Makabila yatakayoendelea kutegemea elimu iwakomboe kiuchumi(ajira) yatashuka kimaendeleo

Kwetu elimu = utajiri. Kama umesoma na hujatajirika basi wewe huna kitu hata kama ni daktari unasaidia kuokoa maisha ya watu wako. Hata kama ni mwalimu unayekisaidia kizazi kijacho kujiandaa na dunia ijayo. Wakati huo huo mifumo ya kiuchumi ilivyosukwa wala hairuhusu watu wengi kutajirika. Ndiyo maana hata Marekani ukisikia nchi tajiri utafikiri sijui nini kumbe asilimia 1% tu ndiyo inamiliki utajiri zaidi ya asilimia 90%. Na ukifuatilia sana wengi wao kwenye hii 1% wala hawajasoma sana na wametumia maisha yao yote kuhangaika kutafuta utajiri maana kutajirika kwa njia za halali siyo kazi nyepesi. Kweli profesa awe na muda wa kufundisha na kufanya tafiti halafu wakati huo huo awe na biashara halali itakayomtajirisha? Labda kama amepita njia za mkato za kwenda kwenye siasa na kuiba huko 😬😬😬

Mara yangu ya kwanza nimefika chuo kikuu kimoja Ujerumani nilishangaa sana. Profesa ambaye umesoma vitabu vyake chuoni anakuja kazini kwa baisikeli. Hana hata gari. Muda wake wote amewekeza kwenye utafiti na kufundisha ili kurithisha maarifa yake kwa kizazi kipya na kijacho. Ndo niligundua hasa maana ya elimu. Tunashangaa kwa nini wenzetu wanapiga hatua lakini ukifuatilia utakuta kwamba misingi ya kinadharia ya mapinduzi yao katika tekinolojia na nyanja zinginezo zimehangaikiwa na wasomi kwa miaka hata 30...life long goal mtu anajaribu tena na tena mpaka anafanikiwa. Na wengi wa waweka misingi hawa ukifuatilia utakuta kuwa waliishi maisha ya kawaida tu lakini wamefanikiwa kuacha alama zisizofutika katika jamii zao.

Tuachane na dhana kwamba elimu = utajiri. Tubadilishe elimu yetu ili iendane na mwendo wa dunia na vijana wetu waende huko wakafanye wakipendacho hata kama hawatatajirika maana kusema kweli kwa jinsi mifumo ilivyosukwa wachache tu ndiyo watatajirika

Na kwenu wazazi. Kama unataka mtoto wako atajirike, elimu ya kidato cha 4 inamtosha. Akimaliza hapo atakuwa anajua mambo ya msingi katika dunia hii. Atakuwa anajua ni kwa nini anatakiwa kupiga mswaki kila siku. Jinsi moyo wake unavyofanya kazi. Jinsi mimba inavyotungwa....na aingie mtaani sasa akapambane. Kama atakuwa vizuri baada ya miaka 10 au 20 hivi atakuwa amepiga hatua japo napo hakuna guarantee. Ila inabidi wawepo na wengine watakaoendelea na masomo ili huyu aliyetajirika akija kuumwa akienda hospitali wawepo madaktari wa kumtibu. Akidhulumiwa pesa wawepo wanasheria wa kumtetea. Na akizaa watoto wawepo walimu wa kumfundishia watoto wake!
 
Wasomi wanalia ugumu wa maisha kwa sababu ya expectation yao baada ya kumaliza chuo ni kubwa ila mtaani realty hakuna kitu
 
Tatizo ni kuwa haujui maana ya elimu. Kitu chochote kinachofanya mtu abadili tabia au mtazamo ni elimu.... Labda kama ungesema "shule"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…