sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Elimu ni muhimu na wala sio ya kubezwa, Lengo kuu la elimu huwa ni kumkomboa mtu kifikra alafu ndio yanafata mengine, Kwa bahati mbaya hapa nchini jamii nyingi hasa makabila wameigeuza elimu iwe kwajili ya kuwatajirosha kupitia ajira. njia nyingine kama biashara wanapuuza.
zamani makabila machache sanasana wahaya na wachaga waliwekea kipaumbele elimu ya kusoma shuleni kwa lengo kuu la ajira na kiukweli waliweza kujazana sana kwenye ajira safi na kujikomboa kiuchumi, Hali hii pengine ilileta tafsiri tofauti ya ule msemo kwamba elimu ni ufunguo wa maisha kwa kudhani maisha ni kuajiriwa na kuanza kubonda mshahara.
makabila mengine nayo yakaanza kuingilia hii keki, makabila kama wasukuma, wanyakyusa, wapare, wakerewe, n.k. nao wakaanza kuona elimu ndio dili, watoto wakaanza kuwekewa mkazo kusoma, shule zilianza kujengwa, n.k. hatimae nao wakaingia kwenye mgao wa ile keki ya wachache hasa katika ajira zilizohitaji elimu za juu.
Kwa sasa keki hii imekuwa kama ya wote vile maana elimu imesambaa sana, kila kata kuna shule, shule binafsi zipo kibao, vyuo vipo vingi, elimu imerahisishwa sana siku hizi kuna vitabu vya mitihani iliyopota, notes zilizorahisishwa, n.k ufaulu umepanda sana kiasi kwamba siku hizi form 4 na 6 shule nyingi mpaka huko pemba na mikoa ya Lindi unakuta shule haina division 4 wala 0, wanafunzi kibao wanafaulu, vijana wengi sana kutoka kila kona ya nchi kwa sasa wana degree zao na huu ni mwanzo tu.
Mgao umesambaa sana kwa sasa aisee, Sehemu ambazo zamani ulikuta makabila machache yamerundikana siku hizi utawakuta karibu kila kabila tofauti na zamani, Ni kawaida pia kukuta sehemu haina watu wa makabila yaliyojazana zamani ila ukakuta kuna watu wengine wengi wa makabila mengine,.
Elimu kuwa sehemu ya kutoboa tundu lake linazidi kuwa dogo.
Kwa sasa Biashara ndio mpango, tena iwe ile ya kuinuana, huku kwenye biashara mkiinuana mtafika mbali sana, hizo elimu leo mhaya anastaafu, nafasi anaichukua mfipa wa sumbawanga,, kwenye biashara baba anastaafu mtoto wake anapewa kiti.
Kuhusu elimu kwenye biashara inayohitajika huwa inahitajika ya kawaida tu, cha muhimu ni kuiheshimu biashara, wakinga elimu zao za kawaida tu lakini ona maajabu wanayafanya, wapemba wao elimu ni janga lakini ona walivyotusua kwenye biashara, tuliobahatika kusoma na waarabu ama wasomali tumeona wengi wanaishia darasa la 7 au form 4 lakini leo hii sio wenzetu kiuchumi,,, hata wachaga nao walijitafakari mapema wakaona waingie kwenye biashara na kiukweli wametoboa si mchezo.