Elimu ni muhimu ila ipewe uzito wake kwa kiwango cha kukukomboa kifikra na sio kuitegemea kama njia pekee ya kupata maendeleo kupitia ajira, Zama zimebadilika.
Zamani ukiwa na gari lako utaendesha kwa uhuru mkubwa sana, ila siku hizi wenye magari ni wengi sana haupo peke yako na kuna foleni, Ndivyo ilivyokuwaga zamani makabila machache sana yalikuwa yana access ama / na uwezo mkubwa wa kusoma shuleni na hatimae kutumia elimu zao kurundikana katika ajira zilizohitaji elimu hasa za vyuoni,
Waliozifaidi sana hizi ajira walikuwa ni wahaya na wachaga.
Kadri miaka inavyozidi kwenda makabila mengine nayo yakaanza kuingilia hii keki, makabila kama wasukuma, wanyakyusa, wapare, wakerewe, n.k. nao wakaanza kuona elimu ndio dili, watoto wakaanza kuwekewa mkazo kusoma, shule zilianza kujengwa, n.k. hatimae nao wakaingia kwenye mgao wa ile keki ya wachache hasa katika ajira zilizohitaji elimu za juu.
Mwamko wa elimu ukazidi kuwa mkubwa kwa makabila mengi zaidi na kusambaa zaidi mpaka vijijini huko ndani ndani, ile keki iliyokuwa ya wachache ikaanza kumegwa na watu wengi zaidi,
Na mpaka sasa tulipo, Eimu imerahisishwa sana kiasi kwamba siku hizi hata matokeo ya form 4 na 6 ni kawaida sana kukuta shule nyingi hazina division 4 wala 0, hii ni mpaka huko Pemba na mikoa ya Lindi ambayo licha ya kuburuza mikia unakuta siku hizi kuna wanafunzi wanafaulu.
Mgao uesambaa sana kwa sasa aisee, Sehemu ambazo zamani ulikuta makabila machache yamerundikana siku hizi utawakuta karibu kila kabila tofauti na zamani, Ni kawaida pia kukuta sehemu haina watu wa makabila yaliyojazana zamani ila ukakuta kuna watu wengine wengi wa makabila mengine,.
Elimu kuwa sehemu ya kutoboa tundu lake linazidi kuwa dogo.
Kwa sasa Biashara ndio mpango, tena iwe ile ya kuinuana kama wachaga, wapemba na wakinga, wachaga nadhani tangu zamani walishaona mbali wakaamua kuruka na kwenye biashara tofauti na makabila mengine, Kimbembe kipo kwa waliokuwa wanategemea elimu pekee, mzee anastaafu na ajira hairithishwi na ndipo penye shida hapo.