CHAGOSI GERALD
Senior Member
- Jan 25, 2020
- 162
- 286
Ndugu zangu,
Kizazi cha taifa hakipotei kwa njaa, hakipotei kwa maradhi, hakipotei kwa umasikini tu. Kizazi cha taifa hupotea pale fikra zake zinapotekwa na kupotoshwa. Hii ndiyo hatari kubwa inayotukabili leo.
Tazameni vyombo vya habari vilivyotujaa ndani ya nyumba zetu. Vijana wetu wakiwasha televisheni hukutana na nini? Hukutana na tamthilia za mapenzi zisizo na uhalisia wa maisha ya Kiafrika. Hukutana na hadithi za uongo zinazowajaza kwamba dunia ni mapenzi tu, kana kwamba maisha hayana jasho, heshima, wala wajibu.
Hawa vijana wanajifunza nini? Kujinyonga kwa sababu ya mapenzi, badala ya kusimama kama wapiganaji wa maisha. Ndio maana nasema: “mnaprogram watoto wetu kuamini kuwa hakuna maisha zaidi ya mapenzi.”
Na mnapanga yote haya kwa makusudi: mnachagua muda wa chakula cha usiku, muda ambao familia hukusanyika, na hapo ndipo mnatuwekea sumu ya fikra.
Na wapi tena? Vijana wetu wakihama kidogo, wanakutana na Azam Sport 1, 2, 3. Mnafundisha michezo si kama afya na mshikamano, bali kama kamari na biashara ya tamaa. Mtoto wetu badala ya kuwa mwanasayansi wa michezo, mnampotosha kuwa mcheza kamari wa michezo.
Wakihama tena, wanakutana na “Sinema Zetu” ambazo si zetu. Hazileti historia ya mapambano yetu, hazijengi mshikamano wa taifa, bali huchimbua siri za familia na matusi ya kifamilia.
Na kisha kuna Wasafi Media. Mnawafundisha watoto wetu kwamba maisha ni muziki na starehe. Mnamwambia mtoto aamini kwamba mafanikio makubwa ni kuwa msanii, si mvumbuzi; ni kuwa nyota wa muziki, si mjenzi wa taifa.
Ndugu zangu, haya yote si makosa ya wazazi peke yao. Tatizo ni serikali kuacha wafanya biashara pekee washikilie mfumo wa media. Wamepanga agenda zao: kuwafanya vijana wetu wasifikiri, bali wabaki wateja wa michezo, kamari, muziki, na mapenzi. Taifa lisilo na vijana wanaofikiri ni taifa lililouzwa.
Hapa ndipo JKT ilipaswa kusimama. JKT kama shule ya uzalendo, kama chombo cha mshikamano wa taifa, ilipaswa kushikilia vyombo vya habari kwa ajili ya malezi ya kizazi. Ilipaswa kuunda redio na televisheni zinazowafundisha vijana falsafa ya taifa, historia ya mapambano, ubunifu, sayansi, na mshikamano wa kitaifa.
JKT ilipaswa kuwa mfumo wa mawasiliano wa kizazi kipya, ikiwapa vijana wetu programu zenye mafunzo, ubunifu, na falsafa. Kwa nini mtoto wetu asione vipindi vya uvumbuzi? Kwa nini asione michezo ya maabara na miradi ya kilimo badala ya kamari? Kwa nini asione tamthilia zetu za kihistoria na fasihi zetu za uzalendo badala ya nakala za kigeni?
Ndugu zangu, tatizo kubwa si kwamba vijana wetu hawana ndoto, bali kwamba ndoto zao zinaporwa na kuuzwa kupitia skrini za televisheni. Ndiyo maana nasema: JKT ndilo lililopaswa kushikilia mfumo wa media ili kulinda roho ya taifa.