Makachero wa Special Branch ndani ya harakati za uhuru wa Tanganyika

Makachero wa Special Branch ndani ya harakati za uhuru wa Tanganyika

..lakini Waingereza walikuwa na utu kuzidi Ccm.

..kwa mfano, ktk uchaguzi mkuu wa mwaka 1958 hakuna mgombea wa Tanu aliyeenguliwa kwa sababu zozote zile.

..uchaguzi wa mwaka 2020 uliosimamiwa na Ccm wagombea udiwani 700 wa Cdm walienguliwa.

..sijui kama kina wazee waliounda Tanu na kudai uhuru lengo lao lilikuwa tujitawale na chama chao kigeuke kuwa cha kidhalimu kama Ccm.
Umesahau uchaguzi wa Serekali za mitaa !.

Niliwahi kujiuliza hivi nani alimshauri Mwendazake ule upuuzi.
 
Umesahau uchaguzi wa Serekali za mitaa !.

Niliwahi kujiuliza hivi nani alimshauri Mwendazake ule upuuzi.

..kwa mfano wanachama wangapi wa Tanu walitupwa mahabusu, au kuhukumiwa vifungo.

..Halafu linganisha na kilichotokea kwa Chadema ktk Tanganyika / Tanzania huru ktk awamu ya 5.

..Kuna kiongozi yeyote wa Tanu alipigwa na kuwa kilema kama ilivyomtokea Tundu Lissu ktk Tanganyika / Tanzania huru?

..Kuna viongozi wa kinamama wa Tanu aliyepigwa, kufungwa, na kudhalilishwa kama Esther Bulaya, Esther Matiko,na Halima Mdee?

..Kati ya Twinning na Jpm nani alimzidi mwenzake kwa dhuluma na ukatili?

Cc Pascal Mayalla , Nguruvi3, Mohamed Said
 
shikamoo Babu!! hivi!! kwa nini una hasira sana??? kwa mfano Unaleta hoja kwa nguvu!! nguvu! tuu!!,,,na vitisho! pili kule JohanesBurg ulikwendaje wkt Tanzania hatukuruhusiwa kwenda huko miaka hiyo??

ulitumia passport ya wapi?? kufika kwa makaburu! je waweza ionyesha hapa km photo copy?.....na kama ulitumia pass bandia ilipe serikali kwa sababu ulidanganya!....
 
Ntemii,
Sikulaumu.

Kitabu cha Abdul Sykes kilipoingia nchini 1998 na watu kusoma yaliyokuwamo wengi walitaabika.

Lakini hawakusema niliyoandika ni ya "kusadikika," na sababu ni yale maelezo na ushahidi wa nyaraka na picha.

Naelewa kwa nini na wewe unapata tabu kuamini.

Akili inakataa na sababu ni kuwa umeaminishwa sicho.

Kwani unajua kuwa kadi ya TANU ya Julius Nyerere ni No. 1 kama President wa TANU na aliandikiwa na Ally Sykes na ndiye aliyechapa kadi 1000 za kwanza kutoka mfukoni kwake?

Unajua kuwa kadi No. 2 ni yake Ally Sykes na kadi No. 3 ni ya kaka yake Abdul Sykes?

Jiulize imekuwaje kadi hizo za hawa ndugu wawili ziwe za mwanzo pamoja na Nyerere zikifuatana?

Yako mengi usiyoyajua na nikikueleza utazidi kushangaa.

View attachment 2251174
Atakasirika zaidi.mi ni mkristo nasikia raha kusoma makala zako kama mtanzania.Naelimika sana Mzee Said endelea kutujuza historia yetu.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
 
Shida ni moja tu mzee wangu Mohamed, kuna watu wameisha karirishwa historia na wameamini sana kwenye hiyo historia na hawataki kuujua ukweli au kusikia historia mbadala na ile walioaminishwa, suala hapa sio uislam na waislam katika harakati za uhuru, ni kuwa hii historia mpya unayohadithia inatishia ushujaa aliojengewa Hayati Nyerere!
 
Back
Top Bottom