Makabila ya wasanii na watu maarufu wa Bongo

Makabila ya wasanii na watu maarufu wa Bongo

yna2, Hivi Diamond umanyemani ni kwa nani? Baba au mama yake?

Cᵃʳᵉᵉᵐ ₜₕₑ ᴸᵉᵍᵉⁿD
 
Anafuata la mahali alipozaliwa
Ndugu huna ujualo, tukutane jukwaa la mapishi[emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]

Cᵃʳᵉᵉᵐ ₜₕₑ ᴸᵉᵍᵉⁿD
 
Hivi kwa tamaduni zetu si mtoto huwa anafuata kabila la baba ?
Mkuu inategemea na kabila. Kuna patrilineal na matrilineal commnunities.
Patrilineal communities, mfano watu wa bara na jamii nyingi za wafugaji, mtoto ni wa baba. Hata urithi unaenda kwa mtoto wa kwanza wa kiume. Mtoto wa kwanza anarithi mali (ardhi, mifugo) ambayo kwa kizazi hiki hizo mali hazipo, lakini pia anakuwa na jukumu la kutunza wadogo zake wote mfano kuoza/ kuozesha, kusomesha etc. Hata dada akiachika anarudi nyumbani kwa kaka mkubwa.

Matrilineal community mfano Luguru, Yao, Makonde, Mwera (I stand to be corrected), hawa ukoo/ ubin unakuwa upande wa mama. Mjomba ndio ana nguvu kwa mtoto. Binti akiolewa yeye ndio muamuzi mkuu na mahari anapanga yeye. Mwanaume kama ana mali, urithi unatakiwa kwenda kwa mtoto wa kiume wa dada na siyo mtoto wake wa ndoa. Mtoto wa kiume wa mwanume atarithi vya mjomba wake. Ulishasikia ule wimbo wa zilipendwa, mjomba amechachamaa amekuja juu harusini.....ndio hayo mambo ya Matrilineal community.

Katika kazi zangu, niliwahi kukutana na famila ambayo watoto baba ni Luguru na mama wa bara. Wale watoto waliniambia wakienda kwa mama bara ni kama wameenda kutembea tu maana kwa baba ni uluguruni, wanajulikana siyo kwao. Wakienda kwa baba pia wanajulikana wao ni wa bara huko ujombani.

Cultural barriers nilikutana nayo pia kwa mahari yangu. baba Sukuma mama wa Pwani and Tanga. Wajomba wakataka kupanga mahari na kuwa vinara wa shughuli. Baba akawaambia kwa wasukuma, huyu ni mtoto wangu siyo wenu. Kama wa kwenu, mbona hamkumsomesha. Pia nilivyovunja ungo baadhi ya ndugu wa pwani walitaka kuniweka mwali na kunicheza ngoma ili wanizawadie kanga na vitenge, Dingi akawagomea.

I am proud of my Dad kwa kweli hasa upande wa mama walipokuwa wanataka nijifunze kuhudumia mume na familia, baba anasema muacheni mwanangu asome. Mpaka leo huwa nawaambia uncles mimi ni msukuma siyo wa huko kwenu.
 
Back
Top Bottom