Ushindi wa CCM ni dhahiri kutokana na msingi imara na mipango mizuri, hayo meninge yote ni sababu tuu za kujiandaa kupokea kushindwa. Upinzani wanajua wazi imewakalia vibaya ila wanawahadaa watu waliowaaminisha kuwa watashinda. Mimi nasema CCM watashinda hata wapinzani waungane, kama huaelewi kwanini hebu jiulize...
Wakati CCM wana wanachama zaidi ya 15mil unaweza kuniambia upinzani wana wanachama wangapi? na wakati huohuo ukumbuke jumla ya wapiga kura ni mil29
wakati CCM wana wana wajumbe wa serikali za mtaa zaidi ya 97% wanaotoa elimu nyumba kwa nyumba upinzani wanafanya nini
CCM wana office kila mtaa na vitega uchumi vya kutosha kujiimarisha wakati huo wapinzani mko kulalamika tuu.
Kujenga upinzani imara inahitaji kujitoa haswa ili kujijenga na kujiimarisha. Upinzani haujengwi kwa kulalamika na kutafuta sababu za kushindwa bali kwa kuijenga misingi ya kushinda