Makabila ya Tanzania: Tamaduni zao na Historia yao

Kichuri hupatikana kwenye wanyama wote wanaoliwa na wakurya isipokuwa tu kwenye hawa wanyama
1. Kondoo
2. Nguruwe
3. Sungura
4. Na wanyama jamii ya ndege
5. Nungunungu kwa wanaotumia japo wengi wao hawatumii
 

Wewe hatuoi binamu zetu hapo futa mura
 
Ni kabila zima na pia naona hata kwa Waruri, Wajita, Wakwaya, Wahacha,Wasweta,Wasurwa, Wasimbiti n.k pia hufanya hivyo na nami nawaunga mkono kwa kuwa ni jambo jema.

Hapana sio kabila zima, labda baadhi ya matabaka
 
Mkuu ukuryani ubabe ndio first priority, na ni lazima ujue kutumia silaha za jadi maana ukibanwa na haja usiku unasafiri mita mia tatu kuelekea chooni,kama ni mgeni ukibanwa night unapewa panga na mkuki kuelekea chooni,
Maana huko lolote laweza kutokea na ukakabiliana nalo
Halafu ni muhimu sana kuwapa kichapo wapenzi wetu a.k.a mama watoto huo ndio upendo wa kweli sokoro
 
Kichuri ni mboga ya kikurya(mavi ya mbuzi yale ya kijan yaliyopo tumboni) hii mboga wakurya wanaipenda sana. Kama unataka kuoa sema sio kuwafahamu tu na kuwachora

Hiyo kitu huwa inapelekea mtu kuiba mbuzi ilimradi aipate.

Tamu sana ukiila kwa ugali wa muhogo uliochanganywa na mtama. Usipoangalia, utavimbiwa
 
Tarime unaweza kukuta nyumba nzuri,lakini choo ndani hakuna ,ati wanasema kuweka choo ndani ni uwoga,unatakiwa utoke nje usiku ukapambane na adui yako.sasa sjui unapambanaje na adui wakati umebanwa na tumbo la kuhara
Hizo ni fikra za watu wasioijua Tarime, anyway labda zamani ndo ilikuwa hivyo lakini sio leo. Tarime ni Wilaya kama zilivyo wilaya nyingine huku bara. Kuna mjini na vijijini, na mjini kuna mchanganyiko wa makabila though sio mengi sana lakin issue za mila sijui kutoweka choo ndani kwasababu za kiujasiri hazipo hizo. Labda kwa upande wa vijijini, huko siwez kukusemea coz hata nyumba zenyewe ni zile local (i mean zilizojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi) ambazo hata hivyo hazina hadhi ya kuweka choo ndani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…