Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu

Ukishasema hoja si uchaguzi bali yatokanayo na uchaguzi, umeshakubali uchaguzi ni hoja.

Kwa maana hakuna kinachotokana na uchaguzi kinachowezekana kuwepo bila uchaguzi.

Kwa mfano, huwezi kuwa na uchaguzi uliofanyika kwa wizi wa kura jimboni, halafu, ukapata mbunge wa jimbo hilo, ukasema huyu ni mbunge halali, hoja si uchaguzi, hoja ni yatokanayo na uchaguzi, uchaguzi umeisha.

Uchaguzi ulikuwa wa haki na huru?

Umejibu hili?
 
Kuamini karma ni ushirikina mungine uliolikumba taifa letu.
 
Labda Paskali kwa heshima ya degree yako ya sheria tueleze kisheria kwanini Kamati kuu ya chadema ambayo iko kikatiba, wewe unaiita Kangaroo court wakati ikitekeleza majukumu yake ya kikatiba, vinginevyo nitaungana na wanaokuita mchumia tumbo. Nayasema haya kwa sababu nimekuwa naheshimu sana mijadala yako tangu siku nyingi ingawa hivi karibuni naanza kupata shida kuamini kuwa ni yule yule Paskali wa miaka ya tisini na kabla ya 2015.
 
Karma ya yapi hiyo? Mungu yupo huyo au mungu wako binafsi Paskal mayala? Ujue ujinga wako ndiyo umekukosesha uteuzi miaka yote, huwezi kuja na story ndefu iliyojaa utetezi wa kiwendawazima utegee uteuzi kwa kuiga utendaji kazi wa kishetani wa polepole, kumbuka kuna wanachadema zaidi ya 400 wapo jela kwa kesi za kubambikiwa na Polisiccm kwa maagizo ya CCM na wao mdee na Bulaya walichezea kichapo cha magerezaccm hadi kulazwa sanjari na kesi kibao za kubambikiwa na utawala wa CCM iweje leo wafanye usariti kwenda kufunga ndoa na CCM kisha waachwe bila kufukuzwa kisa walipigania chama? Huo upumbavu wa kununuliwa na Ndungai ni kupigania chama? Wewe Paskal mayala ni Dalali wa Hiyo biashara haramu ya kishetani ndiyo maana umejitoa fahamu zote kutetea upumbavu wa covid 19 wanandungai.
 
Karma inakata kote kote. Na hiyo hiyo karma iwakute wote kuanzia walioagiza, waliotekeleza na wanaoficha ukweli kuhusu Lisu kupigwa risasi, yaliyomkuta Ben Saanane, viroba vyenye miili ufukweni mwa bahari ya hindi na Azori kwa kuanzia.
Ongezea orodha maana ni ndefu mno.
 
Mungu hawezi kubariki ujinga wa mdee na kikundi chake kamwe hakunaga mungu wa hivyo popote Duniani, mungu atakuja kuibariki Tanzania pindi CCM wakiacha kuubaka kuunajisi kuulawiti uchaguzi mkuu kwa njia haramu za kishetani na kuacha kuwabambikia kesi kesi uonevu unyanyasaji uovu mateso kuwapiga risasi wapinzani, mda huu mungu yupo busy kuwaonyesha CCM mapungufu yao acha kumlazimisha mungu kuibariki Tanzania wakati sasa hakuna Haki tena hakuna utawala wa Sheria katiba haifuatwi
 
Baada ya kuona Mdee, Bulaya, Matiko na wenzao wamemgwaya Mbowe na chama Chake nimetafakari na kuona kuwa chadema sio chama cha kutegemewa na wananchi tena, kama watu hao imara waliokipigqnia chama wameamua kukataa ukamdamizaji ndani ya chadema sembuse mimi na wewe mashabiki maandazi hatuna thamani yeyote.
Kina Mdee wametuonyesha njia ya uzalendo wa kweli tuwaunge mkono
 
Mungu sasa yupo busy kuwaonyesha CCM mapungufu yao kinachofuata baadae mungu atawaadhibu kwa uonevu wao wote kwa wapinzani
 
Bwega kabisa wewe MTU....hata neno Karma ulilijua tu kisa Lema alitamka.
 
Paskal mayala ni Mwanasheria kanjanja bush Loyer hana anachojua njaa ya uteuzi imemtoa fahamu zote
 
Bwega kabisa wewe MTU....hata neno Karma ulilijua tu kisa Lema alitamka.
Paskal mayala sasa anaishi kwa mdee kama marioo amekariri upumbavu wa mdee kaja nao hapa jukwaani kwa Akili zake finyu alidhani watu wamelala sasa mgoja aonje machungu ya kusaka uteuzi kifala fala
 
Kwa hiyo unataka kutuambia kwamba ukiwa ni founder lets say wa organisation yoyote ile kumbe unaruhusiwa kwenda kinyume na Policies...bila kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Paskal mayala atakuwa anavuta Bangi siyo bure
 
Wamepata walichostahili. Kama kiungo cha mwili kikibainika kuambukizwa kansa na ukaamua kutokatwa(mf.kidole) kwa vile unakipenda na utaharibu "formula",yatakayokupata ni chaguo lako.

Hao ni kansa kwa CDM! Kama ni lulu ccm wawakumbatie.Mbona mlipokea makapi mengine kama waitara,lijualikali na kadhalika? Kuondoka CDM hakuwafanyi wakose sifa ya u-Tanzania.Ila CDM hao ni outcasts! Watakaseni.
 
Wewe mwenyewe Karma inakuandama maisha yanaenda kwa shida sana,unahangaika na mapito kibao,sana sana umedata hiyo ndio lugha inayokufaa,unajaribu kujipendekeza kipindi hiki uonekane na Jiwe kwenye teuzi hovyo kabisa,mtu akikosa asiadhibiwe tena kosa la usaliti kwa vile tu alikifia chama nonsense. ukitaka na kama una uwezo wachukue wewe uanzishe nao chama kipya maisha yasonge.
 
Hivyo siyo vigezo vya ununuzi wa covid 19 kwanza ni matumizi ya pesa za walipa kodi
 
Paskal mayala anasaka uteuzi kwa njia haramu za kishetani hawezi kupata uteuzi kwa utetezi wake wa kipumbavu hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…