johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Mwenezi wa CCM Komredi Amos Makala amesema katika Ziara yao Katavi na maeneo mengine watasikiliza kero za wananchi lakini siyo zile zilizoko mahakamani
Makala amesema wanajua Wananchi Wana changamoto mbalimbali na kimbilio lao ni CCM
Source Jambo TV
====== ======
KAULI YA MAKALLA
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Amosi Makalla amesema lazima Watu wajue kuwa mambo yaliyo Mahakamani yanamalizwa Mahakamani na hakuna Kiongozi wa Serikali au Chama anayeweza kuingilia Mhimili wa Mahakama.
Akiongea Mkoani Katavi leo wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Emmanuel Nchimbi na Viongozi wengine, Makalla amesema:
“Ninaposikiliza kero Mimi nimetoka kwenye Ukuu wa Mkoa, la kwanza tutasikiliza kero ambazo hazipo Mahakamani, siku moja nipo Mbeya kuna Mtu alikuja na makabrasha akasema Mahakama ya kwanza nilishindwa, Mahakama ya Wilaya nillishindwa, Mahakama Kuu nilishindwa, Mahakama ya Rufaa nilishindwa, wewe umeteuliwa na Rais tengua hizo hukumu zote, itawezekana wapi!?”
“Lazima Watu wetu wajue mambo yaliyo Mahakamani yanamalizwa Mahakamani, tutakachokupa ushauri basi kata rufaa, tunachowasaidia Wananchi yale mashauri ambayo yanahitaji mambo ya utawala, kwahiyo ukija mkutano wa hadhara tunawakaribisha lakini usilete mambo ambayo yapo Mahakamani, ukweli lazima usemwe itakuwa tunawadanganya tu Watu kwamba hili unajua lipo Mahakamani tutakusaidia, sio kweli lazima wakati mwingine tuwe Wakweli”
Katika hatua nyingine Makalla amesema katika jitihada za kuufanya Mkoa wa Katavi uwe na umeme wa uhakika, mradi kuunganisha Mkoa huo na gridi ya Taifa unaendelea kwa kasi na sasa umefikia 56%.
“Nilikuwa natembelea mara kwa mara kwenye jenereta zetu, umeme hautoshi unakatikakatika na huku mvua za radi zikianza kila saa umeme unakatika na wakati huo unaangalia Simba na Yanga halafu umeme unakatika, ninayo heshima na furaha kusema tayari Serikali inaendele kutekeleza wa kuunganisha Katavi na gridi ya Taifa, mradi umefikia 56% na kasi ya mradi huo mtaiona ikiendelea lazima tuwe na umeme wa uhakika.”
=====
KAULI YA NCHIMBI
Upande wa Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi naye amesema:
Katika mambo tutakayoshughuliki kama kero hatutagusa ambayo yapo Mahakamani, ndio utaratibu wa Utawala Bora.
Katika kutekeleza sera za CCM, moja ya jambo muhimu ni kusimamia suala la Utawala wa Sheria, wakati wote tutakuwa tunahamasisha na kuziwezesha Mahakama kutenda haki wakati wote bila kuingilia katika maamuzi yake.
Nchi inayotaka kufanikiwa lazima isimamie Utawala wa Sheria, ukijenga utaratibu wa kuingilia Mahakama katika mfumo wa Sheria siku moja zitawaumiza wote.
====
Pia soma:
- Makonda kusikiliza kero zenye kesi Mahakamani Arusha, asema yupo tayari kupoteza chochote mradi mtu apate haki yake
- Makalla: CCM tunaheshimu Mahakama kama chombo cha kutoa haki, hatuingilii kesi zinazosikilizwa huko
- Katibu Mkuu CCM kumpinga RC Arusha kimafumbo anataka kumfurahisha nani?