Makalla atua Katavi na kusema Watasikiliza kero za Wananchi lakini siyo zile zilizopo Mahakamani

Kesi iko mahakamani unataka mwenezi aamue kama nani? Jaman majukum ya mahakama yaachwe huko huko
Kuna uozo mahakamani pia mwingi tu wananchi wakitapika nyongo zao ni wajibu wa Chama kubeba na kuyapeleka kwa jaji mkuu aone uozo wa watendaji wake achukue hatua
Makalla naye hajielewi

Akiwasikiliza atapungukiwa nini?
 
Wanazidi kujidhalilisha na kuonekana makanjanja
 
Naona mama kawekwa mtu kati. Wateule wake wa Chama wanapingana na Makonda, Makonda kipenzi cha mama. Sijui anasimamia wapi maana kuwa na serikali ambapo watu wanapingana nayo kisanga
Waende katika mikutano na Wananchi waweleze hizo habari zao ili waishie kufanya vikao vya ndani.
 
Shenzi san makala Yuko radhi kuona wananchi wanaonewa ili wao wamkomoe makondaa iko siku makonda atakuwa rais
 
Mkuu, hivi ulizo la mswalishaji umelielewa kumbe?
 
Makonda ana siasa za ulaghai,anawaaminisha watu mambo ambayo hana uwezo wa kuyafanya. Amewaingiza mkenge wengi kwa sanaa zake za majukwaani lakini katika yale aliyosema ameyapatia ufumbuzi hakuna hata moja lililokamilika,ni mhuni tu.
 
Huyu makonda atakuja kuwa kama job, maana atakosa upande. Amejichanganya sana. Mara anatetea wanyonge mara anasimama na mama yake hataki asemwe kwa mabaya. Atajikuta anaishia kujiuzulu
Wahuni siyo watu. Watamuandikia barua ya kujiuzulu na wamsainie kabisa halafu isambazwe mitandaoni.

Kisha wazee wa makotikoti watampa ulinzi wa kutokutoka nyumbani kwake
 
Kuna uozo mahakamani pia mwingi tu wananchi wakitapika nyongo zao ni wajibu wa Chama kubeba na kuyapeleka kwa jaji mkuu aone uozo wa watendaji wake achukue hatua
Makalla naye hajielewi

Akiwasikiliza atapungukiwa nini?
Kuna mipaka, si kwamba makalla hajielewi. Unae shindwa kuelewa ni wewe. Wakuu wa mikoa, wilaya, meya, mawaziri , makatibu wanakuwa na kazi gani? Mpaka chama kipeleke malalamiko?

Kuna tofauti yoyote chama na wasimamizi wakipeleka malalamiko?
 
Ili mradi Jina la Makonda litokee.

Ukiulizwa kwamba ni hukumu ili alitengua Makonda utabaki kuguna tu.

Embu tutajie hata Moja hapa.

alichoshauri Makonda ni wananchi kutokimbilia mahakamani, maana kule hukumu mara nyingi ni Mtu akijua tu kujitetea wengine wamekwisha

Na hajawahi tengua kesi ya mahakamani.
 
Watu wavivu wa kufanya maamuzi au kusaidia wananchi wako wengi mmoja wapo ni Makala. Huyu atabaki kuandika taarifa za vikao tu.
 
Wahuni siyo watu. Watamuandikia barua ya kujiuzulu na wamsainie kabisa halafu isambazwe mitandaoni.

Kisha wazee wa makotikoti watampa ulinzi wa kutokutoka nyumbani kwake
Watu wa Lema mbona mnaongea asi if watu wa suti mnao nyie. Hahaha.
 
It is very unwisse to try at this point and time to try unwind what has been winded by on Makonda. It can backfire
 
Ukitaka kujua umekosea angalia maadui zako wanavyo toa maoni kuhusu wewe!

Yani chadema hadi wanamsifu Makala 😂😂😂😂
 
Kwahiyo hawajaanza tu kutatua kero? Au kutosikiliza kero zilizoko mahakamani ndo kutatua kero kwenyewe? Ama kweli Makonda alikuwa mwamba
 
Safi sana
Naamini kweli Nchimbi ana akili.

Sio upuuzi ule uliokuwa unafanywa kwa watu kuingilia mhimili wa Mahakama as if Tanzania ni banana Republic na haina Katiba wala Sheria
Jumatatu unatajwa wewe mhuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…