Makadirio ya ujenzi Contemporary ya room 3

Makadirio ya ujenzi Contemporary ya room 3

Inawezeka kweli gharama za ujenzi zikawa juu kwa mikao kama Morogoro, Tanga , lindi , kilimanjaro na Arusha kuliko Dar es salaam ?
Hyo factor haileti tofauti kubwa sana kwenye gharama za ujenzi,gharama za ujenzi zinatofautiana kulingana na sqm za jengo na aina ya building materials used
 
Mkuu kuuliza ni ujinga, umejuaje kuwa ni 190sqm? Na je nikiwa na eneo la 111.5sqm kipi nipunguze itoshee nyumba kama hiyo?
Kwenye michoro imeonyeshwa hapo 189sqm, eneo la 111.5sqm ni dogo sana kwa nyumba ya ukubwa huo, utapunguza dimensions za vyumba, sebule, utapunguza idadi ya vyoo..otherwise eneo lako ni dogo sana kukaa hiyo nyumba.
 
Na akipunguza hzo dimensions basi hyo nyumba haiwezi kuwa na maana tena,nafikiri solution nikutafuta anangalau eneo lenye sqm 300 kwenda mbele
 
Nimefanya calculation mkuu ,
Mimi ni Injia by professional

Na kwa ukubwa wa kiwanja chako hutaweza kujenga nyumba kama hyo.

Njia pekee either upungunze ukubwa wa nyumba,seble na baadhi ya vitu lakini sioni kama itapungua sana .
Injinia hiyo nyumba ina square meter 189????
Unanipa mashaka na wasiwasi mkubwa mno
 
Mbona unabishana na mchoraji? Au hujaona imeandikwa hapo 189sqm? Kwa kuangalia tu huwezi coz kuna kona kona, otherwise upige hesabu kutoa hizo kona na kuongeza palipozidi, tofauti na hapo utatumia CAD ku-calculate.
Huyo pia amekosea, haina 190sqm
Bali Ina 242sqm
 
Kwanini kila room usiweke choo chake? Hafu kimoja kikawa public. Ila ramani kali sana.

Nahisi gharama kubwa itakuja kwenye izo mbwembwe za nje, I wish ungeweka plain upunguze mbwembwe za ukuta.
Katika vitu ambavyo sipendi kabisa ni huu mtindo wa sisi wabongo kuvipa vyoo vya nyumbani kwetu jina la ''public toilet'', Vivyo hivyo, ni huu mtindo wa mtu kutaka kuweka kila chumba na choo chake. Vyoo viwli kwenye nyumba hizi za kawaida vinatosha sana mengine ni kuongeza gharama tu.
 
Mbona unabishana na mchoraji? Au hujaona imeandikwa hapo 189sqm? Kwa kuangalia tu huwezi coz kuna kona kona, otherwise upige hesabu kutoa hizo kona na kuongeza palipozidi, tofauti na hapo utatumia CAD ku-calculate.
Nitakueleza, Ila Kuna injinia hapa nataka nimchallenge. Subiri majibu yake then nami nitaeleza
 
Nitakueleza, Ila Kuna injinia hapa nataka nimchallenge. Subiri majibu yake then nami nitaeleza
Kwa hiyo umesimamia msimamo wako kuwa ni 242sqm, kwamba floor plan ina 242sqm mkuu? Eleza jinsi ulivyopata hivyo sqm nami nijifunze.
 
Hapo kwenye public toilet moja unaweza ukaigawa kati maana vyoo vikubwa hivyo
Ukaigawa kati ukatengeneza sehenu ya washing machine juu ukaweka shelves kwa ajili ya kuwekea vitu vya laundry
Unapenda kufua fua wewe
 
Kwa hiyo umesimamia msimamo wako kuwa ni 242sqm, kwamba floor plan ina 242sqm mkuu? Eleza jinsi ulivyopata hivyo sqm nami nijifunze.
Ndiyo msimamo wangu ni huo, ukubwa wa nyumba ni 242sqm, nitaeleza baada ya injinia kuja kusema hiyo 189sqm imepatikanaje
 
111.5sqm naweza jenga contemporary ya vyumba vitatu(master moja), dining, kitchen na public

Nataka kama hii
Hiyo 111sqm ni ukubwa wa kiwanja au ukubwa wa nyumba? Sijaelewa, na sorry kwa kuingilia Kati
 
Ndiyo msimamo wangu ni huo, ukubwa wa nyumba ni 242sqm, nitaeleza baada ya injinia kuja kusema hiyo 189sqm imepatikanaje
Ukubwa kwa maana ya floor plan area au unasemea ukubwa gani?
 
Gharama za ujenzi zinategemea sana na total square meters za jengo lako,
The more sqm znakuwa nyingi the more gharama za ujenzi wa jengo lako znakuwa kubwa
Hii si kanuni na haina sana ukweli
Square metre zinaweza kuwa kubwa lakini gharama zikawa ndogo, na square metre zinaweza kuwa ndogo Ila gharama zikawa kubwa. Inategemea na building materials zitakazotumika
 
Ukubwa kwa maana ya floor plan area au unasemea ukubwa gani?
Nilitamani kuona majibu ya injinia kwenye hili

Anyway, nikuulize swali je floor area ni ukubwa wa nyumba? Au floor area ni nn kwa unavyofahamu
 
Nilitamani kuona majibu ya injinia kwenye hili

Anyway, nikuulize swali je floor area ni ukubwa wa nyumba? Au floor area ni nn kwa unavyofahamu
Floor plan inaonyesha eneo, zingatia neno eneo (sio ukubwa) wa nyumba. Inaonyesha nyumba inachukua eneo kiasi gani(surface area), ndio maana ikaandikwa Square metre na sio cubic metre
 
Back
Top Bottom