaonea huruma.
 
Back
Top Bottom