Umesahau uchaguzi wa Serekali za mitaa !...lakini Waingereza walikuwa na utu kuzidi Ccm.
..kwa mfano, ktk uchaguzi mkuu wa mwaka 1958 hakuna mgombea wa Tanu aliyeenguliwa kwa sababu zozote zile.
..uchaguzi wa mwaka 2020 uliosimamiwa na Ccm wagombea udiwani 700 wa Cdm walienguliwa.
..sijui kama kina wazee waliounda Tanu na kudai uhuru lengo lao lilikuwa tujitawale na chama chao kigeuke kuwa cha kidhalimu kama Ccm.
Umesahau uchaguzi wa Serekali za mitaa !.
Niliwahi kujiuliza hivi nani alimshauri Mwendazake ule upuuzi.
Atakasirika zaidi.mi ni mkristo nasikia raha kusoma makala zako kama mtanzania.Naelimika sana Mzee Said endelea kutujuza historia yetu.Ntemii,
Sikulaumu.
Kitabu cha Abdul Sykes kilipoingia nchini 1998 na watu kusoma yaliyokuwamo wengi walitaabika.
Lakini hawakusema niliyoandika ni ya "kusadikika," na sababu ni yale maelezo na ushahidi wa nyaraka na picha.
Naelewa kwa nini na wewe unapata tabu kuamini.
Akili inakataa na sababu ni kuwa umeaminishwa sicho.
Kwani unajua kuwa kadi ya TANU ya Julius Nyerere ni No. 1 kama President wa TANU na aliandikiwa na Ally Sykes na ndiye aliyechapa kadi 1000 za kwanza kutoka mfukoni kwake?
Unajua kuwa kadi No. 2 ni yake Ally Sykes na kadi No. 3 ni ya kaka yake Abdul Sykes?
Jiulize imekuwaje kadi hizo za hawa ndugu wawili ziwe za mwanzo pamoja na Nyerere zikifuatana?
Yako mengi usiyoyajua na nikikueleza utazidi kushangaa.
View attachment 2251174
Kabwe...Atakasirika zaidi.mi ni mkristo nasikia raha kusoma makala zako kama mtanzania.Naelimika sana Mzee Said endelea kutujuza historia yetu.
Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app