Mapolomoko
JF-Expert Member
- Feb 16, 2013
- 1,751
- 422
we fundi?
Hahahaaaa!!! mtani upo?. kupaua ndiyo kazi yangu. haujambo mwana kwetu, hongera kwa ushindi. japo ulinisemea nikapigwa BN. sema unamjengo nije nikuezekee?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
we fundi?
Hahahaaaa!!! mtani upo?. kupaua ndiyo kazi yangu. haujambo mwana kwetu, hongera kwa ushindi. japo ulinisemea nikapigwa BN. sema unamjengo nije nikuezekee?
umesahau mbao za kona
Ha ha ha ha nipo mtani ninampango wakuezeka kibanda changu kigamboni nipe makadirio
makadirio bila vipimo tuma ramani kwa email yangu ipo hapo juu
Sema falcia board 1*8 au fisha.
Poa poa mtani nikikumbukaga ile issue nacheka sana
mkuu unaweza ukawa na nyumba ya vyumba viwili lakini kubwa zaidi ya nyumba ya vyumba vitano, hakuna standardized size ya ukubwa wa chumba.. kwahio bila kujua actual floor size ni vigumu mtu kujibu chochote
kwanza nikushauri tumia 2*3 badala 2*2 zinaleta ufanisi wa kazi ikizingatia 2*2 za siku hizi ni kama 1.5*2.
2*4 kwaajili ya makenchi hazina shida. kwaio kwa vipimo hivyo na kama paa litakua kama ulivyosema kutakuwa na kenchi 3 nzima ambazo zitatumia mbao 8 kwa moja hivyo zitakua 24. kutakua na nusu kench 6 ambazo ni mbao 4 kwa moja.hivyo zitakuwa 24 pia. kutakuwa na mbao za mtamba panya 11. kwa hivyo 24+24+11=59 (2*2).unaweza ukaongeza 4.
na hizo za kushikia bati ziwe 26 unaweza ukaongeza 4 pia kwa hizi.
umesahau mbao za kona
Ameshakupa kipimo hiki hapa kwa nje (urefu 38ft upana 24ft ukubwa), na huu ndio msingi wa kwanza wa uezekaji then unaangalia ramani inasemaje, uzuri umesema sio carpenter ila sio mbaya kama ukichukua hiyo ili ukijenga nyumba yako nyingine ya kule Kigamboni fundi asianze kukuzingua kwa kukupa process ndefu ili akutoe ela za ufundi nyingi
makadirio bila vipimo tuma ramani kwa email yangu ipo hapo juu
Tofauti ipo upande wa zile mbao za 2x2 ambazo zinapigwa kama futi moja moja kama unaezeka vigae hata lile bati tuliozoea kuliita la South japo linatengenezwa Alaf na makampuni mengine ila kwa upande wa mbao za kenchi ni idadi sawa iwe ni bati au vigae. Ngoja wataalamu waje watafafanua kiutaalamu wengine ni risasi kidoleHivi vigae vinatumia kama mara mbili ya mbao zaidi ya bati au tofauti sio kubwa sana alafu unashauri bati za aina gani zinazodumu kutokana na uzoefu wako..., sababu siku hizi unaweza kuweka bati leo miezi sita tu utafikiri nyumba ilijengwa wakati wa ukoloni..
Hivyo vipimo ametoa baada ya mimi kumpa huo ushauri, mwanzo kulikuwa hakuna kipimo chochote
Hivi vigae vinatumia kama mara mbili ya mbao zaidi ya bati au tofauti sio kubwa sana alafu unashauri bati za aina gani zinazodumu kutokana na uzoefu wako..., sababu siku hizi unaweza kuweka bati leo miezi sita tu utafikiri nyumba ilijengwa wakati wa ukoloni..
Kwahio na bati za south zinakula mbao zaidi ?, Hizo za 2 x 2Tofauti ipo upande wa zile mbao za 2x2 ambazo zinapigwa kama futi moja moja kama unaezeka vigae hata lile bati tuliozoea kuliita la South japo linatengenezwa Alaf na makampuni mengine ila kwa upande wa mbao za kenchi ni idadi sawa iwe ni bati au vigae. Ngoja wataalamu waje watafafanua kiutaalamu wengine ni risasi kidole
mbao zinazo ongezeka sana ni papi 2x2 au 2x3. bati la kawaida papi hadi papi ni sm 90, bati za vigae papi hadi papi sm 54,nati zinazodumu ni simba dumu
Kwahio na bati za south zinakula mbao zaidi ?, Hizo za 2 x 2
Yes zinakula mbao zaidi kutokana na migongo yake ilivyokaa ili mtu anapotembea juu lisijikunje maana migongo ya bati la kawaida huwa imenyooka kuanzia mwanzo mpaka mwisho hivyo ukipiga mbao mbali mbali kama vipimo vinavyotaka inakuwa poa lakini hili la South kila mgongo unajitegemea though wengine hupiga mbao kama hili bati tulilolizoea ila kasheshe kama kutakuwa na ukarabati juu inabidi utambae kwenye maeneo ambayo kuna papi tofauti na bati zetu hizi za kawaida unatambaa
Kweli mkuu bati za siku hizi kimeo mkuu mpaka basi, Uganda bado wanatengeneza bati standard kwa wale wanaoishi kanda ya ziwa wameona utofauti wa bati za Uganda na za kwetu hata kama zipo gauge moja. Kikubwa ni kununua bati kwa mtu ambae unaamini anauza bati genuine maana kuna mzigo kibao umechakachuliwa upo sokoni tena hata hizi za South nazo ndio balaa kuna zingine ukipiga bati leo baada ya miezi 6 zinakuwa zimepauka zinakuwa na rangi ya kijivu kwa mbali. (angalau walionunua miaka ya 2009 kushuka chini haya mabati yalikuwa hayajachakachuliwa hivyo ukinunua bati mkuu kuwa makini ikiwezekana nenda kiwandani kabisa kama upo Dar kwani ukiwapa ramani wanakutolea bati refu kuanzia mwanzo mpaka kwenye kofia na kukupa mabati ya size ya kawaida kutokana na ramani ya nyumba yako)Ila mkuu hata hizi zetu za kawaida nakushauri ukanyage kwenye papi (yaani pale unapoona misumari) kama hutaki kujikuta umeangukia kwenye ceiling board au kwenye sakafu kabisa.., (tena kama umechukua gauge ndogo) hizi bati ni kama karatasi