Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu

Ndugu Mayalla

Naomba nikufahamishe tu kwanza kwenye harakati hamna mambo ya aliyegharamia zaidi ya mwenzake. Huwezi kusema mtu anayejiunga Chadema leo ni less entitled than Lissu au Mdee.

Ukianza mambo ya hawa wametoa jasho inamaana hata Magufuli hatakiwi awepo kwenye uongozi wa CCM maana sio katika ma comrade wa chama.

Hayo ni maneno ya kuchonganisha ambayo huwezi kuyatumia upande wa pili.
 
Pamoja na Musa kuwa mtu muhimu katika kuwatoa waisraeli utumwani, Mwenyezi Mungu alimnyima kuingia katika nchi ya ahadi kwa kosa moja tu la kiburi.

Amandla...
 
Yaani JF wangeturuhusu kufuta post za wengine naona kuna watu post zao zisingekaa hata dakika 1 ubaoni. Shwaiin...!
 
Paskali
Nimesoma kwa kituo tena kwa kurudia rudia huu uzi wako pamoja na link ulizoziweka nimeelimika kwa upeo mkubwa sana ndani ya siku moja.

Mwenyezi Mungu akutunze na kukupa afya tele.

Nitarudi tena kuusoma kisha nitoe maoni yangu kwenye hoja uliyoiweka
 
Kuwa msaliti haijalishi ulianzia wapi.. Mtu yeyote anaweza kuwa msaliti, msaliti hatoki pembeni, hutokea mulemule...
Poleni sana mliosalitiwa
Wewe je Pascal Mayala karma itakuacha salama kwa uongo mtupu unaouandika humu kila kukicha hadharani bila aibu ?
 
Mkuu Bujibuji , karma is real, kwa vile matukio mengine yamefanywa na watu wasiojulikana, karma tayari imeishawashughulikia, na kwa vile hawajulikani, hata karma ilivyoshughulika nao pia haijulikani, ila wameshughulikiwa!. Hilo la tangu enzi za Mwalimu, tusilizungumze, ila unajua waliondokaje!, that is how karma operates, haijali nani ni nani!.
P
 
Mkuu Njaa(Pascal Mayalla) endelea kukaza uzi baba kuna nafasi nane za ubunge zimebaki..
 
Kila sehemu ya uongozi wa Taasisi lazima kuwe na Ethical Standard na Responsibilit; Halima Mdee alijua consequences za kuvunja hizo ethical standard. Kamari imefanya ilivyotakiwa choosing between Justice Vs Mercy, consequences kama wangehurumiwa zingekuwa mbaya zaidi
 
Mkuu Sophist , longi sana!, nikumbujeshe ni JKT ya wapi, na huyo she wa UD ni nani, maana sisi wengine enzi hizo, foleni ni ndefu mpaka feri!, hivyo kumkumbuka mtu UDSM, kiukweli sikumbuki kuwahi kuwa na mtu UD!, unless ni zile za one night stands, hatuwekagi kumbukumbu!, na sio mbaya kama ukinikumbusha TSJ yalinikuta yepi?.
P
 
we Mzee ushamaliza yaani ,hivi ccm na chadema chama kipi kina madudu,MIMI NAKUMBUSHA MOJA TU la Dr.SALMIN AHMED SALIM basi mengine yawe kiporo.
 

Ngoja tusubiri hiyo nguvu ya Karma ifanye kazi kwa CCM waliowatuma Polisi kwenda kuwapiga mabomu ya machozi akina bibi walioko majumbani kwao mpaka kuwaunguza wao na vitanda vyao!!!!
 
Uchaguzi ulikuwa wa huru na haki au haukuwa hivyo?

Hili ni swali la msingi kabisa.
Mkuu Kiranga, hili siobandiko la uchaguzi, ila kuhusu uchaguzi wa 2020, nimeisha uzungumza sana,

sasa uchaguzi umekwisha tugange haya yaliyopo na yajayo!.
P
 
Uchaguzi hata wa 1965 unajadilika.

Mgogoro mzima umejikita kwenye uchaguzi wa 2020, halafu unasema huu si mjadala wa uchaguzi?

Swali langu dogo sana hujanijibu hapa.
 
Mkuu na wewe unataka uteuzi?
Kwanza kuteuliwa kwenye nafasi yoyote ndani ya serikali hii,sio mafanikio,ni ujambazi mtupu,serikali hii Haina moral authority maana imeingia kijambazi,
Wezi huwa hawavsmii nyumba isiyo na mali,
Kelele zote hizi zinaelekezwa kwa Chadema,mbona madudu ya ccm hamyasemi,hivi ubunge wa Mdee,usingepolwa kijambazi na ccm leo hii tungekuwa tunayaongea haya?
Gari imetibua matope,yakawarukia abilia walio kituoni,badala ya kumlaumu dereva wa gari,unawalaumu abiria.
 
Mwenzio pole pole jina limeshatajwa ongeza bidii mivyeo bado iko mingi

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Uchaguzi hata wa 1965 unajadilika.

Mgogoro mzima umejikita kwenye uchaguzi wa 2020, halafu unasema huu si mjadala wa uchaguzi?

Swali langu dogo sana hujanijibu hapa.
Mkuu Kiranga, kwa vile hoja humu sio uchanguzi bali yatokanayo, na kwenye uchaguzi nimeisha jibu sana hilo, naomba sasa tuendelee na yatokanayo.
Kina Mdee wameishatimuliwa na kangaroo court ya CC ya Chadema, maana hoja yangu ni kuhusu karma ya haya yanayofanyika sasa, then when karma hits back, nitakuwa ninawakumbusha!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…