Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Kweli mkuu bati za siku hizi kimeo mkuu mpaka basi, Uganda bado wanatengeneza bati standard kwa wale wanaoishi kanda ya ziwa wameona utofauti wa bati za Uganda na za kwetu hata kama zipo gauge moja. Kikubwa ni kununua bati kwa mtu ambae unaamini anauza bati genuine maana kuna mzigo kibao umechakachuliwa upo sokoni tena hata hizi za South nazo ndio balaa kuna zingine ukipiga bati leo baada ya miezi 6 zinakuwa zimepauka zinakuwa na rangi ya kijivu kwa mbali. (angalau walionunua miaka ya 2009 kushuka chini haya mabati yalikuwa hayajachakachuliwa hivyo ukinunua bati mkuu kuwa makini ikiwezekana nenda kiwandani kabisa kama upo Dar kwani ukiwapa ramani wanakutolea bati refu kuanzia mwanzo mpaka kwenye kofia na kukupa mabati ya size ya kawaida kutokana na ramani ya nyumba yako)
Vipi za Uganda kwa Kanda ya Ziwa unajua dealer anazo au ndio inabidi kuagiza (ambapo mambo ya ushuru tena na usafiri huenda ikawa issue).
Ila kama hata mtu haupo Dar naona bora ni kuongea kiwandani wakupe bati za moja kwa moja kama kuna uwezekano wa kuzifold na kuzisafirisha