Makalla atua Katavi na kusema Watasikiliza kero za Wananchi lakini siyo zile zilizopo Mahakamani

Makalla atua Katavi na kusema Watasikiliza kero za Wananchi lakini siyo zile zilizopo Mahakamani

Acha tu mkuu!!kuna safari ndefu sana,sasa imekuwa ni kusifia tu,hali ya maisha ni ngumu na hao masikini ndio wanachezeshwa wimbo wa kusifia wasio ujua,wakati hao viongozi hawana shida,pesa kila siku inaliwa tu
Mi nalaumu wasomi na viongozi wa dini badala ya kusaidia wananchi wasio na sauti wamegeuka wasifiaji wakifukuzia maokoto pekee
 
Mwenezi wa CCM Komredi Amos Makala amesema katika Ziara yao Katavi na maeneo mengine watasikiliza kero za wananchi lakini siyo zile zilizoko mahakamani

Makala amesema wanajua Wananchi Wana changamoto mbalimbali na kimbilio lao ni CCM

Source Jambo TV

====== ======

KAULI YA MAKALLA
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Amosi Makalla amesema lazima Watu wajue kuwa mambo yaliyo Mahakamani yanamalizwa Mahakamani na hakuna Kiongozi wa Serikali au Chama anayeweza kuingilia Mhimili wa Mahakama.

Akiongea Mkoani Katavi leo wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Emmanuel Nchimbi na Viongozi wengine, Makalla amesema:

“Ninaposikiliza kero Mimi nimetoka kwenye Ukuu wa Mkoa, la kwanza tutasikiliza kero ambazo hazipo Mahakamani, siku moja nipo Mbeya kuna Mtu alikuja na makabrasha akasema Mahakama ya kwanza nilishindwa, Mahakama ya Wilaya nillishindwa, Mahakama Kuu nilishindwa, Mahakama ya Rufaa nilishindwa, wewe umeteuliwa na Rais tengua hizo hukumu zote, itawezekana wapi!?”

“Lazima Watu wetu wajue mambo yaliyo Mahakamani yanamalizwa Mahakamani, tutakachokupa ushauri basi kata rufaa, tunachowasaidia Wananchi yale mashauri ambayo yanahitaji mambo ya utawala, kwahiyo ukija mkutano wa hadhara tunawakaribisha lakini usilete mambo ambayo yapo Mahakamani, ukweli lazima usemwe itakuwa tunawadanganya tu Watu kwamba hili unajua lipo Mahakamani tutakusaidia, sio kweli lazima wakati mwingine tuwe Wakweli”

Katika hatua nyingine Makalla amesema katika jitihada za kuufanya Mkoa wa Katavi uwe na umeme wa uhakika, mradi kuunganisha Mkoa huo na gridi ya Taifa unaendelea kwa kasi na sasa umefikia 56%.

“Nilikuwa natembelea mara kwa mara kwenye jenereta zetu, umeme hautoshi unakatikakatika na huku mvua za radi zikianza kila saa umeme unakatika na wakati huo unaangalia Simba na Yanga halafu umeme unakatika, ninayo heshima na furaha kusema tayari Serikali inaendele kutekeleza wa kuunganisha Katavi na gridi ya Taifa, mradi umefikia 56% na kasi ya mradi huo mtaiona ikiendelea lazima tuwe na umeme wa uhakika.”

=====

KAULI YA NCHIMBI
Upande wa Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi naye amesema:

Katika mambo tutakayoshughuliki kama kero hatutagusa ambayo yapo Mahakamani, ndio utaratibu wa Utawala Bora.

Katika kutekeleza sera za CCM, moja ya jambo muhimu ni kusimamia suala la Utawala wa Sheria, wakati wote tutakuwa tunahamasisha na kuziwezesha Mahakama kutenda haki wakati wote bila kuingilia katika maamuzi yake.

Nchi inayotaka kufanikiwa lazima isimamie Utawala wa Sheria, ukijenga utaratibu wa kuingilia Mahakama katika mfumo wa Sheria siku moja zitawaumiza wote.

Angeanza na za mahakamani tu
 
Huyu makalla kama alishindwa kuwashawishi watu elfu kumi wampe kura za ubunge hawa milioni arobaini ana muujiza gani? Katest mitambo kasikilizia mlio watu wametawanyika mkutanoni kabla ya mkutano kuisha, yaani wamemkimbia
 
Umeishia darasa la ngapi?

Unajua maana ya (Independence of Judiciary) Uhuru wa Mahakama?

Unajua maana ya Les subjudice?

Au watu waanze kukupa darasa hapa ili ujione kuwa wewe ni kilaza wa mwisho duniani?
Yaani kujua hayo ndio umejiona umesoma?? Mbona Mshamba hivyo wewe? Mimi nina Msc kutoka University of Bolton - UK, na MBA kutoka UDSM. Haya sema wewe umeishia wapi? Hako Ka-LLB ndio kanakusumbua hivyo?? Kilaza ni wewe....Umekaririshwa tu kuwa Mahakama haiingiliwi; wakati unaweza kutoa maoni kuhusu issue yoyote na kuelewesha umma - bila ya kuingilia mahakama. Kuzungumzia issue sio kuingilia mahakama; as long as hicho unachozungumza - sio kitu substance ku-affect maamuzi ya mahakama.
 
Naona mama kawekwa mtu kati. Wateule wake wa Chama wanapingana na Makonda, Makonda kipenzi cha mama. Sijui anasimamia wapi maana kuwa na serikali ambapo watu wanapingana nayo kisanga
Na hofu sana na uwezo wa maamuzi wa maza!...
 
Nadhani hiyo Ziara yao imekwenda kurekebisha na kufuta yale aliyosema Makonda!
 
Makonda alizunguka mikoa ishirini akitangaza kutatua kero, ripoti yake ilipofika kenye chama ikawekwa kapuni.

Leo karibu mkuu ameeleza umma kwamba awapo tayari kuingilia mahakama. Je, wale wananchi walioshangilia ahadi za Makonda ikiwemo zile za kupingana mahakama watasaidikaje?

Kwanini CCM imewachanganya wananchi? Viongoz kila mmoja ana msimamo wake?
---
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Amosi Makalla amesema lazima Watu wajue kuwa mambo yaliyo Mahakamani yanamalizwa Mahakamani na hakuna Kiongozi wa Serikali au Chama anayeweza kuingilia Mhimili wa Mahakama.

Akiongea Mkoani Katavi leo wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCm, Emmanuel Nchimbi na Viongozi wengine, Makalla amesema
“Ninaposikiliza kero Mimi nimetoka kwenye Ukuu wa Mkoa, la kwanza tutasikiliza kero ambazo hazipo Mahakamani, siku moja nipo Mbeya kuna Mtu alikuja na makabrasha akasema Mahakama ya kwanza nilishindwa, Mahakama ya Wilaya nillishindwa, Mahakama Kuu nilishindwa, Mahakama ya Rufaa nilishindwa, wewe umeteuliwa na Rais tengua hizo hukumu zote, itawezekana wapi!?”

“Lazima Watu wetu wajue mambo yaliyo Mahakamani yanamalizwa Mahakamani, tutakachokupa ushauri basi kata rufaa, tunachowasaidia Wananchi yale mashauri ambayo yanahitaji mambo ya utawala, kwahiyo ukija mkutano wa hadhara tunawakaribisha lakini usilete mambo ambayo yapo Mahakamani, ukweli lazima usemwe itakuwa tunawadanganya tu Watu kwamba hili unajua lipo Mahakamani tutakusaidia, sio kweli lazima wakati mwingine tuwe Wakweli”

Katika hatua nyingine Makalla amesema katika jitihada za kuufanya Mkoa wa Katavi uwe na umeme wa uhakika, mradi kuunganisha Mkoa huo na gridi ya Taifa unaendelea kwa kasi na sasa umefikia 56%.

“Nilikuwa natembelea mara kwa mara kwenye jenereta zetu, umeme hautoshi unakatikakatika na huku mvua za radi zikianza kila saa umeme unakatika na wakati huo unaangalia Simba na Yanga halafu umeme unakatika, ninayo heshima na furaha kusema tayari Serikali inaendele kutekeleza wa kuunganisha Katavi na gridi ya Taifa, mradi umefikia 56% na kasi ya mradi huo mtaiona ikiendelea lazima tuwe na umeme wa uhakika”
MAKONDA Ana ELIMU NDOGO sana yeye anadhani kila kitu kinatatuliwa na Mwanasiasa
 
Umeishia darasa la ngapi?

Unajua maana ya (Independence of Judiciary) Uhuru wa Mahakama?

Unajua maana ya Les subjudice?

Au watu waanze kukupa darasa hapa ili ujione kuwa wewe ni kilaza wa mwisho duniani?
Nimeshakwambia nilipoishia, Msc University of Bolton, UK na MBA UDSM - nimekuuliza - hako ka-LLB ndio kanakufanya ujione unajua kila kitu duniani?
 
Back
Top Bottom