Makaburi ya waislamu Segerea yanatoa funzo kubwa suala la kutunza ardhi. Serikali ikemee kujengea Makaburi yote

Makaburi ya waislamu Segerea yanatoa funzo kubwa suala la kutunza ardhi. Serikali ikemee kujengea Makaburi yote

MELEKAHE

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2023
Posts
1,340
Reaction score
5,588
Habari wadau.

Binafsi ni mkristo. Ila nimependa sana utaratibu uliowekwa kwenye makaburi ya waislamu Tabata segerea.

Kanuni yao namba moja ambayo inakataza kujengea kaburi ni nzuri sana.

IMG_20250102_201524_111.jpg
 
Ni utaratibu wa kuigwa. Mkijengea, mwili umekuwa mifupa chini, huku juu bado hamuwezi kuzika
 
Wewe mkristo MELEKAHE unaelewa kweli nini maana ya kaburi?

Kuna wakristo wengine ni wapuuz sana wewe mmoja wapo

Hujielewi kabisa panya buku wewe
 
Dhehebu gani la ndugu zetu hawa wanaotoa fatwa ya maziko.

Toka maktaba :

Jiji la Wafu la Misri Linavyoonekana kupitia mwanahabari picha maarufu Ed Kashi


View: https://m.youtube.com/watch?v=peWvqqCnC6c
ziara ya kuvutia ya kutembea kupitia Jiji la Wafu huko Cairo, Misri. Necropolis hii inayosambaa, iliyoanzia karne ya 7, ni kitongoji cha kipekee na chenye nguvu ambapo wafu na waliohai huishi pamoja kwenye mitaa hiyo hiyo.
1735840910911.jpeg

Huku zaidi ya watu 500,000 wakimiliki eneo hilo, Jiji la Wafu limekuwa jamii inayostawi kwa wale ambao wamelazimishwa kuingia katika umaskini uliokithiri katika eneo la metro ya Cairo.

Ziara yetu itatupeleka katika Makaburi ya Kaskazini na Kusini, yaliyotenganishwa na Ngome, pamoja na makaburi madogo kaskazini mwa Bab al-Nasr. Tutachunguza historia na usanifu wa makaburi na makaburi, pamoja na maisha ya watu ambao wamejenga nyumba zao hapa.
1735840967264.jpeg

Kuanzia vituo vya kilimo hadi majanga ya asili, mambo mengi yamesababisha ukuaji wa jamii hii ya kipekee. Tunapotembea kwenye barabara na vichochoro nyembamba, tutashuhudia maisha ya kila siku ya wakazi wa Jiji la Wafu na kupata maarifa kuhusu changamoto zinazowakabili
 
Kuna makaburi fulani kule kibonde maji hayana hayajajengewa na wala hayana kifusi, ni flat tu. Ukifika alipozikwa ndugu yako kama unakumbuka unasogeza majani ya miti unafanya sala zako unaondoka. Mwendo ni kuzika juu ya kaburi kwa kaburi, wanabana matumizi ya ardhi japo baada ya muda kaburi la ndugu yako litapotea hutajua wapi ni sahihi alizikwa ndugu yako
 
Lengo la kujengea kaburi ni kuacha ukumbusho. Sasa usipojengea kaburi la mpendwa wako, baada ya miaka mingi mbele na kumbukumbu yake si itapotea!!

Au ndiyo kisrma ukishakuwa marehemu ndiyo basi tena!
 
Labda sijaelewa madhara yatokanayo na kujengea makaburi, naomba kujifunza kutokana na hili
 
For normal people's only .... dunian tumekuja kuacha historia huwez kuzikwa kaburi kama MBWA...
 
Haya makaburi ya kujengea yanachukua eneo kubwa, kama haitoshi linajengewa na mnara kwenda juu. Makaburi ya siku hizi hutoa tafsiri kwamba marehemu alikuwa na hali gani kiuchumi kutokana na kujengwa kikandarasi. Yapo makaburi yanawekwa marumaru na vigae vya gharama kubwa. Imekuwa kama kuna mashindano ya makaburi ya gharama kama yale ya wauza mihadarati wa mexico yana mpaka vijumba na ulinzi mkali
 
Zingatia hakunaga cha bure duniani MALIPO ELFU 50

Ishi na hii kanuni, Hakuna cha bure hapa Duniani, Chochote unachokipokea bure, Ipo siku utalipia Gharama yake.
 
Lengo la kujengea kaburi ni kuacha ukumbusho. Sasa usipojengea kaburi la mpendwa wako, baada ya miaka mingi mbele na kumbukumbu yake si itapotea!!

Au ndiyo kisrma ukishakuwa marehemu ndiyo basi tena!
Kwa mtazamo wako, unadhani kaburi linatakiwa lidumu miaka mingapi au vizazi vingapi kuweka hiyo kumbukumbu? Na kumbukumbu ni ule mwili au zege lililo wekwa juu lenye utambulisho?

Kuna makaburi ya miaka mingi sana, ambayo hata hao ndugu hawayafahamu tena yapo tu yameziba nafasi.
Kwa mtizamo wangu haya makaburi yange jengwa kwa mpangilio maalum, na yote yajengwe kwa kufanana, na yawekewe mawe ya kutamua/kutambulisha na wahusika wapewe hati ya miaka 100, baada ya hapo libomolewe au kama kuna ndugu wanataka kuendeleza kukumbuka, waombe hati tena kwa miak hiyo 100, mpaka uzao huo utakapo koma na wahusika hawapo tena eneo apewe mwingine.

Kuna miji mingi imejengwa na kupoteza kabisa makaburi, sijui hapa kwetu tunakumbuka wafu kwa muda gani, na ni muda gani tunasema sasa basi.
 
  • Thanks
Reactions: DPN
Sijawai kufika makaburi ya kisutu ya waislam. Nayo yamejengewa ? Maana ni makaburi ya muda mrefu na hayajai
 
Labda sijaelewa madhara yatokanayo na kujengea makaburi, naomba kujifunza kutokana na hili
Swali zuri sana!
Msingi wa kujengea kaburi ilikua ni kuweka alama, ukumbusho ili lisipotee HASA makaburi ya mijini penye watu wengi. Ila kutokana na life style na mengine ya "kuiga" suala hili limekua kero kubwa HASA baadhi ya watu wanaohodhi eneo kubwa na kujenga structures kubwa kupelekea mbanano na kupunguza maeneo ya maziko.

Ila bado suala la kujengea kaburi lipo palepale na umuhimu wake..

nimeshuhudia watu wakichimba kaburi juu ya lingine kwa maksudi kwasababu tu lile la awali halina alama, hili ninkosa na ukosefu wa utu.

Pia katika hili tuheshimu imani na tamaduni za kila mmoja.
 
Back
Top Bottom