Makabila yatakayoendelea kutegemea elimu iwakomboe kiuchumi(ajira) yatashuka kimaendeleo

Makabila yatakayoendelea kutegemea elimu iwakomboe kiuchumi(ajira) yatashuka kimaendeleo

Uko sahihi kabisa, professor John Dewey alisema" The aim of Education is not to prepare someone to live but Education itself is Life" nyerere pia alipokua anasisitiza Elimu ya Watu wazima, alisema Elimu haina mwisho, Long life education [emoji137][emoji137]
Kwetu elimu = utajiri. Kama umesoma na hujatajirika basi wewe huna kitu hata kama ni daktari unasaidia kuokoa maisha ya watu wako. Hata kama ni mwalimu unayekisaidia kizazi kijacho kujiandaa na dunia ijayo. Wakati huo huo mifumo ya kiuchumi ilivyosukwa wala hairuhusu watu wengi kutajirika. Ndiyo maana hata Marekani ukisikia nchi tajiri utafikiri sijui nini kumbe asilimia 1% tu ndiyo inamiliki utajiri zaidi ya asilimia 90%. Na ukifuatilia sana wengi wao kwenye hii 1% wala hawajasoma sana na wametumia maisha yao yote kuhangaika kutafuta utajiri maana kutajirika kwa njia za halali siyo kazi nyepesi. Kweli profesa awe na muda wa kufundisha na kufanya tafiti halafu wakati huo huo awe na biashara halali itakayomtajirisha? Labda kama amepita njia za mkato za kwenda kwenye siasa na kuiba huko 😬😬😬

Mara yangu ya kwanza nimefika chuo kikuu kimoja Ujerumani nilishangaa sana. Profesa ambaye umesoma vitabu vyake chuoni anakuja kazini kwa baisikeli. Hana hata gari. Muda wake wote amewekeza kwenye utafiti na kufundisha ili kurithisha maarifa yake kwa kizazi kipya na kijacho. Ndo niligundua hasa maana ya elimu. Tunashangaa kwa nini wenzetu wanapiga hatua lakini ukifuatilia utakuta kwamba misingi ya kinadharia ya mapinduzi yao katika tekinolojia na nyanja zinginezo zimehangaikiwa na wasomi kwa miaka hata 30...life long goal mtu anajaribu tena na tena mpaka anafanikiwa. Na wengi wa waweka misingi hawa ukifuatilia utakuta kuwa waliishi maisha ya kawaida tu lakini wamefanikiwa kuacha alama zisizofutika katika jamii zao.

Tuachane na dhana kwamba elimu = utajiri. Tubadilishe elimu yetu ili iendane na mwendo wa dunia na vijana wetu waende huko wakafanye wakipendacho hata kama hawatatajirika maana kusema kweli kwa jinsi mifumo ilivyosukwa wachache tu ndiyo watatajirika

Na kwenu wazazi. Kama unataka mtoto wako atajirike, elimu ya kidato cha 4 inamtosha. Akimaliza hapo atakuwa anajua mambo ya msingi katika dunia hii. Atakuwa anajua ni kwa nini anatakiwa kupiga mswaki kila siku. Jinsi moyo wake unavyofanya kazi. Jinsi mimba inavyotungwa....na aingie mtaani sasa akapambane. Kama atakuwa vizuri baada ya miaka 10 au 20 hivi atakuwa amepiga hatua japo napo hakuna guarantee. Ila inabidi wawepo na wengine watakaoendelea na masomo ili huyu aliyetajirika akija kuumwa akienda hospitali wawepo madaktari wa kumtibu. Akidhulumiwa pesa wawepo wanasheria wa kumtetea. Na akizaa watoto wawepo walimu wa kumfundishia watoto wake!
 
sky soldier ww ni great thinker....unaona mbali, na una feel Hali halisi ya mtaani.

Watu wanaokubeza ni Kwa sababu wametazama neno moja tu 'elimu' hawajatazama maneno mengine zaidi.

Umeandika 'kuinuana' Hilo hawajaliona wao wamekazana na elimu tu.

Kimsingi, umeongea bonge la pointi. Na nataka nikwambie hata wengine wanakwama kwa sababu hawatazami details za ishus mbali mbali.

Ok, tuseme Hilo elimu ni Bora zaidi km wanavyozungumza (ingawa sikatai); SASA iweje wanaolia ugumu zaidi wa maisha ni wasomi kuliko wasio soma? Kwa nini iwe vice versa....

Naweza kujikuta naandika mengi Sana....lkn itoshe kukuambia kuwa jinsi ulivyofikiri ni hivyo ilivyo. Asikiaye na asikiaye.
Wasomi wanalia ugumu wa maisha kwa sababu ya expectation yao baada ya kumaliza chuo ni kubwa ila mtaani realty hakuna kitu
 
Elimu ni muhimu na wala sio ya kubezwa, Lengo kuu la elimu huwa ni kumkomboa mtu kifikra alafu ndio yanafata mengine, Kwa bahati mbaya hapa nchini jamii nyingi hasa makabila wameigeuza elimu iwe kwajili ya kuwatajirosha kupitia ajira. njia nyingine kama biashara wanapuuza.


zamani makabila machache sanasana wahaya na wachaga waliwekea kipaumbele elimu ya kusoma shuleni kwa lengo kuu la ajira na kiukweli waliweza kujazana sana kwenye ajira safi na kujikomboa kiuchumi, Hali hii pengine ilileta tafsiri tofauti ya ule msemo kwamba elimu ni ufunguo wa maisha kwa kudhani maisha ni kuajiriwa na kuanza kubonda mshahara.


makabila mengine nayo yakaanza kuingilia hii keki, makabila kama wasukuma, wanyakyusa, wapare, wakerewe, n.k. nao wakaanza kuona elimu ndio dili, watoto wakaanza kuwekewa mkazo kusoma, shule zilianza kujengwa, n.k. hatimae nao wakaingia kwenye mgao wa ile keki ya wachache hasa katika ajira zilizohitaji elimu za juu.

Kwa sasa keki hii imekuwa kama ya wote vile maana elimu imesambaa sana, kila kata kuna shule, shule binafsi zipo kibao, vyuo vipo vingi, elimu imerahisishwa sana siku hizi kuna vitabu vya mitihani iliyopota, notes zilizorahisishwa, n.k ufaulu umepanda sana kiasi kwamba siku hizi form 4 na 6 shule nyingi mpaka huko pemba na mikoa ya Lindi unakuta shule haina division 4 wala 0, wanafunzi kibao wanafaulu, vijana wengi sana kutoka kila kona ya nchi kwa sasa wana degree zao na huu ni mwanzo tu.


Mgao umesambaa sana kwa sasa aisee, Sehemu ambazo zamani ulikuta makabila machache yamerundikana siku hizi utawakuta karibu kila kabila tofauti na zamani, Ni kawaida pia kukuta sehemu haina watu wa makabila yaliyojazana zamani ila ukakuta kuna watu wengine wengi wa makabila mengine,.

Elimu kuwa sehemu ya kutoboa tundu lake linazidi kuwa dogo.

Kwa sasa Biashara ndio mpango, tena iwe ile ya kuinuana, huku kwenye biashara mkiinuana mtafika mbali sana, hizo elimu leo mhaya anastaafu, nafasi anaichukua mfipa wa sumbawanga,, kwenye biashara baba anastaafu mtoto wake anapewa kiti.

Kuhusu elimu kwenye biashara inayohitajika huwa inahitajika ya kawaida tu, cha muhimu ni kuiheshimu biashara, wakinga elimu zao za kawaida tu lakini ona maajabu wanayafanya, wapemba wao elimu ni janga lakini ona walivyotusua kwenye biashara, tuliobahatika kusoma na waarabu ama wasomali tumeona wengi wanaishia darasa la 7 au form 4 lakini leo hii sio wenzetu kiuchumi,,, hata wachaga nao walijitafakari mapema wakaona waingie kwenye biashara na kiukweli wametoboa si mchezo.
Tatizo ni kuwa haujui maana ya elimu. Kitu chochote kinachofanya mtu abadili tabia au mtazamo ni elimu.... Labda kama ungesema "shule"
 
Back
Top Bottom