Huwezi kutenganisha maendeleo na Private Sector, hayo unayoyasema yote, ati JKT- ni kama Ujamaa vyote vilishindwa hata huko China unakosema. China iligundua hiyo mwaka 1978 Deng alivyochkua ngazi, akafanya mabadiriko, kuleta sector binafsi na ubepari -wakaitwa Socialism in Chinese Charateristics, Deng mwnenyewe akasema afadhali wachache watajirike kwanza, pole pole watatajirika wengi na kuiponya nchi kwa kuwasaidia wengi. Wakaifungua nchi kkwa uwekezaji, akaanzisha mji wa Shenzhen. China imejengwa na Private sector lakini walifanya centralizastion ya Financing na ku-control major import & export. About 98% ya companies in China ni Private sector na ndiyo ina contribute kwa 80% ya maendeleo ya uchumi wa nchi.
Lakini siyo mambo ya wizi, au ulaghai, llazima ufuate sheria, system ya nidham ya hali juu, hmna mtu aliye juu ya sheria. Hawauzi raslimali za nchi.
Strong Private sector, Sheria zifuatwe na stability ndiyo unapata sustainable economy. Usishahu strong institutions.
“Unaniletea hadithi za China kana kwamba tunakunywa chai moja na wao?
China ilifanikiwa si kwa sababu ya Private Sector,
ila kwa sababu Private Sector yao ilizaliwa ndani ya mfupa wa Taifa,
sio kwenye masaburi ya wafanyabiashara wajanja kama kwetu!”
Angalia vizuri, kabla hujaniletea takwimu za Shenzhen:
China ya Deng haikufungua nchi waliifungua baada ya kufungua akili ya taifa.
Umeelewa?
Private Sector yao ilitokea kwenye utaratibu,
siyo kwenye michepuko ya mijini.
Wewe unanishika shati unaniambia:
“98% ya makampuni China ni private sector.”
Ninakujibu:
Ndio! Lakini nani anamiliki hiyo private?
Wachina.
Siyo kaka wa rafiki wa Waziri.
Siyo mfanyabiashara aliyekuja na mkoba wa ‘donation’.
Siyo watu wanaotazama nchi kama fursa ya kuiba Rostam
Umesema China wana rule of law.
Hapa nakuambia kama mwendawazimu:
Sheria zetu ziko wapi?
Ziko kwenye mabango na hotuba.
Sio kwenye vitendo.
China ukiiba pesa ya umma -
unakutana na ukuta wa risasi.
Hapa ukiiba -
unakutana na transfer.
Na unajua tofauti ya Private Sector ya China na ya kwetu?
Private Sector yao inajengwa juu ya misuli ya Taifa.
Private Sector yetu inajengwa juu ya mifupa ya Taifa.
Wao wanatumia private sector kuinua Taifa.
Sisi tunatumia Taifa kuinua private sector.
Umesema:
“Strong institutions! Stability! Private sector!”
Ninakujibu kama mzimu aliyekunywa ugali bila maji:
Institutions gani?
Taifa lenye vijana wanaolelewa na tamthilia za mapenzi,
muziki wa ngono, na michezo ya kamari ya Azam Sports,
halina Private Sector - lina Private Suffer.
Private Sector bila utamaduni wa uzalendo ni soko la minyonyo,
kila mmoja ananyonya anapoweza.
China walifanikiwa kwa sababu kabla hawajapeleka mtu Shenzhen,
walipeleka kizazi kizima kwenye:
Nidhamu
Uzalendo
Kujiamini
Maabara
Kambi za vijana
Mfumo wa kufikiri kwa taifa moja
Sisi?
Tunapeleka vijana kwenye:
BET
Wasafi Festival
TikTok
Kamari
Azam Two romantic series
Halafu tunataka kuwa China?
Mwisho, niseme kitu cha mwisho kama kichaa wa hekima:
Taifa ambalo vijana wake hawawezi kuimba wimbo wa taifa ila wanaweza kuimba wimbo mpya wa msanii kabla hata haujatoka - hilo taifa halijengi Shenzhen, linajenga Shenzi-zhen.
Acha utani.
Kabla hujaniletea China, leta kwanza fikra,
halafu tutajenga Private Sector ya maana.